Saturday, August 10, 2013

Muda Mfupi Kabla ya Sheikh Ponda Kupigwa Risasi


 Kutoka Jukwaa Huru.com

Huku taarifa ambazo zinaendelea kusambaa zikiwa zinadai kuwa Sheikh Ponda amepigwa risasi na Polisi, na huku Jeshi la Polisi likikanusha kuhusika na tukio hili, likieleza kuwa halikuhusika na wala halijui aliko mwanaharakati huyo wa Uislamu, hapa ni picha za kinachoelezwa kuwa kilitokea kabla ya tukio la Ponda kupigwa risasi (kama ni kweli amepigwa risasi) 

Picha hizi ni kutoka blog ya Google Habari, na zimeambatana na maelezo yaliyo chini yake: 




Leo kwenye kongamano la kuita umoja wa waislam katika yanayo wakabili waislam mkoani Morogoro.
Kongamano lillienda vizuri likiwa limepambwa na mashekh wakubwa wakubwa kama vile Riko, Mwaipopo, Kondo pamoja na shekh Ponda.
Shekh ponda alikuwa wa mwisho kutoa mawaidha na aliaga waislam ili aweze kuelekea Msikiti wa Mungu mmoja hivyo waislam walitaka kumsindikiza Shekh Ponda mpaka Mskiti wa mungu mmoja.
Maaskari waliovalia nguo za Field Force wakiwa kwenye defender waliingia na kuanza kuifuata gari kwa nyuma. 
Waislam waliendelea kuizunguka gari ya Shekh Ponda ila maaskari walianza kupiga mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi kisha kuifukuza gari ya sheikh Ponda.
Sikubahatika kushuhudia nini kiliendelea kutokana na mabomu ya machozi yaliyopigwa na maaskari hao lakini dakika chache baadae nilipata taarifa ya kwamba amepigwa risasi ya bega na amepelekwa hospitalini…..endelea kutembelea blog ili ujue nini kinaendelea kwa Shekh Issa Ponda amabae inasemekana yupo Hospitali tayari kupata tiba.

11 comments:

Anonymous said...

Hali hii ni tete, ila pia kuna matumizi mabaya ya mitandao kutoa taarifa nzito bila uthibitisho, ni ngumu sana kuongelea kufa kwa bwana Ponda. Ila cha msingi tulaani matumizi ya nguvu na kwa sasa Ponda hajulikani alipo,.Kutatokea machafuko halafu Ponda ataibuka baada ya siku mbili tatu cjui watu mashuhuri ambao wametumia kurasa zao za Facebook na Twitter kuoneza ''Kifo'' bila kuona mwili watajificha wapi..

Anonymous said...

hahahahaha watz wamechoka amani waache wawe buisy kukitafuta kiberiti cha kulipua machafuko watajuta Rwanda wanaachekaaa Malawi meno yote 32

Anonymous said...

Who is controlling the police.... [Government] ...who is goverment [CCM]...who is CCM .....shame! shame! shame!

Mdau V said...

Tunalaani vikali tendo la kumshambulia kwa risasi Sheikh Ponda au raia yeyote hata kama ni mtuhumiwa! Sheria ipo wazi! Mtuhumiwa akikamtwa. Haki za binadamu zizingatiwe! Akifikishwa mahakamani, akakutwa na hatia na hata akifungwa bado analindwa na sheria, katiba na haki za binadamu. Pale makao makuu ya polisi na katika kuta za baadhi ya vituo vya polisi na magereza kuna posters zinazoelezea haki za mtu anapokamatwa na kuwekwa mahabusu! Sasa hayo ni mapambo au ndiyo yale matamshi bila vitendo? Is Tanzania going to the dogs or are we already in the gutters? Mungu iokoe nchi yangu!

Anonymous said...

Hali hii inatisha! Tuakwenda wapi? Hivi tutafika salama 2014 na 2015?

Leczenie kanałowe Poznań said...

Z niecierpliwością oczekuję kolejnego wpisu:)

Anonymous said...

