Friday, June 18, 2010

Mzungu aua Familia Yake na Mama Mkwe wake Hapa Boston!

Wadau, kuna mzungu ambaye kaua familia yake, mke wake na watoto wawili nyumbani kwake katika mji wa Winchester, Ma. Kwa kawaida nisingebandika habari ya tukio. Ila kinachonikuna ni kuwa watu wanasema kuwa mambo kama hayo (mauaji) hayatokei katika eneo kama Winchester ambako wanakaa wazungu tajiri, wenye maana, wema etc. eneo hauijachauliwa na weusi, minorities.

Huyo baba ameua hata mtoto wake mdogo mweye miaka miwili akiwa amelala katika crib yake. Sijui aliingiliwa na shetani! Kwenye taarifa wa habari walisema kuwa jamaa atapimwa kuona kama ana kichaa.

Yaani utacheka ukisikia kwenye taarifa ya habari watu wakisema, "That kind of stuff doesn't happen here!" Maana yao ni kuwa ni kazi weusi na waspanish kuana huko mjini kwenye ghettos!

Habari haijakamilika lakini inaelekea kuwa huenda mauji yalisabishswa na ukosefu wa fedha. Mmmh, uongo mbaya, lakini uchumi ukiwa mbaya, sijui kwa nini wazungu hawawezi kumudu na kushusha zile living standards zao. Utasikia wanaua famila au wamejiua. Kama vila wakati wa Great Depression miaka ya 1930's, wazungu walijiua wengi kweli kweli na kuua familia zao baada ya kuptoza hela yao!

Mungu alaze roho za marehemu mahala pema mbinguni. AMEN.

Mnaweza kusoma story HAPA:

http://www.boston.com/news/local/breaking_news/2010/06/_the_43-year-ol.html

1 comment:

Anonymous said...

doh mbona yapo kila cku! mswaili akikosea tu media hao wamepata nafasi ya kuuza ilaa mimi najuaa kwamba mtu ambae hamchaa mungu ni mnyaaama wa kuogopa kabisa.mimi hapa nakoishi makaburu matupu waweza tembea cku nzima hujamuona mswaili ilaa zamaa kune mirembe spitali zao uone wazungu watupu vichaa hao wanaa laana za ukubwani na kizazi chao waache waangamizane wehu wakubwa hao.

mdaui chabiki wa malema