Friday, March 21, 2014

Mama Bishanga Asherekea Miaka Minne ya Ndoa

MAMA BISHANGA AMEREMETA/ 4th WEDDING ANNIVERSARY
 
Nawasalimu na kuwashukuru wote mlionitumia kadi, txt, na kunipigia simu kunipongeza na kunitakia heri ya kutimiza miaka minne ya ndoa yangu. Nimeona nitumie njia hii nzuri na rahisi kuwafikishia shukurani zangu na za mume wangu Mzee Marolen. Mungu ni mwema ametupa faraja amani na furaha ya kuungana kwetu sote tukiwa ni mara yetu ya pili kufunga ndoa. Kwa upande wangu sikuweza kufunga ndoa na mchumba wangu wa kwanza kwa tofauti ya dini alikuwa muislamu toka Tanga. Nilifunga ndoa mwaka 1978 na marehemu Isaya Namajojo alikuwa anafanya kazi mamlaka ya bandari Mtwara na alikuwa mcheza mpira wa timu ya Bandari Mtwara na timu ya taifa. Na mume wangu huko Johannesburg alifiwa na mke wake mwaka 2009 kwa matatizo kisukari, na tunamshukuru Mungu kwa kutuunganisha na kujenga ndoa yetu. 
 
Tunawashukuru wote watoto wetu Sizelina, Kilian na Hendrick (Kenny), Floronce, Lucy, Nuru, Ibrahim, Amri, Thato na Zinzi na wajukuu zetu, ndugu zetu, marafiki zetu na wasanii wenzengu toka Tanzania JB, Natasha, Monalisa, George/Tyson, Bishanga, Lulu, Wema na wengine wote tunawapenda sana. AND GOD BLESS YOU!
 
MAMA BISHANGA/ MRS MAROLEN
OHIO
USA

No comments: