Wednesday, June 27, 2007

Mheshimwa Amina Chifupa atazikwa Njombe


Ama kweli kifo cha Mheshimiwa Amina Chifupa kimegusa wengi. Jana nimeshinda kwenye simu na neti kwenye e-mails naongea na watu kuhusu kifo chake. Kifo chake kimegusa wengi.

*********************************************************************

From ippmedia.com:

Wabunge kibao waangua vilio

2007-06-27

Na Emmanuel Lengwa, Mikocheni


Kama kuna siku ambayo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limegubikwa na simanzi, basi ni leo asubuhi wakati Spika, Samweli Sitta alipowatangazia wabunge kwamba mwenzao, mheshimiwa Amina Chifupa, amefariki dunia.

Baada ya taarifa hiyo, wabunge wengi walishindwa kujizuia na kuanza kuangua kilio waziwazi. Mbunge Jenista Mhagama, Aziza Sleyum, Martha Mlaka na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Margareth Sitta ni miongoni mwa wengi waliokuwa wakibubujikwa machozi waziwazi na kuwalazimu wabunge wengine kujipa ushujaa wa kuwafariji muda wote. Vilio hivyo na simanzi vilishika kasi zaidi wakati wabunge wote walipotulia vitini ili kumsikiliza Spika wa Bunge, Mhe. Sitta wakati akiendelea kueleza utaratibu unaofuata.

Kadhalika hapa Jijini Dar, nyumbani kwao marehemu Amina, vilio vilitawala huku ndugu na jamaa wakiwa hawaamini kama kweli mpendwa wao amewatoka. Alasiri ilipotinga nyumbani kwa baba wa marehemu, Brigedia mstaafu Chifupa, Mikocheni Jijini leo asubuhi imemkuta aliyekuwa mume wa marehemu pamoja na na familia yake, wakiwa katika majonzi makubwa.

Akizungumza na Alasiri, Bw. Mohamed Mpakanjia, amesema mazishi ya aliyekuwa mkewe yanatarajiwa kufanyika kesho huko wilayani Njombe. ``Tutaondoka kesho kwenda Njombe kwa mazishi? leo tunatoa fursa kwa ndugu, jamaa na marafiki na wananchi wa waliopo Jijini Dar ili kuweza kumuaga kabla ya kumsafirisha,`` akasema Bw. Mpakanjia.

Bw. Mpakanjia amesema ikiwa ratiba itakwenda kama ilivyopangwa, baada ya wabunge kutoa heshima za mwisho, mwili wa marehemu utaondoka kwa ndege kuelekea Njombe ambako utazikwa kesho,? akasema. Kabla ya kifo chake, Mheshimiwa Chifupa anakumbukwa jinsi alivyokuwa akitoa hoja kadhaa nzito nzito bungeni.

Marehemu alikuwa akiwashangaza wengi kutokana na ujasiri wake wa kuibua mambo mazito kama yale ya kujitolea kuongoza mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya waziwazi, jambo ambalo wazoefu wengi wamekuwa hawaonekani kulifanya.

Pia alikuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya vijana, kukemea rushwa na kupigania haki za wanawake.

Historia ya mbunge huyo aliyekuwa miongoni mwa waheshimiwa wenye umri mdogo zaidi katika bunge la sasa inaonyesha kuwa amepata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Ushindi ya Jijini, kisha akajiunga na shule ya sekondari ya Kisutu. Alipomaliza kidato cha nne, Amina Chifupa alijiunga kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Makongo kabla ya kuhitimu na kwenda kujiunga katika Chuo cha Uandishi wa Habari cha Royal College cha Jijini Dar es Salaam. Inaonyesha historia yake kuwa tangu akiwa shuleni, marehemu Amina alishaanza kazi ya utangazaji wa redio. Mwaka 2005, Amina Chifupa alitwaa ubunge baada ya kufanya vyema katika uchaguzi mkuu kupitia tiketi ya viti maalum (Vijana-CCM).
Hadi anafariki dunia jana usiku, marehemu Amina Chifupa alikuwa na umri wa miaka 27.

