Monday, June 11, 2007

Kwa Heri Sopranos!



Sijui kama mlikuwa mashabiki wa Sopranos. Jana ilikuwa mwisho wa hiyo show. Na watengenezaji waliacha watazamaji kwenye mataa iliishia vipi. Walitumia Njia ya 'Fade to Black' kumaliza show. Kwa hiyo sisi watazamaji tubakie kujadili Sopranos iliisha vipi.

Mimi nimekuwa mshabiki wa Sopranos kama mwaka moja hivi. Nilikuwa nasikia watu wakiongea kuhusu Sopranos lakini wala sikutazama miaka yote hii. Ila nilianza kutazama kwenye reruns. Comcast wana On Demand, na uliweza kuonza Seasons zote. Kwa muda mfupi nilijua habari za Big Pussy, Christopher, akina Aprile na wengine.

Basi nikaanza kuzitama na kugundua kumbe Sopranos ni nzuri. Huyo Tony Soprano, japo ni mobster ana maisha na familia, na marafiki na watu wanaomwabuud na wanaomwogopa, na pia alikuwa amejaa ashki ya uzeeni. Episodes nyingi walimownyesha Tony akifanya mapenzi na wanawake wasio mke wake. Wengine waliweza kuwa hata umri wa binti yake, wazungu wanaiita 'mid life crisis'.

Lakini ilikuwa kila ukimzoea character, huyo anauliwa! Kifo nilichofurahia ni cha mshenzi Ralph, aliyeua fariai wa Tony Soprano. Ralph alikuwa kichaa anaua watu kwa kufurahia kweli. Kifo nilichosikitika kuona ni cha Bobby Bacala, wiki iliyopita. Huyo baba, alikuwa mpole na alikuwa anajali watu, lakini Tony alimlazimisha kwenda Canada kuua mtu. Bobbby aliuliwa kwenye Toy store.

Yule Baba mdogo wa Tony, Uncle Jr. jana walimwonyesha hana akili kabisa, zimefyatuka shauri ya ugonjwa wa Alzheimers. Na Silivio aliyekuwa concilieri (mshauri) wa Tony alipigwa risasi wiki iliyopita na sasa yuko kwenye coma.

Mtoto wa Tony A.J. maskini ya mungu, show ingendelea nadhani anefanikiwa kujiua. Tokea yule binti mDominica amwache amekuwa kama mwehu hivi. Na hata siku moja atakuwa katili kama baba yake.

Binti yake Tony, Meadow, naona atafanikiwa kimaisha. Anasomea sheria. Na inaelekea ataolewa na rafiki aliyekuwa anatembea naye kisirisiri.
Dada yake Tony, Janice, kawa binadamu alikuwa anajadili ataishaje na watoto wa marehemu mume wake, Bobby Bacala. Hao watoto wa Bobby ni yatima, maana mama yao alikufa kwenye ajali ya gari, ndo Bobby kamwoa Janice.
Paulie, yule mzee rafiki yake Tony mwenye nywele kama vampire, haachi kuchekesha. Jana kasema eti paka ni nyoka mwenye manyoya (fur). Kisa Tony katokea kumpenda paka wa mitaani. Ajabu huyo paka alipena kukaa na kulia mbele ya picha ya Christopher, aliyeuliwa na Tony. Je, roho ya Christopher imo ndani ya huyo paka?
Kuna mengi ya kusema kuhusu Sopranos, nadhani kwa vile imekuwa na washabiki wengi huenda wakatengeneza sinema za Sopranos. Na wakitengeneza mtasikia kuna Sopranos Movies hata 20!

Asante HBO kwa hadithi tamu ya The Sopranos.

No comments: