Saturday, January 15, 2011

Rais wa Tunisia Akimbia na Kuacha Madaraka!!

Rais Ben Ali

Duh! Yaani zamani ilikuwa kawaida kusikia rais kapinduliwa na damu imemwagwa. Yule Sylvanus Olympio wa Togo aliruka geti ya ubalozi fulani kabla ya kupigwa risasi. Thomas Sanakara wa Burkina Faso alipiwa risasi usingizini. Sasa inaelekea kuna mtindo mpya, kupanda ndege na kutangaza hutarudi nchini kwako.

Rais Zine El Abidine Ben Ali, aliyeongoza Tunisia katika siasa za Chama Kimoja kwa miaka 23, hivi sasa yuko Saudi Arabia ambako inasemekana amepokelewa kwa shangwe na mfalme wa huko. Awali alikimbilia Ufaransa lakini walimrudisha wakisema hawamtaki. Tunisia ilikuwa koloni ya wafaransa.

Siku za hivi karibuni wananchi wa Tunisia walichachamaa kutokana na hali mbaya ya uchumi na ukosefu wa ajira. Walichochewa baaada ya mwanaume ambaye alikuwa msomi lakini kashindwa kupata kazi, alijichoma moto baada ya polisi kumnyang'anya kigari chake ambacho alikuwa anatumia kuuza matunda.

Tunisia iko Afrika Kaskazini. Wananchi wake wanajiita waarabu.

Kwa habari zaisi someni:

http://edition.cnn.com/2011/WORLD/africa/01/15/tunisia.protests/

1 comment:

Anonymous said...

Hakuna anayeweza kushinda nguvu ya umma. Huyu pamoja na utajiri wake na kuwa na jeshi linalomtii aliikimbia nchi usiku baada ya kugundua kuwa wananchi hawamtaki tena baada ya kuwatawala kwa mabavu kwa miaka 23.