Saturday, April 07, 2012

Msanii Lulu Anashikiliwa na Polisi!

Msanii, Elizabeth Michael aka. Lulu (18) anashikiliwa na Polisi Oyster Bay, Dar es Salaam, baada ya ugomvi na mpenzi wake marehemu Steven Kanumba.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni Charles Kenyela, amethibitisha kushikiliwa kwa Lulu
Habari zinasema kuwa Kanumba alikuwa anajiandaa kutoka na mpenzi wake usiku wa kuamkia leo, alipokuwa bafuni anaoga akamsikia Lulu akiongea kwenye simu na mwanaume mwingine. Alipotoka bafuni kumwuliza kuhusu simu, Lulu alimsukuma kwenye ukuta, Kanumba kaanguka kufa pao hapo!  Ina maana kuwa kifo cha Kanumba umesabishwa na 'Domestic Violence'!

Mungu ailaze roho ya Steven mahala pema mbinguni.   Ameacha pengo kubwa katika fani ya sinema Tanzania.


pichani - Msanii  Elizaneth Michael aka. Lulu, ambaye alikuwa Mpenzi wa Steven Kanumba

Elizabeth Michael , aka, Lulu,  Julai 1, 2007, alipokuja kwenye audition ya Sinema Bongoland 2, aliigiza katika hiyo sinema kama, Chapati Girl
Lulu akipiga pozi hii karibuni


Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

Kuna picha nyingine ya Lulu HAPA:

Kwa habari za kilio nyumbani kwa KANUMBA MTEMBELEE KAKA MICHUZI KWA KUBOFYA HAPA:

KUSOMA SIMULIZI YA UGOMVI NA MDOGO WAKE KANUMBA ALIYESHUHUDIA BOFYA HAPA:

15 comments:

Anonymous said...

REST IN PEACE BROTHER STEVEN KANUMBA! YOU ARE GONE MUCH TOO SOON!

Anonymous said...

Oooh..! My God it pains a lot,but God loves u much than us REST IN PEACE KANUMBA

Anonymous said...

acheni kumuhukumu lulu kwa kifo hakikosi sababu na kuhusu mbo ya ogomvi yapo kwenye majumba yetu kwa wale walio owa wanajua pia na wale wenye wachumba wanajua tui iachie jamhuri.

Anonymous said...

Lulu huna jpya maninar wewe mtoto usordhk ningekuwa wewe ningetulia na huyo kanumba na kuacha umalaya ningekosa nini ufie jela m,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Anonymous said...

Kama ni mkosaji, haina haja ya kumwombea, ajiombee mwenyewe huko aliko. Atatumika balaa pande za lokap (Keko) sema angekuwa anajiheshimu tangu kitambo ingekuwa swadakta…acha maombi na sala zetu tuwekeze katika familia zetu zenye matatizo mengi zaidi ya hayo…

Anonymous said...

Kama ni mkosaji, haina haja ya kumwombea, ajiombee mwenyewe huko aliko. Atatumika balaa pande za lokap (Keko) sema angekuwa anajiheshimu tangu kitambo ingekuwa swadakta…acha maombi na sala zetu tuwekeze katika familia zetu zenye matatizo mengi zaidi ya hayo…

Anonymous said...

Haya madai eti haka ka-Lulu kalimsukuma Kanumba na kumwangusha na kusababisha kifo chake siyaamini. Hapa kuna kitu kimejificha.

Anonymous said...

Jamani watu tusi-jump into conclusions. Tasnia ya filamu Bongo imegubikwa na wivu wa kupindukia, majungu na bifu za chinichini na za wazi hasa dhidi ya watu waliopata mafanikio makubwa katika kipindi kifupi kama Kanumba. Nothing can be ruled out, including murder.

Anonymous said...

Kweli Kanumba Mwana Shinyanga kama alivyokuwa anajiitaka katika nyimbo zake kama ule wa Demokrasia.

Umetuacha mapema,bali yote ni mapenzi ya mungu.

Anonymous said...

Huyu Lulu ndiyo kwanza anamiaka 18 sasa hivi. Wakati Kanumba alikuwa na miaka 28. Na kuna picha ya Lulu hapo ya mwaka 2007, ambapo alikuwa na miaka (kama 13 hivi).

Kwanini mvulana wa miaka 28 unatoka na mtoto wa miaka 18? Na wewe msichana wa miaka 18, mwanaume yoyote mwenye miaka zaidi ya 22 unamtaka wa nini? Kwanini usitoke na mtoto mwenzako ambaye mnawiana kimaisha, kimawazo na pia katika mipango ya baadaye?

Anonymous said...

Inaskitisha sana kwakweli, lakin hatuna cha kufanya kilichobaki ni kumwombea kanumba kila la khery huko aendapo, na jamany tukae tukijua kwamba kifo hua kinatafuta sababu tu, hata kama lulu asingemsukuma bas kanumba angekufa angekufa tu, coz ndo ilikua ishafika ahad yake..lulu nakuskitikia sana ndugu yangu..pole yote maisha...just be strong..deep inside something is tellin me u didnt min to kill kanumba..u were just shocked that he heard ur conversation on the fone..

Muke Shadrack said...

Nina masikitiko makubwa mno,
Marehemu nilikuwa naye hapa Africa ya kusini mwaka wa 2010 alikuwa kama nabii nilipo muuliza maswali kuhusu wasichana ambao anawashirikisha kwa kutengeneza filamu zake aliongeya
Kama lucky Dube alivyo fariki leo furaha ya jamii ya kiafrika Steven KAnumba ametoweka.
Mungu ampumuzishe salama peponi.

Anonymous said...

Zikifika zimefika ingawa LULU ndio inaonekana ni chanzo ila hatujui humo chumbani alisukumwa au alianguka au hakusukumwa alikosa nguvu labda sababu ya uchovu hatimae mauti yakamkuta.
KATUTOKA HATUNA BUDI KUMUOMBEA WATANZANIA WOTE MAKE ALIKUWA KIOO CHA JAMII NDANI NA NJE YA NCHI.MUNGU AULAZE MWILI WA MAREHEM PEMA PEPONI AMINA

Anonymous said...

Kweli siku ikifika,sababu kidogo tu,lulu unajuta now!yamekukuta mazito,bado mdogo wewe,tunajua ni bahati mbaya hukudhamiria ila serikali hawatambui hilo mama,kuna manslaughter serikali haijui sheria ni ngumu hapo utachukuliwa hatua! RIP kanumba..pole sana lulu mazito yamekukuta

Anonymous said...

Kweli siku ikifika,sababu kidogo tu,lulu unajuta now!yamekukuta mazito,bado mdogo wewe,tunajua ni bahati mbaya hukudhamiria ila serikali hawatambui hilo mama,kuna manslaughter serikali haijui sheria ni ngumu hapo utachukuliwa hatua! RIP kanumba..pole sana lulu mazito yamekukuta