Saturday, July 19, 2014

Wema Sepetu 'Amlipua' vibaya Kajala -

Wema Sepetu (R) na Kajala

Kutoka BONGO MOVIES. COM

Ikiwa ni siku chache zimepita baada ya mwigizaji  Kajala kudai kuwa mrembo Wema Sepeteu ni Mnafiki, hatimaye Mwanadada Wema Sepetu , amemlipua aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ‘K’ ambaye wiki iliyopita alimwita mnafiki, habari  ambayo  ilisambaa  katika  mitandao  mbalimbali  ya  kijamii.

Katika habari hiyo, Kajala alikaririwa akisema kwamba licha ya watu wengi kuamini wamepatana, hakuna ukweli kwani rafiki yake huyo ni mnafiki kufuatia kutomthamini na kutokuwa karibu naye kama zamani likiwemo suala la kumsifia mtu ambaye alikuwa na ugomvi na Kajala (Dacutee).

Akizungumza na mwanahabari wetu, Wema alisema alishangaa kuona Kajala anamwita mnafiki wakati hakuwahi kupatana naye tangu walipotofautiana kipindi cha nyuma kama alivyosema.
“Nashangaa Kajala ananiambia mimi ni mnafiki ‘ok fine’ na huo unafiki wangu unakuja pale nilipomu-wish Dacutee siku yake ya kuzaliwa, alitakaje eti? Yaani kwa kuwa yeye ana bifu la kumchukulia bwana’ke na mimi nijiingize kwenye bifu lao?

“Au tofauti zangu mimi na yeye, Aunty Ezekiel aingilie, itakuwa sahihi kweli kama wanavyofanya hao watu wake anaozurura nao siku hizi? Wanaingilia vitu ambavyo hawavijui kiundani wake? Nasema siyo sahihi kabisa mimi nitabaki kama Wema Sepetu na yeye atabaki kama Kajala Masanja na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama zamani na yeye halafu kama anamaindi kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man ambaye ana uhusiano naye aliweka picha.

BOFYA HAPA KUSOMA HABARI KAMILI BONGO MOVIES.COM

No comments: