Wednesday, August 04, 2010

Anguilla Safari Katika Picha I

Kisiwa cha Anguilla kinavyoonekana kutoka angani.

Kisiwa cha St. Maarten. Tulikuwa karibu kutua uwanja wa ndege. Njia rahisi kwenda Anguilla ni kupanda ndege hadi St. Maarten halafu unapanda boti/ferry kwenda Anguilla.
Mama Mkwe wa mdogo wangu, mimi, na Eustace. Tuliekuwa tumetoka dukani. Tulisimama kwenye kivuli cha klabu bubu. Wanauza nyama choma hapo lakini walikuwa wamefunga kwa ajili ya sikukuu.
Kisiwa cha St. Maarten kwa mbali. Hapa nilipofikia ni eneo la Blowing Point, Anguilla.
Baba yangu, Dr. Aleck Che-Mponda akipunga hewa na mjukuu wake, mpwa wangu Anguilla.
Shule ya msingi ya eneo ya eneo la South Hill, Anguilla. Ina mafeni na Air conditioning!
Hapa ni eneo la shule ya msingi. Huwezi kwenda mwendo wa kasi maana kuna matuta kila baada ya mita 20! Wanajali sana usalama wa watoto wao.
Mama akisubiri kumwona daktari. Huduma pale ni nzuri sana.
Nje ya zahanati. Mama yangu alikuwa anajisikia vibaya tukampeleka kwenye zahanati. Daktari pale ni MNigeria.
Huyo Rastaman katika kisiwa cha St. Maarten. Anasema anakwenda Anguilla kutembea kila wikiendi. Alikuwa mcheshi kweli.
Hapa napumzika kwenye veranda ya nyumba ya shemeji yangu. Huyo mbwa 'Zoe' alikuwa ananiamsha kila nikitaka kusinzia. Upepo mzuri kweli kutoka kwenye Caribbean Sea. Kwa mbali mnaweza kuon kisiwa cha St. Maarten.

3 comments:

emu-three said...

Wenzetu mnafaudu, hebu nipe siri ya hayo mafanikio, manake wengine tunakusikia tu majuu, kama ndoto za Alinacha

Anonymous said...

Tuletee picha zaidi. Safari njema.

Anonymous said...

da chemi huyo ni mtoto wa malaika?eh!mpe hongera sana!tuwekee basi picha ya malaika nimuone amekuwaje!ni siku nyingi sana!tulikuwa tunacheza wote kipindi fulani tukiwa wadogo. alikuja zanzibar michenzani (block 8)mhh looong time ago!LOL
kisses to the boy!