Tuesday, July 26, 2011

Vyombo Vya Habari USA Vinaagusha!

(Maombolezi Norway)


(pichani Amy Winehouse kabla na baada ya kuwa mlevi kupindukia)



Hapa Marekani naona hao Stars waimbaji na waigizaji ni kama Miungu Midogo. Watu wanawaabudu mno. Nimebahatika kukutana na Stars wengi na lazima niseme ni binadamu kama sisi ila tu wana hela zaidi, wanajulikana zaidi.

Nasema hivyo, kwa sababu nashangaa vyombo vya habari vya hapa USA! Habari kuu ni kifo cha yule mwimbaji mlevi wa Uiingereza, Amy Winehouse (27)! Ile habari ya mshenzi kuua watu karibu mia huko Norway ni habari ndogo sana! Khaa! Maiti ya Amy imechomwa moto leo (Cremation). Lakini bado tutaenedelea kusikia habari zake na jinsi alivyoingia 27 Club (yaani klabu ya waimbaji maarufu waliokufa wakiwa na miaka 27 wakiwemo Jimi Hendrix). Je, ile habari ya kuwa baada ya wiki moja serikali ya USA haitakuwa na pesa je?

Kwanza, watu wengi walitabiri kuwa huyo Amy Winehouse atakufa kabla ya wakati wake. Alikuwa mlevi wa pombe na madawa ya kulevya bila haya. Mnafahamu wimbo wake, 'Rehab' ambao ana kashifu kwenda kwenye Rehab (hospitali/kliniki za walevi kupona ulevi wao).

Sasa huyo jamaa wa Norway, ni Mzungu, Anders Behring Breivik (32) ukiona picha yake watu wanasema handsome anafaa kuwa modo, lakini mimi namwona kama wale Aryans wa Hitler! Ni mzungu mwenye itikadi kali ya Kikristo (Christian Fundamentalist) lakini hapa Marekani zaidi wanastahili kumwita White Supremacist (yaani mzungu anaona kuwa Uzungu na ngozi nyeupe ndo wanaostahili kuishi dunia hii).

Ina maana kuwa, huyo mzungu angekuwa hana sura nzuri, au angekuwa si mzungu, angekuwa mwislamu ingekuwa habari ya maana zaidi? Watu 76 wamekufa, ile si habari kubwa? Bila shaka watasema kuwa wanataka kuuza magazeti na watu watapenda zaidi kusikia habari ya kifo cha Amy Winehouse. Wanajuaje?

Mungu alaze roho za waliokufa mahala pema mbinguni. Amen.

11 comments:

Anonymous said...

My God! She looks jaundiced! Drugs will make you old and ugly before your time!

Anonymous said...

Dada Chemi,wewe umekaa sana America na labda hata kuwaona hao Idols sasa nashangaa kuona unaandika the obvious! Marekani ni taifa linaloabudu Heros au Idols! Hivyo magazeti yanaandika kile jamii inaamini!na kile ambacho jamii inakipa kipau mbele.

Halafu unaposema kuwa huyo muuaji wa Norway angelikuwa mwislamu ingelikuwa kivumbi, ni kweli nyoka wa ugaidi kupitia imani ya waislamu ndie aliyewauma na kuwaachia kovu kubwa wamarekani! Sasa ulitaka wasemeje? Stereotyping kuwa kuna uhusiano wa Imani ya ugaidi na uislamu itachukua muda sana kufutika! Kama ambavyo kwa baadhi ya watu maradhi ya Ukimwi yanavyohusanishwa na umalaya, uasherati, uhuni nk.

Halafu magezeti mengi yanaandika habari inayouza gazeti......swala la mauaji ya mzungu huko Norway unadhani yatauza gazeti gani hapa marekani? Lakini iangalie jamii ya vijana wa Kimarekani na huyo marehemu mvuta unga wa kike! Hiyo ndio habari ati!

Anonymous said...

Mume wake ndiye aliyemwanzisha kweneye madawa ya kulevya. Wameaachana. Amy hajamwachia hata senti moja!

Anonymous said...

great point dada yangu, mimi ni mwanafunzi wa media hapa marekani na kwa kutafakari ni kwamba jambo hili si la kutukuza ma-star tu bali, media ya marekani inafanya makusudi kufunika kile wasichokitaka kiingie akilini mwa watu. ugaidi ni ugaidi tu, na hawa jamaa hawataki kuonesha watu wao kwamba hata mkristu mbaya zaidi mzungu kuwa anaweza kufanya jambo kama hilo...naamini angekuwa mwarabu ama mwislamu ungeona news zote za Amy na tukio hilo vikiwa sambamba kwenye media, sasa wanajua tukio la juzi lina prove wrong kwa kile wanacho feed watu wao kuwa ugaidi ni sehemu ya uislam.

Anonymous said...

Anonymous wa July 27, 2011 11:47 AM

Hivi ni Media ndio imefanya Uislamu uhusishwe na Ugaidi.....au ni hivyo vikundi vya kiislamu vilivyoupotosha Uislamu na kufanya uonekana una Itikadi za kigaidi.

Sielewi uko Marekani muda gani, jamii ya Kiimarekani KIHISTORIA haiufahamu SANA Uislamu, na bahati mbaya sana waliokuja kuwafungua macho Marekani Uislamu ni nini au ni watu wa namna gani wakawa ni hawa perveted Moslems! Na wala sio Media iliyosababisha picha hiyo mbaya!

