Wednesday, June 27, 2007

Mipango ya Mazishi ya Marehemu Mheshimiwa Amina Chifupa

The late Amina Chifupa's ex-husband Mohamed Mpakanjia talks to ITV.



Jeneza lenye mwili wa Marehemu Amina Chifupa



From ippmedia.com

Bunge laahirishwa...mwili kuagwa leo

2007-06-27

Na Usu-Emma Sindila, Dodoma

Kifo cha Mbunge wa Viti Maalum-CCM, Mheshimiwa Amina Chifupa kimelifanya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuahirisha shughuli zake ili kujipa muda wa kumlilia mwenzao, Mheshimiwa Amina Chifupa aliyefariki usiku wa kuamkia leo.

Spika wa Bunge, Mhe. Samweli Sitta amesema shughuli za Bunge zitaendelea tena kesho asubuhi saa tatu. Hata hivyo amesema wabunge kadhaa wameteuliwa kuja Jijini Dar es Salaam kuungana na ndugu wa marehemu kuomboleza na kushiriki shughuli nyingine za msiba huo mzito.

Awali ilikuwa imetangazwa kwamba mwili wa marehemu ungepelekwa Dodoma kuagwa na kisha kusafirishwa kwenda Njombe kwa maziko.

Spika amewataja watakaoongoza msafara huo wa wabunge kwa ajili ya kuuaga mwili na kisha kesho kushiriki maziko kule kijijini Lupembe wilayani Njombe kuwa ni pamoja na yeye mwenyewe, kiongozi wa upinzani bungeni, Mhe. Hamad Rashid Mohamed, wabunge wote wa Dar es Salaam, wabunge wote wa Iringa na Mbunge Anne Kilango aliyekuwa mlezi wa marehemu.

Amesema watakaowakilisha Serikali katika msiba huo ni Waziri wa Usalama wa Raia, Bw. Bakari Mwapachu. Amesema marehemu atazikwa kesho katika kijiji cha Lupembe wilayani Njombe kule Iringa, alasiri. Kwa mujibu wa Spika Sitta taarifa marehemu alifariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Jijini Dar.

12 comments:

Anonymous said...

Habari za kawaida
Posted Date::6/27/2007
Maelfu wajitokeza kumwaga Amin Chifupa Dar
Na Jonas Songora

MAELFU ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiongozwa na viongozi wa juu wa serikali jana waliuaga mwili wa Mbunge wa Viti Maalum wa CCM, marehemu Amina Chifupa nyumbani kwao Mikocheni.


Shughuli ya kuanga mwili wa marehemu iliyoongozwa na Rais Jakaya Kikwete, ilianza saa 7.00 mchana na kukamilika baadaye jioni, ilighubikwa na huzuni kubwa.


Watu wengi walishindwa kujizuia na kuangua kilio wakati wa kuaga huku wengine wakisema Tanzania imepoteza kijana shupavu ambaye hakuogopa kusema kile ambacho hakina maslahi kwa nchi.


Familia yake imesema marehemu alikuwa na magonjwa mengi ya ajabu yaliyoshindikana kupata tiba ya kitalaam.


Baba wa marehemu, mzee Hamis Chifupa, alisema magonjwa hayo yalimuanza tangu Mei 8 mwaka huu.


Kuhusu taarifa kuwa mwanawe alikufa kwa kisukari Mzee Chifupa alisema marehemu hakuwa na rekodi ya kuumwa ugonjwa huo.


Mume wa marehemu Mohammed Mpakanjia alisema alifanya mambo yote kama muislam na amesikitishwa huku akiwa haamini kama kweli Amina amekufa. Alisema kutengana kwao si chanzo cha kifo bali matakwa ya Mungu.


Watu wengi walijitokeza nyumbani kwa marehemu, akiwamo mwanasiasa mkongwe Mzee Rashid Kawawa, Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, Meya wa jiji la Dar es Salaam, Ayub Kimbisa, na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa.


