Saturday, March 01, 2014

Rasimu ya Katiba imewashau Vijana! - Makonda

Mimi ni Kijana, ninayoyazungumza,ninayoyafanya yana reflect uhalisia huo. Hivyo kwa wito wa Ujana najikuta nashawishika sana kuongeza umakini katika masuala yahusuyo vijana hasa kwenye Katiba.

Ni ajabu lakini kweli kuwa sehemu inayotaja juu ya Haki na Wajibu wa Vijana katika Rasimu yote ni Ibara ya 44 tu, tena inataja kwa ujumla wake bila hata kuweka ibara ndogo ama vipengele vya ufafanuzi.

Ibara hiyo inasema;

"..kila kijana ana haki na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Jamhuri ya Muungano pamoja na jamii kwa ujumla, na kwa mantiki hiyo, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, serikali za nchi washirika na jamii zitahakikisha kuwa vijana wanawekewa mazingira mazuri ya kuwa "Raia Wema" na kupatiwa fursa za kushiriki kikamilifu katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni..."

Sikuwa nategemea huu unaweza ukawa ndio mwisho wa maelezo ya Rasimu kuhusu Vijana. Nilitegemea nitakuta vipengele vinavyobainisha namna vijana watakavyonufaika na rasilimali, namna ambavyo sheria ndogo na taratibu baguzi ktk upatikanaji wa ajira na fursa zitakavyobainishwa kikatiba ili kumaliza kabisa matatizo ya Vijana.

Nilidhani Rasimu itaweka bayana Uanzishwaji wa Baraza La Vijana la Taifa ili kiwe chombo cha kikatiba cha Vijana.

Nikitumia fursa na nafasi yangu kama mbunge wa bunge maalum la Katiba zipo hoja hizo kuu (3) tatu ambazo nitazisimamia ziingie kwenye Katiba kwa manufaa na mustakabal mwema wa Vijana bila kujali tofauti ya itikadi, dini ama kabila.

Na nakaribisha mawazo na michango ya fikra ktk hoja zihusuzo Vijana.

IMETOLEWA NA:
PAUL MAKONDA.
MBUNGE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA.

No comments: