***********************************************************
Global Publishers wanasema Mimba ya Lulu Imetoka!
Kutoka Global Publishers:
Na Shakoor JongoULE ujauzito wa miezi mitatu wa
mwigizaji nyota wa sinema Bongo ambaye kwa sasa yuko nyuma ya nondo za
Gereza la Segerea, Dar es Salaam kwa kesi ya kifo cha Steven Kanumba,
Elizabeth Michael 'Lulu' umedaiwa kuchoropoka, Ijumaa Wikienda lina cha
kushika mkononi.
CHANZO CHAFUNGUKA
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika ambacho ni
makini, sababu kubwa ya mimba hiyo kutoka ni kutunga nje ya mfuko wa
uzazi hali ambayo ingemletea matatizo Lulu.
“Nikwambie kitu, unajua
wengi wanaamini Lulu ana mimba na hivi karibuini iliandikwa imefikisha
miezi mitatu, ilikuwa sahihi, lakini ukweli ni kwamba kwa sasa imetoka.
“Sababu
kubwa ni kwamba afya yake ilidorora, ukiachia ule ugonjwa wa U.T.I
alioripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba anao, lakini kingine
ni kuwa iligundulika ujazuito wake ulitunga nje ya mfuko wa uzazi ikawa
haina jinsi, ikabidi kutolewa na kusafishwa,” kilisema chanzo hicho bila
kuainisha tukio hilo lilitokea lini.
ETI NI MIMBA YA TATU
Kikiendelea kuzungumza kwa umakini mkubwa, chanzo chetu kilidai kuwa eti ujauzito huo ni wa tatu kuchoropoka kwa msanii huyo.
“Unajua
huu unakuwa ujauzito wa tatu kwa Lulu kutoka. Kwa kweli kama si hivyo
angekuwa na mtoto,” kilisema chanzo bila kuweka wazi nyingine mbili
zilitoka kwa matatizo gani.
“Kuna wakati Lulu alikwenda China,
aliporudi alikuwa na ujauzito, lakini nao ulitoka, inaonekana ana
matatizo kidogo kwenye upande wa kizazi,” kilidai chanzo hicho.
Kikaendelea:
“Baada ya hapo, haukupita muda mrefu, akanasa nyingine ya mwanamuziki
mmoja wa Bongo Fleva, pia hiyo nayo ikaja kutoka ya tatu ni hii ya
Kanumba.”
MAMA LULU
Katika kupata mzani wa habari hiyo, Ijumaa Wikienda
lilimsaka mama Lulu, Lucresia Karugila ili kusikia kutoka kwake lakini
hakupatikana hewani kutokana na kuzima simu.
USHUSHUSHU GEREZANI
Ijumaa Wikienda lilituma ‘mpelelezi’ wake
kwenye Gereza la Segerea ili kukutana na Lulu na kuzungumza naye kuhusu
madai ya mimba yake kuchoropoka.
Ilikuwa kazi kubwa kumpata ‘laivu’
nyota huyo kutokana na ukweli kwamba kuna watu maalum watatu ambao ndiyo
wenye ruhusa ya kumwona mtuhumiwa huyo, mbali na hao marufuku kwa
wengine.
Hata hivyo, ‘shushushu’ huyo alifanikiwa kupata fursa ya
kumjulia hali mahabusu mwingine aliyepo kwenye gereza hilo na ndipo
akapata bahati ya kuonana na Lulu ambaye alionekana kuwa mnyonge.
Baada ya salamu, shushushu wetu alimuuliza Lulu kuhusu afya yake na ya ujauzito alionao ambapo alijibu kwa mkato.
“Nani amekwambia mimi nina mimba?”
MASTAA WA BONGO WANENA
Baadhi ya mastaa wa sinema Bongo ambao
hawakuwa tayari majina yao kuchorwa gazetini, walipozungumza na gazeti
hili kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa ujauzito wa Lulu walipishana
‘kiswahili’.
Wapo waliodai ujauzito huo ulitoka akiwa gerezani,
wengine walidai ulitoka wiki moja kabla ya kifo cha Kanumba lakini wapo
waliodai bado anao.
Staa wa kiume: “Lulu hana ujauzito, ulitoka.
Ninavyojua mimi, wiki moja kabla ya kifo cha marehemu (Kanumba) ndiyo
ulitoka, kwa hiyo hana.”
Staa wa kike: “Lulu bado ana mimba ila ni siri sana. Lakini hata nyiye wenyewe si mmeona tumbo lile, anao.”
Staa
wa kike: Lulu mpaka anaingia kwenye matatizo kwa kifo cha Kanumba
alikuwa na kibendi, hawezi kukitoa kwa sasa, maana yuko gerezani.”
Lulu anatarajiwa kufikishwa Mahakama Kuu ya Tanzania Mei 28, mwaka huu ili kujibu tuhuma zinazomkabili juu ya kifo cha Kanumba.
Former Tanzanian film star Steven Kanumba's girlfriend Lulu Michaels
is rumoured to be pregnant. Lulu who was charged with his murder is now
three months pregnant. According to Tanzanian tabloids, Lulu, 17, is
reportedly carrying the late actor's baby. She has however not commented
on the pregnancy. Lulu is rumoured to have previously dated Tanzanian
Ali Kiba. They remained friends after they broke up. Kanumba’s sudden
death devastated his fans from both within and outside the country.
According
to the police, Kanumba and Lulu were fighting over calls that were
coming on her phone while she was at his home. He demanded to see the
calls and the girl wasn't ready to surrender it. While he was taking
it by force, she pushed him and he fell, hitting his head hard. She is
still in police custody as the investigations are still underway.