6 comments:

Anonymous said...

Lakini wengi wao wanasema ni "mchezo mchafu" aliochezewa huyo binti mdogo ba baadhi ya vingunge ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hasa huyu Emmanuel Nchimbi.
Lakini all in all, watu wengi wanarudi tena kwa bw.Nchimbi kama ilivyokuwa wakati wa kifo cha Ipyana Malecela kwamba alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakiwania cheo cha mwenyekiti a vijana, kijana wa mzee Malecela aliondoka kana kwamba pamba inavyotekea kwa sekunde na moto.
Kwa nini watu wanamuhusisha nchi na kifo cha Amina?
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa unasadikiwa kuwa Marehemu Amina tayari alishajijengea mizizi tosha ya kuhakikisha kua anakuwa mwenyekiti wa umoja wa Vijana ka kufanya kampeni nzito, hali ambayo ilimkatisha tamaa bw.Nchimbi ambae indaiwa tayari ameshakuwa na mtu wake mfukoni.
Ilidaiwa awali Marehemu Amina alikwenda kuomba ushauri wa kutaka kugombea nafasi hiyo kwa Nchimbi na huyu bwana alimueleza bayana kabisa marehemu kwamba bado hajapevuka kisiasa kushika nafasi hiyo nzito kwa Vijana wa CCM.
Hali ambayo Amina alipingana nayo na kumuhakikishia kwamba yeye amekomaa na kama bado badi atajivunza humo ndani atakaposhika nafasi hiyo, huku Nchimbi akimpiga mkwara kwamba tayari nafasi hiyo ina mwenyewe tangu maka 2005.
Marehemu Amina baada ya hapo alitoka katika mazungumzo hayo kwa nguvu mpya, kasi na hari kuhakikisha kuwa anafanya kampeni kabambe kabla ya muda kuhakikisha anachukua nafasi hiyo.
Iliyobaki huku nyuma ni Nchimbi na kundi lake kuhakikisha kwamba huyu binti wanammaliza kisiasa, ndiyo majungu yalipoanza kwa kuhusishwa kwake kutembea nje ya ndoa na mbunge kabwe zitto wa Chadema.
Baada ya saka hilo, Amina aliahidi kumwaga mchele hadharani pale katika ukumbi wa idara ya habari maelezo, kisa cha mumewe kumuacha na ilidaiwa kwamba alikuwa anataka kumtaja bwana Nchimbi, lakini kutokana na ushauri wa wazee wake aliamua kusitisha uamuzi wake, lakini alitumia simu yake ya mkono kumtumia bwana Nchimib ujumbe mfupi ulisomeka;
Ujumbe huo ulisomeka; “Alichounganisha Mwenyezi Mungu binadamu hawezi kukitenganisha. Nakuheshimu sana kama kiongozi wangu, Mwenyekiti wangu, Naibu Waziri, M-NEC, M-CCM, mkubwa wangu kiumri, mbunge na kadhalika. Nimesikitishwa sana na jitihada za kutaka kuvuruga ndoa yangu, nakutakia kila la heri, lakini usisahau malipo ni hapa hapa duniani na kila mwenye kufanyia wenzake mabaya na yeye hulipwa kwa ubaya. Nampenda sana mume wangu na ntailinda ndoa yangu kwa gharama yoyote cko tayari kumpoteza, mi ni zaidi ya mwanamke. Asante sana, kila la heri na kazi njema katika kulifanikisha hilo, wizara yako nyeti sana, ina mambo mengi sana. Bye

Hakika hatujui Bw. Nchimbi alimjibu nini Amina, lakini baada ya hapo hatukumsikia tena Amina,massage hii ya Amina ni ushahidi tosha Nchimbi alikuwa hana mahusiano mazuri na huyu bwana Nchimbi.

