Friday, October 09, 2009

Rais Obama Ashinda Tuzo ya Nobel (Amani)

Rais Barack Obama ameshinda tuzo ya Amani ya Nobel (Nobel Peace Prize). Hiyo ni tuzo enye heshima kubwa sana duniani. Watu wengi hapa Marekani wamepigwa butwaa maana wanasema kuwa hasthili kupewa. Wengine wanatania kuwa eti kapewa shauri ya kusuluhisha ugomvi kati ya Prof. Henry Louis Gates, Jr. na polisi Sgt. Jim Crowley hapa Cambridge, MA.

Wanakamati wa Nobel wanasema kuwa Rais Obama alichaguliwa shauri ya bidii yake ya kupoza chuki kati ya Marekani na nchi za KiIslamu.

Wengine waliowahi kushinda ni: Al Gore, Jimmy Carter, na Martin Luther Jr.

Kwa habari zaidi someni:

http://edition.cnn.com/2009/WORLD/europe/10/09/obama.nobel.international.reaction/

http://freakonomics.blogs.nytimes.com/2009/10/09/a-little-soon-for-the-nobel-peace-prize/

4 comments:

Anonymous said...

Obama angekuwa mzungu wangekuwa wanamsifu! Kazi nzuri Rais Obama Keep it Up!

Anonymous said...

it is true kuwa hastahiki kupewa. ilikuwa wasubiri angalau miaka 2 ndio wampe. hii ni upendeleo wa wazi. hata mkewe kuwa ni no1 katika orordha ya wanawake ambao ni powerful duniani ni kupendelewa tu. siku hizi hayo mbambo ni biashara.

mbona hawajampa rais kikwete? rais kikwete anastahiki kwa sababu zifuatazo:#

1. amesuluhisha mgogoro wa comoro.

2. amesuluhisha mgogoro wa kenya baada ya uchaguzi.

3. akiwa kama mwenyekiti wa au amechangia kusuluhisha mgogoro wa zimbambwe.

4. pia amechangia kusuluhisha mgogoro unaoendelea wa madagascar nk nk.

lakini pia tanzania ina dk salem ahmed salem ambae amesuluhisha migogoro lukkuki siyo na idadi mbona hajapewa hiyo tunzo. ni wizi mtupu.

John Mwaipopo said...

hili jamaa lichawi nini?

SIMON KITURURU said...

@John: Komenti yako imenivunja mbavu!:-)