Showing posts with label Theluji. Show all posts
Showing posts with label Theluji. Show all posts

Monday, February 11, 2013

Kimbunga Nemo Ilivyotukomesha!!

Wadau, Kimbunga Nemo imemwaga theluji (snow) kibao hapa Boston! Yaani karibu futi tatu!  Sasa kazi kuindoa maana haiyeyuki haraka, na kwa vile ilidondoka haraka kwa kipindi kifupi, ma-plow walishindwa kuondoa theluji kwenye barabara nyingi hapa mjini.

Wazungu hawajazoea kuambiwa wasiendeshe magari yao. Basi siku ya Ijumaa wakawa wanamwita Gavana wetu, Deval Patrick ambaye ni mweusi, Dikteta, MKomunisti nk..  Lakini sasa wanamshukuru na kukubali kuwa alifanya jambo la maana, maana barabara kuu ziliweza kusafishwa haraka.  Hata Connecticut na Rhode Island walifuata nyayo za Gava wetu na kuzuia watu wasiendeshe magari yao! Huko Long Island New York, watu walikoma maana mamia ya magari ya kwama na watu ndani.


Mtaani kwangu Cambridge, MA jumamosi mchana! Plow haikupita hadi jioni. Ilikuwa kazi kweli kufika nyumbani maana hiyo snow iliuwa zaidi ya futi mbili!!!  Nilitoka kazini nimechoka.  Ingawa Gavana alizuia watu kuendesha magari nilibahatika kupata lifi hadi karibu na napokaa.  Kufika mtaani ndo jinsi nilivyokaribshwa! DUUUUHHHH!

Wadau, mgongo unaniuma! Jana ilinichukua masaa kufukua mkweche wangu!!!!

Hii ndo Executive Order ya Gavaana wa Jimbo la Massachusetts kuamurisha watu wasiendeshe magari baada ya saa 10 jioni siku ya Ijumaa Februari 8, 2013.  Ilikuwa ukikamatwa unaweza kufungwa jela mwaka moja na kupigwa faini ya $500!   Gavana kaitwa Fashisti, na kutanawa matui ya nguoni.  Watu walirushusiwa kuendehsa magari saa 10 jino siku ya jumamosi. Hata hivyo, utaenda wapi bila ku-risk gari kukwama kwenye snow!

Tuesday, February 01, 2011

Mwokozi Wetu Tunaopambana na Snow?


(pichani Mnyama aina ya Groundhog)


Kesho macho ya wanaoishi maeneo ya baridi Marekani yako kwa huyo mnyama
aina ya groundhog. Hasa groundhog ambaye anaitwa Punxatawney Phil na anakaa Pennsylvania.
Watu wanaamini kuwa Phil asipoona kivuli chake basi tutaendelea kupigwa na snow na barafu. Kama akiiona basi ina maana haya mateso yataisha. Kwa vile mwaka huu tumekuwa na winter mbaya sana watu hawatalala leo usiku wakingojea kusikia Phil atasemaje!
Phil, Please don't see your shadow!
Kwa habari zaidi za Groundhog Day na Phil someni:

Snow Imezidi Boston! Tumechoka!



Yaani leo ni siku ya kwanza ya Februari. Tunapigwa na snow tena. Kesho tutapigwa tena. Ikiisha tutakuwa na karibu futi mbili na nusu ya snow! Hiyo ni juu ya ile snow ambayo ilianguka majuzi! Hatuna pakuiweka. Ni hatari kutembea na kuendesha magari shauri ya milima ya snow. Watu wameonywa kuwa ikianza kuyeyuka kutakuwa na mafuriko!

Thursday, January 27, 2011

Hii Winter ni Mbaya Mno!


Wadau, sijui huko ulipo lakini hapa Boston tunapigwa na theluji (snow) si kawaida. Sasa hatuna pa kuiweka. Wanasema kuwa snow ya mwaka huu itaingia katika vitabu vya historia. Sasa watu wanatania na kusema kuwa hali ikiendelea kama ilivyo sasa itakuwa kama wale wanaodesha magari yao pichani! Kama snow ingekuwa inayeyuka kabla ya nyingine kuanguka hali isingekuwa mbaya. Lakini sasa kuna milima ya snow kila mahala!
Kwa habari zaidi soma:

Thursday, January 13, 2011

Tunapambana na Theluji na Barafu!






Ni msimu wa winter (Baridi) hapa Marekani. Tunatamani joto la Dar. Hizi picha nilipiga hapa Cambidge, Massachusetts leo asubuhi.

Monday, December 22, 2008

Ilitokea kweli - No. 1

Hapo zamani za kale, wabongo walichukuliwa kwa wingi na serikali ya USSR (Soviet Union) Urusi, kwenda kusoma huko.

Sasa si mnajua ubaridi wa kule. Yaani baridi hasa. Theluji na barafu kibao. Sasa kuna mBongo fulani, mwanaume alipenda sana kunywa vodka ya Urusi. Yaani baada ya kazi ngumu ya kubukua kazi kunywa vodka.

Siku moja baada ya kunywa alitoka na kawa anatembea barabarani. Theluji ilianguka kwa wingi mpaka jamaa akaona taabu kutembea. Aliamua kusimama na kupumzika kidogo mtaaani huko theluji inazidi kuanguka kwa wingi. Mwisho kalala hapo hapo alipokuwa.

Asubuhi yake, warusi walikuwa wanasafisha mitaa na kuzoa ile theluji iliyoanguka. Wakakuta maiti ya mwafrika mle kwenye snowbank (mlima wa theluji). Wakaita gari la kuja kuchukua maiti. Ile gari likaja na wakatia maiti ya mwafrika mle.

Kufika mortuary, wakailaza maiti mapokezi. Kumbe ile joto ndani ya gari la maiti na ndani ya jengo ilikuwa inafanya mambo. Jamaa ambaye alidhani maiti kakaa wima halafu kaongea Kiswahili! Wacha wazungu wakimbie!

Wataalam wanasema na sikumbuki vizuri lakini ilikuwa kama ile pombe ilipunguza metabolism sijui na ile theluji ilikuwa insulation ndo maana hakufa.

Nafurahi kusema jamaa alimaliza masomo yake Urusi na alirudi Bongo miaka ya 90.