TANZANIA INAENDA WAPI????
WATAFUTE FILM ZA NCHI ZENYE VITA NDO WATAJUA NINI MAANA YA KUMWAGA PETROL NANI NA KUWASHA KIBERITI

KILA KONA MAJANGA TUU YANACHOSHA
TINDIKALI
RISASI
MAUAJI
VISASI
ASKARI WANAJIAMULIA TUU
SERIKALI IKO WAPI

SIE TUNAISH EOROPE TUNAANGALIA TLC TV PROGRAM ULIONA WAMAREKANI WANAVYOMILIKI SILAHA NA MADHARA YAKE HUTOTAMANI

WACHA TUENDELEE KUBEBA MABOX KAMA WASEMAVYO WABONGO

ILA AMANI FULL
HATUJIULIZI TUTAKULA NINI??
TUNAJIULIZA NIPIKE CHAKULA GANI
SIPANGI FOLEN HOSPITALI NAENDA KWA APOINTMENT.
NALIPWA NA NILIKIZAA KINALIPWA TOKA MWEZI WA KWANZA

WAKUBWA WASISHIKE USUKANI WAKATI HAWAJUI KUENDESHA BWANA TUMECHOSWA NA WAPOTEZA AMANI

Anonymous said...

Tafadhali polepole.nimekaa na shehe ponda segerea.Ni mtu makini sana na inspirational.anazo hoja nzito kwelikweli ukimsikiliza.baada ya kukaa karibu naye na kumsikiliza,kumhoji na kujadili naye,yapo mambo mengi sana ya msingi sana kwenye madai yake ambayo sentensi kama hii ya kwako haimtendei haki.haina maana hata kidogo kudhani na kupuuza madai yote anayoyatoa.hii haina maana pia kuwa yote anayoyadai apewe.mimi naona tumwombee heri apone na tuepushwe na majanga.usipende kufurahia anguko la binadamu mwenzako.

Anonymous said...

Gharama ya uchochezi, kuchoma makanisa, kumwagia watu tindikali ni
sawa na kisima cha maji yasiyo salama!

Anonymous said...


Sheikh Issa Ponda is understood to have survived the raid and was on the run but injured, police sources told The Daily Telegraph.

He had visited Zanzibar in the weeks running up to the attack on Katie Gee and Kirstie Trup, both from north London, who were on Saturday still in hospital being treated for their injuries.

Ponda earlier this month met with the imprisoned leaders of a Muslim separatist group, Uamsho, who police believe may have inspired the attack on the two women.

Tanzania’s director of public prosecutions, Elieza Feleshi, on Friday ordered that the cleric be arrested after accusing him of inciting violence, for which he was convicted earlier this year and given a 12 month suspended sentence.

“He narrowly escaped from the police in Morogoro, he was shot by our officers, but we are pursuing him,” said Faustine Shilogile, a senior police commander in Morogoro, the town 110 miles west of Tanzania’s commercial capital, Dar es Salaam, where Ponda was shot.

The Telegraph: Radical preacher wanted over Zanzibar acid attack shot in police raid - Telegraph

Anonymous said...


Nilipomuuliza Sheikh Ponda swali kuhusu kwa nini anasema kuna mfumo kristo,alianza kwa kusema akiniambia nimwambie ni kwa nini waislamu wengi hawajakwenda shule,nitamjibu haraka kuwa wao wamebase kwenye madrasa badala ya academia ya kawaida.tukacheka.baada ya kicheko,nikamwambia si viongozi wengi tu wakuu ni waislamu? akacheka sana.akaketi kunipa somo.refu sana na lililojaa weledi.mfano nakumbuka aliniambia kuwa wanaposema mfumo,wanakwenda mbali kuangalia ni namna gani historia ya taifa imeathiriwa na mfumo wa ukoloni wa kimagharibi,na ukoloni mambo leo.ukristo umesukwa katika ustaarabu wa mataifa haya.serikali yetu imechukua mifumo mingi ya kisheria,kielimu na kiutawala kutoka wakoloni hawa wa kimagharibi.na haya yote yana exclude wislamu,kwa kutaka au bila kutaka .hoja kuwa lakini waislamu hawakuzuiwa kwa vigezo vya dini aliijibu kuwa basi mimi sielewi maana ya mfumo.akanipa mfano wa mfumo dume.akasema kwani shule huwa zinawabagua wasichana? lakini ni kwa nini tunalalamikia mfumo dume? hebu angalia mfano mmoja tu huu.kwa hiyo hatimaye,upo mlingano usiyo sawa kati ya waislamu na wakristo katika mtazamo wa makundi,na jinsi yanavyokuwa na ushawishi katika serikali,na waislamu wanaona wameachwa nyuma.na kumbe mambo ya kisheria,ki utawala na mengine ni ya kimagharibi,kwa hiyo ya kikristo,na kwa hiyo kandamizi kwa waislamu
nimesema ninajaribu kukumbuka tu na wala sijaweka kabisa kama alivyokuwa anasema exactly.nipeni jibu la kuonyesha kuwa katika hili hakuna hoja ya msingi