Akitoa nasaha zake, Maalim Seif aliwataka vijana zaidi wajitokeze kupinga vita dhidi ya dawa za kulevya kama ilivyokuwa enzi za marehemu aliyekuwa mstari wa mbele kupiga vita biashara ya dawa za kulevya.


Alisema CUF walikuwa wakiunga juhudi zake siku zote na kwao wamempoteza mtu muhimu. Londa aliwataka vijana kuiga mfano wa marehemu na kufanya kazi kwa bidii katika nyanja tofauti ili wapate mafanikio.

unaweza kuyapata haya kutoka linkhttp://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=191

Anonymous said...

Da Chemi,kwani Amina alikuwa na watoto wawili?au hapo ni mmoja ndo wake?

Anonymous said...

Mumtaz,
Nijuavyo mimi alikuwa na mtoto mmoja ambaye aliwahi kumpeleka na kumtambulisha bungeni Dom kwenye mojawapo ya vikao vya mwanzo wa Bunge hili la sasa. Huyo mtoto mwingine si wake labda wa mumewe. Any way cha muhimu ni wamebaki na baba ila mmoja kampoteza mama mzazi. Upo hapo mumtaz?

Anonymous said...

Mapakanjia analia nini??
si alishataliki au ndo alikua anatingisha kibiriti tu

Anonymous said...

Hivi huyo katili Mpakanjia haoni hata haya. Analia machozi feki kabisa. Si alimtaliki? Je, Amina alionekana hadharani baada ya kashfa za huyo Mpakanjia?

Anonymous said...

Nawaonea huruma hawa watoto kuachwa bila mama. Ila watampata mama wa kambo sasa hivi.

Anonymous said...

Asante kaka mnyamapori kwa kunijibu.

Anonymous said...

wewe michuzi jr wacha ujinga wewe hivi na wewe unaamini kwamba mungu akimpenda mtu zaidi yetu ndio anamuua?
ndio kusema kwamba mungu kamchukua kutoka kwnye sura ya ulimwengu huu kwa kumuua namna hiyo na kuwatesa ndugu zake kwa uchungu wa kuondokewa na wampendaye?
wacha hizo wewe tafakali kabla ya kuandika

Anonymous said...

Mpakanjia na Shigongo wasihuzunike kwa lolote, hatutaki unafiki.

Anonymous said...

Huyo Shigongo anapenda sana majungu. Haoni hata haya. Anasema uwongo na kuongeza chumvi ili auze gaeti. Haya tuone atamwonea nani sasa.

Anonymous said...

Dada Chemi,kifo cha Amina kinatufundisha kuwa duniani tu wapitaji yatupasa kuishi kwa matendo mema ili tutakapoondoka matendo yetu yaendelee kuishi.Nadhani wa kwanza wanaotakiwa kulipokea somo hili ni viongozi wetu ambao mambo mengi wanayofanya ni ya kuchefua.

Anonymous said...

Najua mpakanjia anatuhumiwa kuhusika na kifo cha amina labda hakujua kwamba Amina alikua na mapenzi ya dhati tofauti na yeye na kwamba alipata mwanamke ambae ni kama kapata dhahabu ndani ya mikocheni, wanaume wengi tu walikua wanasubiri atamwacha lini wamuoe wanaume wa maana wanaojua nini kupendwa na kupenda wanaowaheshimu wake zao, waliofundwa wanaojua nini cha kuongea na waandishi wa habari wanaojua kuficha siri za wake zao ambao wameumbwa kama kichwa cha familia.Wanaojua thamani ya mwanamke ambao wangemshukuru Mungu kila kukicha kupata hazina kama Amina. Lakini kwa kuwa wewe u kinyume na yote niliyoyaodhoresha hapo juu hukumstahili Amina hata kidogo. Ulimtumia kupata umaarufu tuuu!!

Kuna mengi ya kuandika ila kwa kua kuna mtoto na amekosa Mama anamstahili baba yake sana kwa sasa hivi.

JIREKEBISHE