Wednesday, February 13, 2013

Wanapinga ukeketaji wanashabikia Ushoga na Usagaji?


 
JUMATANO wiki hii nilishtuka kusikia mtangazaji wa redio moja jijini Dar es Salaam, akitangaza kuwa siku hiyo ilikuwa siku ya kupinga ukeketaji duniani!

Kilichonishtua ni jinsi ambavyo wazungu kupitia mawakala wao wa kiafrika walivyokomalia hilo tendo la  ukeketaji au tohara kwa wasichana na kulivyolibebea bango, utadhani ni dhambi kubwa kuliko zote duniani.

Wamelikomalia, kila mwaka wanatenga bajeti kubwa kupambana na tamaduni zetu za kiafrika,wakiziita za kishenzi na  sisi tunachekelea kwasababu wanatupa peremende na shanga tunaogopa kuwahoji  vipi ushoga sio ushenzi?

Wazungu wana tamaduni nyingi za kipuuzi ambazo kama ni sisi tungekuwa tunaziendekeza pengine tungeitwa wanyama tusiostahili kuitwa binadamu. 

Wanatenga siku ya kupambana na ukeketaji lakini wao ambao wameathiriwa na vitendo vya ushoga hawataki kutenga siku ya kupinga ushoga na usagaji!

Najiuliza hivi kama vitendo vya ushoga chimbuko lake lingekuwa afrika hawa wakoloni wetu wa zamani wangetudharau vipi,wangetutukana vipi?

Tulidhani kuwa ingekuwa vema wakaja kujifunza kwetu, kufanya utafiti halisi inakuwaje baadhi ya makabila ya kiafrika wanafanya tohara kwa kisu au wembe bila kutumia ganzi na kijana anavumilia halafu anapona bila kutumia dawa ya hospitali?.Inakuwaje kijana anatahiriwa kwa kisu halafu akitoka damu nyingi anapewa dawa za asili kukomesha damu hiyo na anapona  kabisa bila kwenda hospitalini kutumia madawa ya kizungu?
Hawataki kujiuliza hayo wanaoona tutapewa sifa waafrika wanatulazimisha tufuate kile wanachoamini,kwamba wao hutahiri wanaume wanataka tutahiri na sisi, kwamba wao hawakeketi wasichana na sisi  wanatuzuia. 

Sisi weusi tulizoea tendo la  ndoa hufanywa na jinsia mbili tofauti yaani mke na mme kama mwenyezi alivyoamuru lakini wazungu wamekuja na mapenzi yajinsia moja, yameendelea kushika chati katika miji mbalimbali hapa nchini.

Lakini cha ajaabu ni kwamba wakati utamaduni huo wa kishenzi ukizidi kushamiri katika shule za seminari na kwingineko mitaani, hakuna mkakati wowote wa kupinga vitendo hivyo zaidi ya kusikia wazungu wakitulazimisha tutambue haki za mashoga.

He! yaani hao watenda maovu yanayo mchukiza Mungu na jamii ya wanadamu mnaataka tuwatambue lakini wafrikakudumisha utamaduni wao kwa kufanya tohara mnawambia kuwa utamaduni wao  ni wa kishenzi.

Wafrika  wakioa wake wengi ili  kukidhi haja ya tamaa zao na kuepuka uzinzi wanaambiwa kuwa suala la kuoa wake wengi limepitwa na wakati,lakini kuwa na boyfriend au girl friend ruksa hata kama upo ndani ya ndoa!
 
Suala la kuoa wake wengi limeandikwa hadi kwenye biblia wafalme waliotukuka kama Suleiman walioa wake 700 na hata suala la kurithi ambalo wazungu wanalipiga vita kwa waafrika lilikuwepo tangu zamani.

Sisi tunapojaribu kufanya kile ambacho wazungu hawakipendi tunaambiwa kuwa utamaduni wetu ni wakishenzi wa kwao safi, hata kama wanalala na watoto wao wa kuwazaa.        
Kutokana na upuuzi huo wa kizungu leo katika safu hii nampongeza  kamanda wa Polisi  kanda maalum ya Tarime na Rorya,Justus Kamgisha na wengine waliofanya nzuri kama yeye  kuhakikisha utamaduni wetu unabaki.

