Wednesday, October 07, 2009

Victoria Rowell Avaa Kitenge Kwenye Emmy Awards

Wadau, mcheza sinema Victoria Rowell, alivaa gauni ilishonwa na kitenge kwenye tuzo za Emmy Awards hivi karibuni. Kitenge chenyewe kilikuwa na picha za Rais Obama. Basi hiyo gauni imezua zozo! Kuna watu wanasema kuwa eti Rais Obama ametukanwa kwa vile picha yake iko kwenye kitambaa. Hao wanaosema hivyo hawalewi kuwa ni sifa kuwa na picha yako kwenye kitenge barani Afrika!

Wengine wanasema eti Victoria alionekana kama kajitundika kitambaa cha mezani (Tablecloth). Wengine eti ni kama blanketi. Kuna waMarekani weusi ambao wamesema kuwa wameona aibu kwa vile kavaa nguo ya kiAfrika! Heh!

Mimi namsifu Victoria kwa kupenda uAfrika na kutangaza Afrika na mila yake! Weusi waMarekani wamepoteza uAfrika wao na mila zao za kiAfrika kutokana na utumwa. Nashukuru kuna weusi wanaopenda weusi wao.

VICTORIA, YOU GO GIRL! BIG UP ON YOUR BOLD MOVE!

Kwa habari zaidi someni:

http://www.starsareblind.com/2009/09/21/victoria-rowell-emmy-dress/

http://blackpoliticalthought.blogspot.com/2009/09/actress-victoria-rowell-wears-obama.html

1 comment:

chib said...

She looks so lovely on that dress