Friday, June 18, 2010

Mnakumbuka East African Airways?
Wadau hapo zamani za kale kulikuwa na shirika la ndege East African Airlines. Ilikuwa sehemu ya East African Community. Waliokuwa wanakmiliki ni Tanzania, Kenya na Uganda.
Mwaka 1971, familia tulisafiri Mbeya hadi Dar na ndege ya East African Airways. Ilikuwa Prop Job kama ile kwenye picha ya kati kati. Tulikuwa tunatoka kijijini Manda kwa ndugu wa baba. Mkikaa kwenye kiti kama vile mnatazama hewani, halafu ilisha ruka ndo mnakuwa sawa. Ingawa nilikuwa na miaka saba nakumbuka waliwapa aibiria lunch box. Mwaka 1976 tulisafiri na ndege 727 Nairobi -Dar. Haikuwa mbaya. Pia tulisafiri na treni, lakini jamani zilikuwa safi na wenye wahudumu waliopenda kazi yao.
Nakumbuka nikiwa Form One mwaka 1977, ghafla shirika hiyo ilivunjwa. Waliokuwa na mali (treni, ndege, mabasi) kwenye nchi yao ndo ilikuwa mali yao. Wakati ule damu ulikuwa mbaya kweli kati ya WaTanzania na WaKenya.
Mwalimu shuleni alitusimulia hivi, waKenya walivizia siku ambayo ndege kubwa na nzuri zitakuwa zimetua pale Embakasi airport Nairobi, ndo wakazizoa na kuita Kenya Airways! Tanzania tuliambulia zile Fokker Friendships na ndege nyingine 737 ikawa Air Tanzania, halafu Uganda walikuwa wazembe eti walipata ndege moja tu! Ikawa Uganda Airways.
Lakini jamani nakumbuka watu walikuwa na huzuni kubwa mno jumuiya ilivyovunjika. Mbaya zaidi watu wakawa wanyama. WaTanzania walifukuzwa Kenya kama mbwa. Hasa hao waliokuwa wanafanya kazi na East African community. Wengine walirudi Tanzania kwa mguu na begi moja!
Wenye stori za wakati ule hebu mtupashe.

4 comments:

Anonymous said...

alafu wana taka tuungane tena wazimu mtu

Anonymous said...

Enzi zile walikuwa wachapa kazi, hakuna hongo kupata tiketi! Mambo fresh. Service with a smile.

Anonymous said...

Wee acha tu wala usitukumbushe hayo maumivu, nakumbuka marehemu baba yangu na baba yangu mdogo walivyokuwa hawana tena pesa kwa sababu upande wa TZ hawakulipwa mafao yao. Vile vile nakumbuka tulivyokuwa tunakula na kuvaa vizuri wakati baba yangu akifanya kazi EAC, ukizingatia angalau alikuwa na elimu ya sekondari ya Mkoloni (alisoma Tabora boys) basi maisha yalikuwa poa kweli. Sasa kibembe jumuia ilivyovunjika tuliachwa weupe, na kuanza kujua njaa maana yake nini, na nguo za kushonwa na cherehani sio za kutungua dukani kumbe ni nzuri. Nasikia pesa za mafao za wazazi wetu zilitumika kwenye vita vya Uganda ili kumtoa Iddi Amin, wakati sie tulikuwa tunakula kwa tabu na maisha kuwa magumu kweli kweli halafu leo ati nasikia Nyerere ataka kuwa mwenye heri, mwenye heri! Atuombe kwanza msamaha kwa kuwadhulumu wazee wetu haki zao, kutumia pesa zao kwa mambo mengine ilhali familia zikipata tabu!

Baba mdogo alioa mwanamke wa Mombasa basi kitim tim kile wakarudi Tanzania, maisha ya Mombasa na Tanzania yalikuwa na tofauti kubwa, siku moja ikaletwa kesi nyumbani mke wa bamdogo kamwaga sufuria ya maharage barabarani kwani haelewi kwanini maharagwe yanakuwa mboga. Akawa anamuuliza mama ati maharagwe nayo ni mboga? (hapo ni 1978, mimi nina miaka 11)Ugomvi ukawa mkubwa kweli kweli kumbe masikini mama wa watu alipata depression mwishoe ugonjwa ukazidi akawa kama kichaa wakamrudisha kwao Mombasa Kenya, akaondoka na watoto wengine mpaka leo hatujuani tena, na wala hatujui masikini ya mungu kama yu hai au alikufa.

Mimi sitaki kabisa kusikia haya mambo ya Jumuia ya sijui nini wala nini, mpaka baba yangu ameingia kaburini hajalipwa haki yake na mpaka hivi leo wajanja wamekula pesa yake, lakini midamu ilikuwa jasho lake basi watamlipa tu hata siku ya hukumu, siku watu watakapokutanishwa kufanyiwa mahesabu yao na hakimu wa kweli asiyehongwa na asiyependelea mtu, siku tutakaposimama mbele ya Mungu watamlipa baba yangu jasho lake! Kwani jasho la mtu haliliki.

Anonymous said...

Mdau wa june 19 12.09pm pole sana kwa yaliyo kukuta hawa Wakenya siyo watu wazuri hata wenyewe kwa wenyewe hawapendani wana roho mbaya sana.Kuhusu tatizo la mafao ya E.A.C. siyo kweli kama serikali ilitumia kwenye vita kwani kila kitu kilibaki Kenya sasa hiyo serikali ya Nyerere ilipata wapi pesa za mafao wakati mipaka ilikuwa imefungwa na hakuna mawasiliano yoyote baina ya nchi hizi mbili? Usisikilize maneno ya mitaani ongea ukiwa na uhakika.Hata hivyo mbona nimesikia wastaafu wa E.A.C. wamelipwa mafao yao miaka ya karibuni?Nakama wamefariki wamepewa warithi wao wewe hukupewa? watu wamepata pesa nyingiHii inamaanisha serikali ya Nyerere haikuzitumia kwenye vita. Kama alvyosema Mwalimu Nyerere hawa watu ni manyang!au ni kweli kwanza wao hawana ardhi kwa hiyo watamiliki ardhi ambayo Mtanzania mwenyewe hana.Viongozi wetu acheni uroho kwa kuiuza nchi yetu kwa kipande cha mkate. Lazima muangaliena mlinde malizetu kwaajili ya kizazi kijacho. Atakayefaidika na E.A.C. ni wakenya tu na safari hii watatunyanyasa kwenye nchi yetu. Angalao 1977walitufukuza kwao tukarudi kwetu sasa hivi sijui tuta kwenda wapi.Wadau vijana wetu na wasomi naomba muliangalie suala hilo na inelekea serikali itaupitisha muswaada huu bila kujali maslahi ya wananchi.