Anonymous said...

suala si kwamba niko marekani kwa muda gani,ama wewe upo marekani kwa muda gani, literature inaweza kukupa mwangaza wa nini kilitokea hata kama hukuwepo katika jamii hiyo, that is not true and I don't know unaongea kwa what stand point of view kwamba wamarekani hawakuwa aware na uislamu, hapa duniani kuna dini nyingi sana lakini kwa karne na karne uislamu na ukristu zimekuwa ni dini mashuhuri sana, na licha kuwa mashuhuri zimekuwa zikilita mvutano wa karne na karne duniani kote including marekani, nadhani inabidi ufanye utafiti zaidi ya kujua hili, wewe umekuja marekani lini? 1776? come one! upende usipende that's how media work, zina set agenda kwenye kwa makusudi na ndo maana zinajulikana republicans ama democrats media hapa merekani,you should be aware of what to get from FOX about Obama ama MSNBC about Obama!

Anonymous said...

Anonymous July 28, 2011 5:34 PM....Hebu leta hizo literature zako za historia za Uislamu toka 1776!......na kwa nini vyombo vya habari viwe na agenda mbaya dhidi ya Uislamu? Una kitu gani cha ajabu na tishio na kipya?! Na hata kama vina agenda mbaya dhidi ya Uislamu,Je Ukristo? Je dini za Kiyahudi? Mbona kuna vyombo vya habari vingi viko biased na dini hizo? Utasemaje?

Anonymous said...

Unayehitaji kujua kuhusu Uislam na Amerika nenda kwenye hii website http://www.muslimsinamerica.org/

huko utakuta historia yote yaani pre Columbus, na pre slavery pia na baadae. Ngoja nikuanzishie, kisha endelea mwenyewe ingia HISTORY kwenye hiyo website

The Early History

Pre Columbus & Pre Slavery Years

Compiled By Amir Muhammad

In Dr. Barry Fell’s book Saga America, he reports that the southwest Pima people possessed a vocabulary which contained words of Arabic origin. Dr. Fell also reports that in Inyo County, California, there exits an early rock carving which stated in Arabic:"Yasus ben Maria" ("Jesus, Son of Mary"). Dr. Fell discovered the existence of Muslim schools in Nevada, Colorado, New Mexico, and Indiana dating back to 700-800 CE.

By 1312, Mansa Musa’s brother Sultan Abu Bakri II of Mali made his second expedition on the Atlantic ocean. In 1324 on his famous journey to Hajj, Mansa Musa reported in Cairo that his brother had left him in charge of Mali. Anthropologists have proven that the Mandinkas under Abu Bakri explored many parts of North America via the Mississippi and other river systems. At Four Corners, Arizona writings show that they even brought elephants from Africa to the area.

In 1492, Columbus had two captains of Muslim origin during his first voyage, one named Martin Alonso Pinzon the captain of the Pinta, and his brother Vicente Yanex Pinzon the captain of the Nina. They were wealthy expert ship outfitters who helped organize Columbus’ expedition and repaired the flagship Santa Maria. The Pinzon family was related to Abuzayan Muhammad III, the Moroccan Sultan of the Marinid Dynasty (1196-1465).

October 21, 1492, Columbus admitted in his papers that while his ship was sailing near Gibara on the northeast coast of Cuba, he saw a Mosque on the top of a beautiful mountain. Ruins of Mosques and minarets with inscriptions of Qur’anic verses have been discovered in Cuba, Mexico, Texas, and Nevada.

In 1527, the Spanish explorer Panfilo de Narva’ez left Spain for the Americas. In his fleet he had five ships and six hundred people in his company. The expedition met with many hardships. Several ships were destroyed by a West Indies, hurricane and a group of Indians killed a large number of the remaining members of the party. Afterward, when only a few members of the expedition were left, Cabeza de Vaca, the former treasurer of Narva’ez took up the leadership of the remaining members of the party with Estevanico being among them.

Estevanico was called an Arab Negro, a Muslim who came from Azamore on the Atlantic Coast of Morocco. He was among the first two persons to reach the west coast of Mexico in an exploring overland expedition from Florida to the Pacific Coast. It’s reported that Estevanico acted as a guide and it took them nine years to reach Mexico City where they told stories of their travels.

Anonymous said...

shukrani sana anonymous uliyeshusha nondo za uislam na america, naamini ndugu yangu sasa ameelimika.

Anonymous said...

shukrani sana anonymous uliyeshusha nondo za uislam na america, naamini ndugu yangu sasa ameelimika.vilevile tambua kukaa sana sehemu si kujua yale ya sehemu hiyo, unaweza ukajiona unajua kumbe unajua mitaa tu na story za kwenye baadhi ya vijiwe vya kahawa ambavyo hawati "facts."

Anonymous said...

......MBONA SIJAONA JIPYA...?ILA INAKUFANYA UJIULIZE NINI LICHOTOKEA BASI KAMA NONDO HIZO NI KWELI KIKAUFANYA UISLAMU USHINDWE HATA KUFIKISHA ROBO TU YA RAIA NCHII.....! JE KUNA KIPINDI WAUMINI WALIUKIMBIA!.......NI SAWA SAWA NA KUMFANYA MTU ASHUSHE NONDO ZA UKRISTO KUWA ULIKUWEPO KABLA YA MTUME SAUDIA!