Ni kweli na ni wazi kuwa mtu akitenda jambo jema anastahili pongezi akikosea, akosolewe,akiwajibishwa awajibike.
Kamanda wa Polisi wa Tarime/Rorya anastahili pongezi na tuzo ya heshima kwa watu wanaolinda na kutetea utamaduni wetu wa kifrika.
Kamanda huyo  amekataa kupokea mawazo ya kitumwa kutoka kwa mawakala wa kizungu eti azuie wakazi wa wilaya ya tarime kuwatakasa mabinti wao. 
Hiki ni kipindi kigumu ambacho dunia inapitia kuelekea katika utandawazi unaokuzwa na kuenezwa na mabadiliko makubwa ya teknolojia.
Anapotokea mtu kama Kamanda Kamgisha akapuuza amri ya mawakala wa Kizungu waliomtaka kukamata wananchi wa Tarime ambao wangediriki kujihusisha na vitendo vya tohara ya kiafrika, anapaswa kupongezwa.
Kamanda  huyo ameonyesha mfano kwa  makamanda wenzake kuwa unaweza ukatumia akiri kufikiri badala ya miguu au tumbo.
 kiongozi akifanya jema apewe shukrani zake akikosea akosolewe bila aibu, ndivyo leo ninavyoendelea kumpongeza  Kamanda huyo kwa jinsi alivyoshughulikia suala la tohara kwa wasichana wilayani tarime Mwezi Disemba Mwaka 2012.
Hicho ni kipindi ambacho mabinti wengi waliomaliza shule walikuwa wamejiandaa kutahiriwa ili kujiweka tayari kisaikolojia kwa ajili ya kuolewa ,kuposwa kwani tendo hilo huashiria pia ukuaji kimwili.
Kumuingiza kijana wa kiume au kike jando baada ya kumfanyia tohara kunamuepusha na vitendo hatarishi vya ushoga na usagaji, kwani anajitambua yeye ni nani anatakiwa kufanya nini baada ya hapo.
Kijana aliyetahiriwa kwa kisu ni vigumu kumkuta akiwa anajihusisha na utamaduni huo wa kizungu wa kugeuzana, watu wa jinsia moja kufanya yasiyompendeza Mwenyezi Mungu.
Hata hivyo licha ya kwamba utamaduni huo unasaidia kwa kiasi kikubwa kukomesha  vitendo hivyo lakini wenzetu hawapendi wakiona wanatenga fungu la pesa kuwagombanisha raia na serikali yao.   
Wanasema kamateni wote wanaojihusisha na mila hizo kwani zimepitwa na wakati,lakini hawatuambii zilipitwa na wakati kuanzia Mwaka gani.    

Ndipo taarifa zikamfikia Kamanda akitakiwa kuwakamata wale wote ambao wanafanya hivyo,bahati nzuri kamanda huyo ni mtani wa wakurya akitokea Bukoba ikabidi aone aibu akaamua kutumia busara kujumuika na watani zake katika sherehe hizo. 
Kamanda na kupongeza kwa kukataa mawazo  na fikra za kitumwa, umewaruhusu wakazi wa Tarime kuendelea na ustaarabu wao wa kutahiri watoto wa kike.

Hilo ni jambo la heshima kabisa analo stahili kufanyiwa kijana wa kiafrika kwa baadhi ya makabila hapa nchini hivyo,lisingefanyika kama Kamgisha angetumia miguu na tumbo kufikri, kutokana labda na ushawishi wa bahasha.

Nimefurahi nililiposikia kuwa Mkuu wa wilaya ya Tarime Dc.Frank Uhahura alipotoa amri ya kukamatwa wale wote waliokuwa wanakeketa wasichana kama wanavyoita wao, lakini  wewe kwa kushilikiana na vijana wako mkapuuza amri hiyo ili kudumisha amani tarime.
Busara zako, hekima zako zimedumisha amani Tarime kwa gharama ndogo, lakini kama Polisi wangedhubutu kuanza kuwakamata wale wote waliokuwa wanajihusisha na sherehe za jando amani ingetoweka na kuirejesha ingetumika gharama kubwa na umwagikaji wa damu.
Lakini kwa busara zako, Ewe Kamgisha umetambua kazi ya Polisi ni kulinda amani sio kushiriki kuvunja amani, wadau wa maendeleo ya tarime tunaamini kupitia busara hizo unaweza kukomesha mauwaji ya mgodi wa Nyamongo.

Unaweza kukaa na  wamiliki wa mgodi huo mkakubaliana namna ambavyo vijana wa Tarime wanavyoweza kuruhusiwa angalau mara moja kwa wiki kuzoa mawe yanayotupwa kama uchafu ili wao wakasafishe madini ya dhahabu kuliko sasa wanavyoitwa wavamizi.
Mnaweza kukaa mkakubaliana , eneo likaandaliwa ambalo mzungu atakuwa anakwenda kutupa mawe hayo kama dampo ili vijana waende wakaookote kule badala ya kuingia mgodini kama ilivyo sasa ili kuepuka maaafa zaidi.

Nimemalize kwa kuwapa ujumbe waafrika wenzangu hakuna utamaduni wa kishenzi hapa afrika,tunaweza kuungana na wamasai kudumisha utamaduni wetu.

3 comments:

emu-three said...

Laana kwa wale wanajihusisha na ushoga ..hivi hawo watu hawana dini, hawaikumbuki zama hiyo ya sodoma na gomora.

Anonymous said...

Makala hii imeandikwa vyema ingawa mwandishi hana elimu yoyote ya afya. Lazima kujua athari za ukeketaji na kutahiri kwa kutumia visu vyenye viambukizo.

Hakuna uhusiano wowote kati ya tohara na ushoga au usagaji. Elimu katika hilo pia ni muhimu kuzingatia. Katika utoaji wa habari ni vyema kuelimisha umma, badala ya kuandika tu.

Anonymous said...

Yuck! I mean, hiyo picha ya juu.