Monday, July 14, 2014

Mwache Mzee Balali Apumzike Kwa Amani!

Jamani, nimeshangaa tangu wiki iliyopita  kuna mzozo kuwa Marehemu Daudi Balali aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu yu au la.  Mzee Balali amefariki! Ni marehemu!  Rest in Peace Mzee Daudi Balali (1942-2008)!

Kama hamwamini basi tumeni maombi ya death certificate huko alipokufa, Maryland, USA. Kama cheti haitoshi basi mlipe hela kwenda mahakamani kuomba kaburi lake lifukuliwe na mfanye testi kwenye mabaki mtakayokuta. Inaweza kuwagharamia dola $65,000!

Kuna mtu ana Twitter akaunti ya Utani! Kuna watu wameapa eti ni Marehemu Mzee Balali anayeandika!
Kaburi la Mzee Balali huko Silver Spring, Maryland, USA
Kutoka Gazeti la Mwananchi:

Mkazi wa Kijiji la Luganga, Wilaya ya Mufindi, Iringa, alikozaliwa Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali analazimika kutumia saa 32 kufika katika kaburi la kiongozi huyo lililopo eneo la Silver Spring, Maryland nchini Marekani.

Ndugu wa Ballali wanaweza kutaka kwenda kuona kaburi la ndugu yao, kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawakuwahi kupata fursa ya kumzika Gavana huyo ambaye alikuwa kiongozi wa juu kabisa wa taasisi kubwa inayosimamia masuala ya fedha na uchumi wa nchi.

Mwandishi wa gazeti hili alisafiri kwa saa 24 kutoka Dar es Salaam hadi Washington, Marekani ambako alithibitisha pasi na shaka kwamba Ballali alizikwa Mei 21, 2008 katika makaburi ya Gate of Heaven, baada ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake Maryland, Mei 16, mwaka huo.

Safari hiyo ya siku kumi, ilianza Alhamisi Juni 26, 2014 hadi Jumapili, Julai 6. Mwandishi wa habari hizi aliligundua kaburi hilo baada ya kwenda makaburi ya Gate of Heaven kwa siku tatu mfululizo.

Siku ya kwanza, mwenyeji wa mwandishi ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa alimfikisha katika makaburi hayo, lakini kaburi la Ballali halikuonekana na hata mwandishi alipokwenda siku ya pili peke yake, kaburi hilo pia halikuonekana kwa kutokana na ukubwa wa eneo hilo.

Siku ya tatu, Mwandishi wa Mwananchi alilazimika kuomba msaada wa Ofisi ya Makaburi ya Gate of Heaven, ambayo ilimsadia kuonyesha eneo lilipo kaburi hilo, hivyo kuwezesha kupata picha zake.

Kaburi lake liko katika msitari wa mwisho kabisa na Ukanda wa Kijani wa miti iliyozunguka makaburi ya Gate of Heaven, likiwa limeandikwa jina la kiongozi huyo, pamoja na maneno ya Kiingereza yanayosomeka “When the heart weep for what it has lost, the soul rejoices for what it has found”.

Maana ya maneno hayo ni kwamba “wakati moyo ukiomboleza kwa kile kilichopotea, roho hufurahi kwa kile kilichopatikana”. Kaburi hili limezungukwa na makaburi mengine kadhaa ambayo si ya Watanzania, kwani kwa haraka kutokana na mazingira yalivyokuwa, Mwandishi wa Mwananchi hakuweza kuona kaburi jingine lenye majina yenye asili au kuwa na mwelekeo wa asili ya Tanzania.

Uthibitisho huu ni tofauti na hekaya za miaka nenda rudi zilizogubika kifo cha kiongozi huyo, ambaye tangu alipoondoka nchini kwenda Marekani Agosti 2007, hakuwahi kurejea na badala yake zilisikika taarifa za kuugua kwake, kifo chake na baadaye mazishi yake yaliyokuwa ya siri kubwa yakiwahusisha ndugu wa karibu pekee.

Kutokana na mazingira hayo, kumekuwapo na uvumi kwamba Ballali hakufa na pengine amefichwa kusikojulikana, madai yanayochagizwa na mtu aliyejitokeza katika mitandao wa kijamii ya Twitter na facebook, akidai kwamba yeye ni Ballali na kwamba hajafa, huku akisisitiza kuwa wakati ukiwadia ukweli utafahamika.

Mtu huyo asiyefahamika hadi sasa alianza kujitokeza Twitter, Oktoba Mosi, 2012 pale aliposema “Nitakutana na Rais Kikwete (Jakaya) na ujumbe wake wiki hii hapa Marekani”. Mtu huyo alidai kwamba alikuja nchini Tanzania na kukaa karibu na Hoteli ya Hyatt Kempinski Kilimanjaro na baadaye kuondoka ghafla kwa kile alichokiita sababu za kiusalama.

Novemba 13 mwaka huo alituma ujumbe akisema:“In Dar es Salaam, Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kempinski Kilimanjaro Hotel. Feels good to be close to my former office, BoT,” akimaanisha kwamba niko Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, najisikia vizuri kuwa karibu na ofisi yangu ya zamani BoT.

