Monday, December 17, 2007

Mbunge Mwingine aaga Dunia!


Mwaka huu wa 2007 umekuwa mbaya kwa Bunge. Leo nimepokea kwa masikitiko habari ya kifo cha Mbunge wa Kiteto, Mheshimiwa Benedict Kiroya Losurutia.

Habari kutoka ippmedia.com zinasema kuwa: Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na ofisi ya Bunge, marehemu Lusurutia amefariki jana katika Hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kusumbuliwa na maradhi ya figo, kisukari na shinikizo la damu.

WaBunge wengine waliopoteza maisha mwaka huu ni Bw. Juma Akukweti (Jimbo la Tunduru), Amina Chifupa (Viti Maalum - CCM) na Mhe. Salome Mbatia, aliyekuwa pia akishikilia nafasi ya kuwa Naibu Waziri wa Wanawake, Jinsia na Watoto.

1 comment:

Anonymous said...

http://www.dalianmitmita.com