Friday, December 21, 2007

Jamie Lynn Spears ana mimba! Ana miaka 16!


Bila shaka mmesikia habari za huyo binti Jamie Lynn Spears, ambaye ni mdogo wake Britney Spears. Ana mimba na ana miaka 16 tu. Baba wa mtoto Casey Aldridge, ana miaka 19. Anatoka Mississipi. Sehemu zingine hapa USA hiyo ni kosa la jinai kumtia mtoto mimba, na angeitwa sex offender.

Jamie Lyyn sasa anaitwa, kila jina chafu ya kiingereza ambayo unaweza kufahamu ya neno malaya. Kaitwa tramp, whore, ho, slut, skank. Wanasema ni nyege mwasho kama dada yake Britney.

Familia yake wametukanwa kuwa ni wazungu wasio na thamani. Wameitwa Cracker, white trash, trailer trash, bayou swamp trash, washamba, inbred (kuzaana wenyewe kwa wenyewe katika ukoo) doh! Wanasema "The apple doesn't fall far from the tree" ( Yaani tuna la apple haianguki mbali na mti wake). Yaani sikujua kuwa wazungu wanaweza kutukanana hivyo!

Wamekasirika kwa sababu Jamie Lynn Spears ni mdogo wake Britney Spears. Jamie Lynn ana TV show kwenye Nickolodeon inaitwa Zoey 101. Wasichana wanaipenda kweli na wazazi wengi walimwona kama mtu wa kumwiga. KUMBE!

Halafu alikuwa anajifanya ni Mkristo mwema. Mtakatifu hawezi kuvunja amri za Mungu. Yaani awe bikira mpaka siku ya kuolewa. Sasa hiyo mimba inaonyesha watu alikuwa anafanya nini. Inatoboa siri, hakuna cha ubikira hapo.

Na jambo la kuongeza chumvi hapa. Mwezi wa saba gazeti la National Enquirer walitoa stori kuwa huyo binti ana mimba. Nickolodeon walitafuta mawakili na kuandika barua kali kuwa watawa-sue kwa ajili ya kuchafua jina la binti mwema, Mkristo safi kama Jamie Lynn. Sasa inaelekea huenda hiyo habari ya mimba ilikuwa ya kweli na aliitoa.
Sasa watu wanasema kuwa Nickolodeon ni wanafiki maana angekuwa ni msichana mweusi show yake ingesimamishwa mara moja. Lakini wameruhusu iendelee kuonyeshwa.

Mama yao alikuwa anaandika kitabu kuhusu malezi bora. Publishers wa hicho kitabu wamesimamisha mkataba waliokuwa naye maana inaelekea hawezi kumlea mtu.

Karibuni mtoe maoni hapo.

Kwa habari zaidi someni:



6 comments:

Anonymous said...

Wakati mwingine tukitazama hali ya kwetu huwa tunapiga kelele sana kuhusu suala la watoto kuzaa, hasa sie tulio ughaibuni, huwa tunaona kama huku ughaibuni ni kila kitu na kudharau kabisa mambo ya kwetu. Kuna watu wanadhubutu hata kusema maneno machafu kuhusu kwetu. Lakini hili limethibitisha kuwa angalau kulingana na mila na desturi zetu sie tuna nafuu kidogo. Watoto wanafanya hayo mambo lakini kwa uficho.

Pili umeonyesha wale wazazi wenzangu wanaoona kuwa kila kitu cha mzungu ni kizuri na cha kukikumbatia kuwa hali hiyo siyo kweli yapo ya kuchukua na kuchuja. Watoto wengi huko Dar wanawaiga wamarekani kwa kuwa ni maendeleo na wazazi wanafurahia watoto wao kuwa Americanized, sasa hili la mdogo wake na Britney, jamie Lynn sijui watalipokeaje, kuwa ni ajali kazini? Nashukuru Mungu hali imeonyesha kuwa hata wamarekani wenyewe hawapendezewi na hali hiyo na sijui sie tunaoiga tunapendezeshwa na nini?

Ukienda shule za sekondari za kulipia na hata za serikali zilizopo Dar ndio utaona hali halisi ilivyo vitoto vidogo vya 13 na 14 vina boyfriends na wazazi wanafurahia, hao wa umri wa 16 ndio wamekubuhu na wazazi wanachekelea sie tunaoona vibaya tunaonekana washamba. Haya sasa na wamarekani nao wamekuwa washamba?

Haya si ya kucheka au kumcheka mtu midam nasi tuna watoto wa kike, ni kukazana na maadili ya dini na tamaduni zetu hata kama tuko ughaibuni, tusijisahau kuhusu suala la malezi na kumuomba mungu sana ili atuepushe na hayo maana na haya maradhi ya zinaa ni hatari tupu.

Anonymous said...

Hiyo familia ya Spears imelaaniwa. Huyo Britney amaenyanganywa watoto wake kwa vile hawezi kuwalea. Anatembea bila chupi na kuonyesha paparazi watoto wametoka wapi. Sasa huyo mdogo wake alikuwa na mfano wa kuiga huyo Britney anayopenda umalaya. Na kumbuka kusikia hiyo kesi ya Julai kuwa ni mtakatifu sijui malaika sijui nini. LOOOOO!!!

Anonymous said...

Hayo ni matokeo ya kuvaa nguo fupi!

Anonymous said...

Chemi hiyo terminology uliyotumia ya "nyege-muwasho" imenichekesha hadi nimepaliwa!!!

Anonymous said...

Nyege mshindo mavyakula wanayokula.ukimwi kapima kama mimba iliingia hakutumia condom

Anonymous said...

Hakuna haja ya kushangaa kuwa binti wa miaka 16 ana mimba, huku nyumbani TZ kuna wanawake/binti wangapi vijijini kwetu wanapata mimba katika umri kama huo au wakati mwingine chini ya hapo. Aliachia alifikiri anapanda nini???