Inadaiwa kuwa bana Nchimbi sasa hivi ni miongoni mwa watu wanaodaiwa kuogopwa kama ukoma na wabunge wenzake hata mawaziri kwa ukalumanzila,lakini hakuna mwenyewe ushahidi wa kutosha,Je Amina ametolewa kafara? wanasiasa wakubwa wa Marekani wanasema Politics is of the heart as well as of the mind,many people don't care how much you khow until they khow how much you care.

Anonymous said...

Niliwahi kusema kabla na nasema tena, huyu binti ameucheza mpira wa siasa na wanaume wenye majungu, wivu na chuki. Hawapendi kuona maendeleo ya vijana kama hawa katika maswala ya Siasa.

Amina Chifupa alikua ni tishio kwao, amekuja kwa kasi na ujasiri, kwao wao ni tishio, ijapukuwa mimi si mpenzi wa chama tawala, lakini hii inaonyesha dhahiri dosari kubwa ndani ya hiki chama, watu wakishakalia madaraka hawataki kuyatoa, wanahisi kwao ni urithi si kazi tu.

Habari hizi kama ni za kweli kama unavyozieleza any.. hapo juu, basi itakua ni dhahiri kwamba ni sehemu ya chanzo cha hatma Amina Chifupa.

By Mchangiaji.

Unknown said...

Daima hatutasonga mbele! uongozi si urithi ni kazi na hapa ndipo Watanzania na Waafrika kwa ujumla tunapo kosea vibaya.
Ni kijana ambaye wakati wa uteuzi wake kuna waliodiriki hata kusema alishindwa kufaulu form six atafanya nini bungeni? ni swali ambalo alilijibu kwa vitendo na ufanisi mkubwa.
Na hii inadhihirisha wazi kwamba kusoma sana si kuwa na akili sana.
kwa kipindi kifupi tu alichotumikia nafasi yake amefanya mambo ambayo hta wa kabla yake walishindwa kuyafikia, lakini tukae tukijua kwamba kizuri hakidumu. Mengi na wengi wamehusishwa ktk kifo chake na naungana na mengi ktk hayo kwani si mageni na imekuwa ni kawaida ktk maisha ya mafanikio ya Kitanzania.
Tulikupenda mungu akakupenda zaidi.
Hakika sote ni wa mungu na kwake tutarejea!!
AMIN!

Chemi Che-Mponda said...

Sunday, asante kwa maoni yako. Kwa kweli kufeli shule siyo kufeli maisha. Marehemu Amina amethibitisha hayo.

Ukweli marehemu alikuwa celebrity na ametutoka mapema mno. Lazima yatasemwa mengi kuhusu chanzo cha kifo chake.

Kwenye maoni hapa kwenye blogu nimeona kuna watu wanajifanya papparazi kuwa wanajua chanzo chake. Amina anaendelea kuwa celebrity katika kifo.

Mola amlaze marehemu Amina mahali pema peponi. Amin.

Anonymous said...

Mheshimwa Emmanuel Nchimbi alimtongaza na akakataliwa na Amina, akamchimba na kumzushia na kumtia fitina kwa mumewe eti anatembea na mheshimiwa mwengine anaitwa Zitto, Mpakanjia akatoa talaka tatu, baada ya hapo Amina akwa anaumwa sijui depression, kapoteza kumbukumbu mpaka Mwenyezi Mungu kachukua kiumbe chake. But I believe there is more to it than that... kwasasa na tusikilize tutayapata.

Ina lillahi wa ina illahi rajiun

Anonymous said...

Sunday ulitegemea nini kwenye siasa , zaidi ya fitna ,chuki, mizengwe, ubabe, majungu na mengineyo mabaya kama hayo. Siasa ina uzuri wake kwa wanaopenda umaarufu lakini ukubali tu ukipiga wenzio zengwe lazima na wewe upigwe zengwe. Kila kitu huenda hatua kwa hatua, mtoto hatembei bila kwanza kukaa chini, kisha atambae halafu mengine yanafuata. Hata kama tunapenda vipi maendeleo yake ya haraka ni lazima apitie hatua hizo....Hiyo ndiyo siasa mwanangu.