Wednesday, December 19, 2007

Wapiga Picha wa enzi zile!

agosti, 1985: *mwalimu nyerere akila pozi na paparazi wa enzi hizo. toka shoto juu ni *max madebe (mfanyakazi), *sam mmbando (shihata), *vicent urio (daily news - huyu ndiye kanifundisha kazi), *mzee makwaia (maelezo), mwanakombo jumaa (maelezo) juma dihule (shihata), mzee nanihii (maelezo), adinani mihanji (shihata) na john lukuwi (maelezo)
chini toka shoto: mdau simfahamu, charels kagonji (shihata), boaz mpazi (shihata) moshy kiyungi (maelezo) na raphael hokororo (maelezo). wenye nyota * wote ni marehemu
******************************************************************************

Kabla ya Michuzi. Hao ni baadhi ya wapiga picha maarufu wa Tanzania. Huyo Boaz Mpazi alikuwa ni mchapa kazi kweli kweli na mwenye moyo wa kazi.

Mzee John Makwaia alipiga portrait kadhaa 'official' za Mwalimu. Pia alikuwa mwalimu wangu wa Photography nikiwa nasoma TSJ. Kwa bahati mbaya aligongwa na gari Morogoro Road maeneo ya Magomeni 1989. Alikufa papo hapo. Tulikosa mwalimu mzuri sana.

Vincent Urio alikuwa mpiga picha mkuu wa Daily News kwa miaka mingi. Alienda kwenye vita vya Kagera. Wengine walioenda kwenye vita ni Juma Dihule na Ben Kiko. Alivyorudi alikuwa analalamika kichwa kinamwuma na alishindwa kufanya kazi vizuri. Alistaafu na aliaaga dunia si muda mrefu baada ya kustaafu. Mzee Urio anaigiza kama Baba Mariamu katika sinema, Arusi ya Mariamu.


1 comment:

Anonymous said...

Huyo mzee John Makwaia ndiye baba wa Makwaia wa Kuhenga?