Wednesday, December 12, 2007

Aftershock Beyond the Civil War
**********************************************************************************

Jamani msishangae sana. Huu ni mguu wangu! Na bado niko hai. Nilikuwa naigiza katika sinema ya 'Aftershock:Beyond the Civil War' kama Field Hand. Hao field Hands walikuwa ni watumwa walioachiwa huru lakini bado walikuwa wanaishi katika hali ya kitumwa baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe (Civil War) 1865. Wakati wa filiming tulikuwa peku kwenye matope! Sinema ilipigwa mwezi wa sita na wa saba hapa Massachusetts.

Hiyo make-up ya damu feki ilipakwa kwenye mguu baada ya kulala chini! Nakumbuka Director David Padrusch anamwambia make-up lady, ongeza, ongeza damu haitoshi! Ai! Walinipaka mwili mzima. Niliona kinyaa maana hiyo damu feki inaonekana kama damu kweli. Na usoni pia nilipakwa madamu na majeraha, ilikuwa tuonekana kama tumepigwa risasi nyingi. Ni kwamba weusi wengi waliuliwa na wazungu wenye hasira baada ya hiyo vita

5 comments:

Anonymous said...

Hivi ndio ile sinema ulituambia ulionekana umechelewa uwanja wa ndege?

Chemi Che-Mponda said...

Hapana hii ni TV show. Hapa nilikuwa mtumwa aliyeachiwa huru baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe hapa USA 1866. Ile ya ndege ni Pink Panther 2, itatoka 2009.

Ilham said...

Chemi ,mbona nikiclick kucheki video haiji?

Chemi Che-Mponda said...

Samahani, hiyo ni picha siyo linki.

jaribu hii:

http://www.youtube.com/watch?v=ApV1PvLH0jU

[url]http://www.youtube.com/watch?v=ApV1PvLH0jU[/url]

ilham said...

Duu imenigomea pia.Akhsante.