Saturday, July 26, 2014

Mwimba Injili Bahati Bukuku Apata Ajali ya Gari!


 
 
 
 
Msanii wa Injili Bahati Bukuku (40) ni miongoni mwa majeruhi watatu wa ajali ya gari iliyotokea iliyotokea leo katika barabara ya Morogoro – Dodoma eneo la ranchi ya Narco Wilaya ya Kongwa .

Majeruhi wengine ni Edson Mwakabungu (31) ambaye alikuwa dereva na Frank Christopher (20).
 
Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Dodoma David Misime  ajali hiyo ilitokea saa tisa alfajiri.
 
Alisema taarifa za wahusika zinasema kwamba gari walilokuwa wakisafiria Bukuku, IT 7945 aina ya Toyota Nadia likiendeshwa na Edson Mwakabungu mkazi wa Tabata Dar es salaam liliacha njia na kugonga gema baada ya kugongwa na gari inayodaiwa kuwa ni Fuso.
 
Kamanda Misime amesema kwamba Bukuku analalamika maumivu sehemu mbalimbali za mwili huku Frank akiwa na michubuko usoni na mkono wa Kulia.
Aidha amesema kwamba watu wote hao wamelazwa  katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
 
 Kwa mujibu wa Kamanda Misime mwimbaji huyo na wenzake walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, huku Bahati Bukuku na Frank Christopher walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la injili.
 
Source: Sifa Lubasi, Dodoma

3 comments:

Anonymous said...

Bahati bukuku ni kweli alipata ajari lakini ajaumia sanaa kama watu wanavyovumisha yupo powa anaendelea vzr kabisa yani ombilangu kwenu msilazimishe uwongo kuwa kweli na unafki kwenye matatizo msiutumie kwenye matatizo ya wenzenu

Anonymous said...

pole sana bahati mungu akuponye katika jina yesu ameni, utareje na kuendele na kazi ya mungu, usihofu adui ameshidwa maadamu roho yako ingalipo.

Anonymous said...

MUNGU WA MBINGUNI AWAPONYE NA MAJERAHA YOTE .KWA UTUKUFU WA JINA LAKE.