Mtu huyo ambaye sasa tunaweza kuthibitisha kuwa ni feki amekuwa akiendelea kutuma ujumbe akijitambulisha kwa jina hilo la Ballali.

Ballali alifariki dunia kama ilivyotagazwa, lakini ilikuwaje akaenda safarini Washington, ugonjwa wake na hata kifo chake kilikuwaje? Je ndugu zake wanasemaje, safari ya kwenda Marekani ilikuwaje? Fuatilia mfululizo wa habari hii itakapoendelea kesho.Source: Mwananchi

*********

 

9 comments:

Anonymous said...

hv nyie serkali kitendo mnachokifanya kwa watz Si kizuri,Mungu atakwenda waumbua mchana kweupe,mambo ya kifo sio ya kuchezea.na mambo ya mwenyezi mungu,dhoruba litakumba serikali kwa kufanya mambo yanayokiuka utu,

Anonymous said...

Kwa nnavyoijua bongo, hii habari very likely ina link na uchaguzi mkuu ujao. Stay tuned........

BTW toka lini Balali alianza kuitwa Ballali, just asking, au ndiyo yale yale ya Martin kuitwa Martine (Kuna kipindi kalizuka sana haka katabia). Fanyeni hata research hata kwa google to kuhusu jina Balali.

Anonymous said...

Mwanzoni hata alipozikwa mlikuwa hamjui...sasa mwandishi na kampuni ya Tido kafanya utafiti wake na bado mnamdharau.

Nani alikua akijua Balali alizikwa wapi?? tuache dharau

Anonymous said...

ipo toka kuch accnt ya bilali ya twitter co mwenyewe kabisa coz ata ukiangalia twit zake zanyuma azishawishi kabisa na wakutengeneza but jama ajafaa 100% yupo!

Daniel said...

Kiongozi wa serikali kama yeye hawezi kuzikwa kama kuku.au kama mzoga wa mbwa huyu bwana bado yupo hai anakula bata.

Anonymous said...

Hii bado ni riwaya, kwa nn hataki kumtaja huyo mwenyeji anaetafuta nae kaburi la balali? Kwa nini hatujawai sikia ndugu wakisema chochote, ama kwa nini hawakuhusishwa kuonesha kaburi mana wanaotafuta hawajui liliko, eti alizikwa na familia tu!!! tangu lini kiongozi wa nchi kauguzwa na kuzikwa na familia tu wakati wakiugua mafua tu tayari ticket ya ndege mkonon kwenda huko kwa ela ya umma? Hiyo picha naeza tengeneza hata mobile box nkalipiga picha na kuliita kaburi la ballali

Anonymous said...

Tuliambiwa hadi paster hakuruhusiwa kuona mwili wa marehemu! Ballali anajulikana kuwa alikuwa ni US ASSET! aliifanyia nchi hiyo kazi nzuri sana ktk kipindi cha uhai wake! Ballali alifanikisha sera yetu ya MADINI 1998, Fedha na Uwekezaji ya 1996! Ballali alifanya economic restructuring katika nchi nyingi zilizokuwana maslahi mapana na USA zikiwemo Ghana, Nigeia et al! Ballali alikuwa one of economic Hit Men aliekubuhu! Ballali alimpokea na kumbadilisha mtazamo Benjamin William Mkapa alipokwenda Washington kuwa balozi wa Tanzania enzi zile!.. Ballali asingeweza kuuawa ama kufa kizembe kwa level na cheo chake ndani ya USA!...Tambueni kuwa USA huwa haiwapokei viongozi mafisadi!!!! Ballali kwao alikuwa na umuhimu wa kipekee! ... No hard feelings LAKINI naamini ile ilikuwa zuga tu kama ambavyo wale faya mens waliohusika na ile tukio la 9/11 walivyohamishwa na kuhifadhiwa maeneo ya Austria hadi leo! Same kwa wale wataalam wa Semiconductor waliokuwa na uwezo wa kutengeneza drones ndogo zisizoonekana ndege yao (Malasia ) ilivyotekwa na kupelekwa Kisiwa cha Diego Garcia .... Huyo Mwandishi aligharamiwa na NANI? Kwanini familia haikujua kaburi ilipo? Kweli Waandishi wetu ni makanjanja wa kutupwa!!

Anonymous said...

Iwapo ni kweli amefariki Mz Balali, basi tutakuwa tunawatonesha kidonda na kuwapa maumivu mke, watoto na nduguze.

Mwalimu said...

Naendelea kutafakari juu ya maelezo kuwa aliye kuwa Balozi wetu Marekani wakati Balali naugua , kufa , na kuzikwa Marekani, sasa ndiye Katiba mkuu Kiongozi na huyu ni Katibu Mkuu Kiongozi bila shaka anayeyajua mengi kuhusu mamabo ya siri za nchi hii. Pia hayotunayoambiwa eti maelezo ya ndugu zake ya kuwa akifa mwili wake kutopigwa picha
hasrani inatia shaka sana juu ya aina ya kifo alichokufa masikini Dr Balali, kama kweli alikufa!!! Ipo siku ukweli utajulikana hata kama wote tutakuwa tumeisha kufa au kuuliwa! Nchi hii kweli ina mambo!!