Wednesday, November 21, 2007

Dokta aliyempasua mama yake Kanye West amkimbia Larry KingMama yake mzazi Kanye West alifariki dunia majuzi baada ya kufanyia opresheni ya urembo. Opresheni eneyewe ilikuwa ya kupunguza matiti (breast reduction), kupunguza nyama kwenye tumbo (tummy tuck) pamoja na kuondoa mafuta (liposuction). Daktari mwenyewe ni Dr. Jan Adams.

Navyoona walimfanyia huyo mama opresheni nyingi kwa mpigo. Kawaida wangefanya moja wasubiri, wafanye nyingine, halafu wasubiri tena. Lazima alikuwa na maumivu makali.

Kanye West mwenyewe amesema alikubali kulipa gharama za hiyo opresehni lakini alitaka mama yake aende kwa trainer. Alisema kuwa mama mwenyewe alisisitiza kuwa alitaka hiyo opresheni.

Jana Dr. Adams alialikwa kwenye show ya Larry King ili ajitetee. Alikaa dakika moja halafu alikimbia. Baada ya kifo cha mama Kanye, utalaamu wake wa kufanyia opresheni za urembo ulianza kuchunguzwa na bodi ya madaktari. Pia iligundulika kuwa Dr. Adams, alikamatwa na polisi akiwa anaendesha gari amelewa.
Pia baada ya kifo cha mama Kanye, wanawake wengi walijitokeza kulalamika juu ya huduma anayotoa. Wengine wanasema kuwa Dr. Adams aliwacheka baada ya kulalamika mfano matiti yameenda upande! Mwingine anasema alienda kwa Dokta mwingine na kukutwa kuwa Dr. Adams aliacha sponji ndani!
Unaweza kuona Video ya Larry King hapa:

Dr. Donda West alizikwa kwao Oklahoma City jana.

4 comments:

Anonymous said...

huyo mama alikuwa na miaka 58! Alitaka apunguze matiti na tumbo ya nini? Alipata BF nini? Angefuata ushauri wa mwanae angekuwa hai!

Anonymous said...

Huyo daktari ni tapeli hebu fanya search kwenye neti! Yaani Kanye hakumchunguza au aliona anampa kazi mweusi mwenzake!

Anonymous said...

Huyu Dokta sijamuelewa kabisa dhumuni lake lilikuwa nini?Kama ni kuelezea tu na kutotaka kujibu aswali si angetoa statements na sio kufanya alichokifanya..

Concord

Anonymous said...

huyu dokta safi sana huyu. anatakiwa awafundishe madokta wenzake utekelezaji wa mipasuo ya urembo.