Tuesday, February 01, 2011

Mwokozi Wetu Tunaopambana na Snow?


(pichani Mnyama aina ya Groundhog)


Kesho macho ya wanaoishi maeneo ya baridi Marekani yako kwa huyo mnyama
aina ya groundhog. Hasa groundhog ambaye anaitwa Punxatawney Phil na anakaa Pennsylvania.
Watu wanaamini kuwa Phil asipoona kivuli chake basi tutaendelea kupigwa na snow na barafu. Kama akiiona basi ina maana haya mateso yataisha. Kwa vile mwaka huu tumekuwa na winter mbaya sana watu hawatalala leo usiku wakingojea kusikia Phil atasemaje!
Phil, Please don't see your shadow!
Kwa habari zaidi za Groundhog Day na Phil someni:

2 comments:

Malkiory Matiya said...

Hii kali kweli!

emu-three said...

Poleni sana, mukion vipi ombeni likizo ya dharura mje bongo, maana hapa jua ni kali kweli...lol