Thursday, September 02, 2010

Hurricane Earl Kilivyopiga Kisiwa cha Anguilla

Hurricane Earl kilipita nchini Anguilla mwanzoni mwa wiki hii. Kwa siku kadhaa visiwa vya Leeward Islands vilikosa umeme. Kwa bahati nzuri hakuna aliyepoteza maisha kutokana na kimbunga. Ila nyumba kadhaa zilipoteza paa zao na zingine kuaathirika kwa upepo kali na kuangukiwa na miti. Mnaweza kusoma habari zaidi HAPA:

Hivi sasa hapa Massachusetts tuko chini ya Hurricane Watch.
Mdogo wangu Malaika Che-Mponda ambaye anakaa huko ameniletea picha hizi.





Baada ya Kimbunga Earl Kupita


Paa ilitoka kwenye Stadium yao
Miti imeanguka
Hizo boti zitatembea tena kweli?
Mwenye boti kapata hasara!
Barabara ulizibwa


Jamaa aliamua kuacha ferry baharini...ilipona!

2 comments:

La Princessa said...

yani inasikitisha! love ur spot...showing some blogger love, do pass by laprincessaworld.blogspt.com. cheers!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hivi vimbunga si mchezo. Mwaka 2004 vilipita viwili hapa Florida ninapoishi na ilikuwa kasheshe nguo kuchanika. Yaani unahisi nyumba nzima kama inataka kufurushwa. Mpaka mtu unaanza kujilaumu ni kwa nini hukuwasikiliza watu wa hali ya hewa na kukimbilia sehemu salama.

Natumaini kwamba hakuna waliopoteza maisha kule Anguilla - na hilo ndilo jambo la muhimu. Kama ni nyumba na boti zao basi watanunua nyingine. Poleni!