Saturday, September 08, 2012

Wazazi Wangu Washerekea Miaka Hamsini ya Ndoa

Wadau, napenda kuwafahamisha kuwa wazazi wangu, Dr. Aleck na Mrs. Rita Che-Mponda wamesherekea miaka hamsini ya ndoa wiki iliyopita mjini Dar es Salaam. Ndoa yao ilibarikiwa katka kanisa la Anglikana St. Albans, Dar es Salaam. Walifunga ndoa mwaka 1961, baba akiwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Howard. Mama alikuwa amemaliza masomo yake ya unesi.

Mungu azidi kuwabariki.

Dr. & Mrs. Aleck Che-Mponda 
Misa ya Kuwabarika St. Albsans
Wazee wakiwa na baadhi ya ndugu


1 comment: