Sunday, October 14, 2012

Kolonia Santita - Kitabu Kipya


Kolonia Santita: Riwaya ya Kiswahili ya Kijasusi Inayosisimua

 
Kolonia Santita ni shirika kubwa la madawa ya kulevya (drug cartel). Panthera Tigrisi ni mfanyabiashara wa madawa ya kulevya, katili kuliko wote katika Hemisifia ya Magharibi. Kitabu hiki kinahusu ujasusi, madawa ya kulevya na ugaidi wa kimataifa. Ukianza kukisoma hutakiweka chini kamwe unless kimeisha … 

Kitabu hiki kimetungwa na mtunzi anayekuja juu akiwa ni mjomba kabisa wa mtunzi maarufu wa Riwaya za Kijasusi Marehemu Elvis Musiba ambaye alitamba na kitabu chake cha kwanza cha 'Njama'.

Enock Maregesi ambaye anaishi na kufanya shughuli zake kwa Malkia Elizabeth anasema kitabu hiki amekifanyia kazi kwa umakini na kitaleta mapinduzi kwenye uandishi wa Riwaya za Kiswahili za Kijasusi.

“Kolonia Santita ni tofauti na hadithi zingine kwa sababu ya wapelelezi wake. Wapelelezi wake ni makomandoo-wapelelezi-wanajeshi.” www.goodreads.com

Kwa habari zaidi wasiliana na Enock Maregesi kupitia ukurasa wake wa Facebook: http://www.facebook.com/pages/Kolonia-Santita/462971887081149  au enockmaregesi.wordpress.com

Kwa wapenzi wa vitabu kaeni mkao wa kula kwani kiko njiani na kitapatikana kwenye Bookstores zote. Altenatively, kinapatikana Amazon na Authorhouse.com.

No comments: