Monday, October 10, 2011

Hali ya Dr. Harrison Mwakyembe ni Mbaya! Amepelekwa India kwa Matibabu

Kutoka IPPMEDIA.Com

Dr Mwakyembe leaves for medical checkup in India

By Correspondent


10th October 2011

Works deputy minister Dr Harrison Mwakyembe has been rushed to India for treatment of a skin related disease.

Dr Mwakyembe, who is also Member of Parliament for Kyela, left the country yesterday morning accompanied by his wife, Linah.

To see him off at the airport was Works minister Dr John Magufuli and other people, including the IPP Executive Chairman, Reginald Mengi.

The family spokesperson, Victor Mwambalaswa, said Dr Mwakyembe is suffering from a skin disease.

Speaking on the phone from his home to our sister paper Nipashe before he left, Dr Mwakyembe said that he was going to India for further medical checkup but did not disclose what he was suffering from.

He dismissed reports that he was seriously ill, stressing that he was not in bad condition.

For his part, Dr Mwakyembe’s personal assistant, Salum Nkambi said he has been receiving many calls from well-wishers seeking to know the condition of their lawmaker.

Nkambi said the health status of Dr Mwakyembe was not bad as reported in the media (not The Guardian).

Chama Cha Mapinduzi publicity secretary Nape Nnauye, who had driven the deputy minister to the airport, said Mwakyembe was flying to Mumbai, India where he will undergo medical checkup.

He said Dr Mwakyembe was not accompanied by a doctor because his condition was not bad.

President Jakaya Kikwete on Saturday saw Dr Mwakyembe at his residence at Kunduchi Beach in Dar es Salaam.

Water minister Prof Mark Mwandosya, who left the country in June for medical treatment in India was admitted at Applo Hospital where he is still undergoing treatment.

Prof Mwandosya started feeling unwell when he was attending the budget parliamentary session in Dodoma in June this year.
He was first rushed to Muhimbili National Hospital (MNH) before being referred to India for specialised treatment.

On Saturday he spoke by phone to Radio One saying that his condition was improving.

********************


Dr. Harrison Mwakyembe
Dk Mwakyembe Mgonjwa

Saturday, 08 October 2011

Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe

AVIMBA MWILI MZIMA, JK AMTEMBELEA

Na Mwandishi wetu

AFYA ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, ni tete baada ya kuugua ugonjwa uliomsababisha kuvimba mwili wote.Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na yeye mwenyewe zinaeleza kuwa, alianza kuwashwa ngozi miezi mitatu iliyopita kabla ya hali kubadilika siku za karibuni na hatimaye kuvimba sehemu kubwa ya mwili wake.

Mwakyembe alilieleza gazeti hili jana kuwa, baada ya hali yake kubadilika alianza kupata matibabu katika hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam akiwa nyumbani kwake Kunduchi Beach.Akizungumza na gazeti hili kwa shida, Dk Mwakyembe alisema hajui chanzo cha ugonjwa huo wa ngozi, daktari wake ndiye anaweza kuelezea kwa usahihi.

“Ni kweli naumwa nipo nyumbani, hata sura yangu imebadilika. Sasa hivi namsubiri daktari wangu, nilisikia natakiwa kupelekwa India kwa matibabu, nasubiri kauli yake si mimi niamue,” alisema na kuongeza;

“Siwezi kusema nimelishwa sumu, ninachosema mimi nimevimba kweli mwili mzima naumwa kweli hapa nimelala na sijui umenipataje kwa simu kwa sababu huwa siiwashi muda huu una bahati kweli”.

Mke wa Dk Mwakyembe Mkewe Linah Mwakyembe alipozungumza kwa njia ya simu na Mwananchi Jumapili, alisema kwa mujibu wa daktari wake, Dk mumewe anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi unaojulikana kitaalamu kama Exfoliative Dermatitis.

“Alianza kuugua muda mrefu kidogo, kama miezi mitatu iliyopita, hali hiyo ilikuwa inatokea na kupotea hadi sasa ambapo hali imekuwa mbaya zaidi,” alisema.

Alisema madaktari waliomfanyia uchunguzi kwa nyakati tofauti katika kipindi hicho walitoa majibu tofauti na kuongeza kuwa wapo waliosema hali hiyo ilisababishwa na kisukari na mwingine ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kulikuwa na chembechembe za sumu katika damu yake.

“Baada ya ngozi yake kubadilika sana na hali kuwa mbaya, tulienda hospitali na madaktari walitupa majibu tofauti, wapo waliosema ni kisukari na kuna mwingine alisema kuna chembechembe za sumu,” alisema Linah na kufafanua kuwa daktari aliyedai hivyo hakuwapa maelezo zaidi.

Kwa mujibu wa Linah, ngozi ya Dk Mwakyembe inawasha na inakuwa kama inatoa mba mwili mzima hadi kichwani.

Aliongeza kuwa daktari wake ameshauri ufanyike uchunguzi wa kina zaidi ili kujua kama atahitajika kupatiwa matibabu nje ya nchi.

“Walipendekeza afanyiwe uchunguzi zaidi, hivyo kama kutakuwa na ulazima wa kupatiwa matibabu zaidi nje ya nchi basi watatueleza,” alisema Linah.

Alisema kuwa leo ndio watapata jibu kama atahitajika kwenda nje au kuendelea na matibabu hapa nchini.

Alisema kumekuwa na uvumi mwingi juu ya ugonjwa wa Dk Mwakyembe na kusisitiza kuwa wao kama familia wanasikiliza kinachosemwa na madaktari na kile watakachoshauri.

“Sisi tunaendelea kusubiri kile kitakachogundulika baada ya uchunguzi huo na kama kutakuwa na mengine tutajulishwa na kujua hatua itakayofuata,” alisema Linah.

Exfoliative Dermatitis Kwa mujibu wa maelezo ya kitabibu, ugonjwa huu huweza kusababisha madhara makubwa ya mwili na matatizo mengine hivyo kuhitaji uangalizi wa karibu wa kitabibu.

Ugonjwa huu ukikomaa husababisha ngozi ‘kuwaka moto’ na huathiri wanawake na wanaume lakini zaidi wanaume wenye umri kuanzia miaka 55.

Dalili Dalili za ugonjwa huu ni kuwashwa, mwili kuishiwa nguvu pia sehemu ya juu ya ngozi hupukutika.

Chanzo kwa mujibu wa maelezo ya kitabibu, sababu za ugonjwa huo bado hajizulikani, hata hivyo matukio ya ugonjwa huu mara nyingi yanahusishwa na magonjwa mbalimbali ya ngozi, madhara ya dawa kama penicillin, sulfonamides, isoniazid na phenytion.

Rais Kikwete amtembelea Baadaye mchana Rais Jakaya Kikwete alifika nyumbani kwa Dk Mwakyembe Kunduchi Beach kumjulia hali.

Mwakyembe ambaye ni Mbunge wa Kyela mwaka 2008, aliongoza Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza kashfa ya Mkataba wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond.

Katika baraza jipya la mawaziri ambalo Rais Kikwete aliliunda mwaka jana, alimteua Dk Mwakyembe kuwa Naibu waziri wa Ujenzi akimsaidia Dk John Magufuli.

Mikasa ya Mwakyembe

Mei 21 mwaka 2009 Dk Mwakyembe alinusurika kufa katika ajali mbaya ya gari eneo la Ihemi kilomita 40 kutoka Iringa mjini akiwa safari kutokea Mbeya kwenda Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za Polisi, gari alilokuwa akisafiria Toyota Landcruiser T362ACH, liliacha njia saa moja asubuhi baada ya kukanyaga shimo na tairi ya upande wa kulia kuchomoka na dereva wake, Joseph Msuya (30), kupoteza mwelekeo kabla ya gari hilo kutoka nje ya barabara upande wa kushoto na kuparamia mti kisha kupinduka.

Ajali hiyo ilitokea wakati dereva wa Dk Mwakyembe akijaribu kulipita lori kabla ya kukanyaga shimo hilo.

Dk Mwakyembe na abiria wengine waliokolewa na Wasamaria wema pamoja na trafiki wawili waliokuwa kwenye basi dogo wakisafiri kutoka Iringa kwenda Njombe.

Baada ya ajali hiyo alilazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa. Ilifahamika kuwa aliumia taya kisha alihamishiwa Dar es Salaam kwa matibabu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) aliunda tume iliyoongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakati huo, Kamanda James Kombe, kuchunguza chanzo cha ajali hiyo. Matokeo yalionesha kwamba ilisababishwa na uzembe wa dereva wake, Msuya.

5 comments:

Dr. Ustaadh said...

Exfoliative Dermatitis ni ugonjwa ambao unatokana na sababu kubwa tatu:

1. Mwili kuwa 'allergic' na dawa fulani na hivyo dawa hiyo kugeuka kuwa kama sumu katika mwili.

2. Sawa na sababu ya kwanza, inaweza mtu akawa amekunywa sumu ambayo inafanya mwili kuwa na 'reactions' za namna hiyo.

3. HIV.

Wanaopata ugonjwa huo ambao ni hatari sana, ni 19% ndiyo hufanikiwa kupona. Ni vyema watanzania tukawa watulivu kipindi hiki cha mpito na kizito cha mpendwa wetu Dr. Harrison Mwakyembe. Tungependelea wale mafisadi ndiyo wawe Mwenyezi Mungu anawaadhibu namna hii, lakini tunapoona wanapeta tu basi uchungu unakuwa mwingi. Ee Mola, iangalie nchi hii ya Tanzania na uwaghafilishe wale wote wanaofanya watu tuzidi kuwa masikini na nchi kulundikiwa madeni kwa ufisadi wao.

Anonymous said...

Mm huwa inafikia mahali natamani kumkufuru Mungu kwa kumuuliza kwa nini aliniumba kuwa Mtanzania? Nchi zote za kiafrika ambazo wananchi wake ni aggressive wamevikataa vyama vyote vilivyopigania uhuru kwa sababu baada ya nchi hizo kupata uhuru vyama hivyo viligeuka kuwa wakoloni hali hii ndiyo iliyopo tanzania hivi sasa ambapo CCM imepoteza malengo yake ya awali na kimegeuka kuwa chama cha kikoloni ambacho kinatumika kwa maslahi ya wakoloni wachache na wanajulikana kuwa ni huyo burushi wa kiirani na jamii yote ya wahindi waliuziwa mashirika yetu km Manji, Jeetu nk, vibaraka wa kitanzania kama Mkapa,Mkono, white hair n.k. hawa wote wanalindwa na jk this is clearly known na mpango wao ni kumweka madarakani mtu atakayelinda maslahi yao 2015. Jk kwenda kumjulia hali Mwakyembe ni unafiki ulikithiri kwa sababu he knows what they have done kwa Mwakyembe na yeye akiwa ni mwenyekiti wa CCM haya yamefanyika kwa baraka zote za CCM ili kulinda maslahi ya hao wakoloni. Hivi watanzania kweli mmekubali kurudi kuishi ktk maisha ya kikoloni angalieni wenzenu kenya, zambia, ghana, libya, tunisia, misri nchi hizi zimewakataa wakoloni wanaojifanya walipigania uhuru ifikie mahali watanzania tuwe agressive tukatae hii hali inabidi tuanze kuingia mitaani kuyakataa haya mambo ya ki[NENO BAYA] kwa mfano hivi sasa dowans inataka kulipwa 111Bilion hivi tunakubaliana na mambo kama hayo. nayahamasisha makundi na mashirika ya kijamii na tasisi za wasomi na hasa wanafunzi wa vyuo vikuuu tuonyeshe mfano tuanze na hili la dowans. Tusiwe kama wananchi wa igunga walioamua kukirudisha chama cha wakoloni kiendelee kuwatawala sijui wana raha gani na hali ya sasa ya mgawo wa umeme, inflation 12%, tena wilaya hiyo wananchi wake wanakabiliwa na njaa, wanafunzi wanakaa chini kwa kukosa madawati barabara ndio usiseme! Its time to say ukoloni wa ccm sasa basi! EE mwenyezi Mungu uwe upande wetu tunapoanza kuuwasha moto wa kuuondoa ukoloni wa CCM nchini mwetu!

Anonymous said...

Tumwombee apone! Hizo sumu ambazo wanapewa wanasiasa ovyo!

Anonymous said...

Tumwombee apone! Hizo sumu ambazo wanapewa wanasiasa ovyo!

Anonymous said...

TATIZO TUNAWANAUME MAYAI SANA, KUMRADHI NDIO KAKA ZETU, BABA ZETU, WAJOMBA...N.K LAKINI SIJUI NI KITU GANI KWAKWELI, US*NGE SANA, WANAUME WETU WANAUZA SURA, ONLY MAKOMANDO KINA DR MWAKYEMBE NA KINA SLAA NA WAKE ZAO HAWAJALI SURA ZITACHAFUKAJE KWA KUPIGANIA UFISADI UNAONUKA TANZANIA, TUNAFUKIZIWA UBANI HUKO BAGAMOYO KILA KUKICHA TUSIAMKE....TUAMKE JAMANI, KINA MAMA.. TUSISUBIRI TENA WANAUME WETU WAKATUPIGANIE, WASHAVUNJWA MFUPA HAWA,SISI KINA MAMA NDIO TUNALEA WANETU SASA, TUTAFUTE KILA NJIA YA KUWAFUKUA WATU HAWA WABAYA SO CALLED VIONGOZI..