Monday, November 05, 2007

Oprah Jihadari!


Hii skandali ya shule ya Oprah sasa unaingia kwenye ukurasa mpya. Kuna baadhi ya wa South Africa wanamwonya Oprah kuwa awe mwangalifu. Wanasema amezidi kuleta umarekani na ufahari kwa hao wasichana waliotoka kwenye familia maskini.

Wanasema ni kawaida wasichana na hata wavulana waliokosa nidhamu kuchapwa kwa mila zao. Wengine wanasema kuwa wana wasiwasi kuwa madai ya unyanyasaji ya hao wasichana si ya kweli. Wana hofia kuwa msichana akimchukia mkubwa basi watasema uwongo juu yao na kwa vile Oprah ni mtu mzito mtuhumiwa hatasikilizwa.

Wengine wanasema kuwa Sangoma (waganga wa kienyeji) zao wana dawa kali, Oprah anaweza kuamka siku moja ajikute kichaa au kapofuka.

Oprah alifungua shule kwa nia nzuri mwanzoni mwa mwaka huu. Watu wanacho hofia ni kuwa ametenga hao wasichana anaowaita binti zake na kuwalea kifahari mno. Pia watu wana hofu watakosa kulelewa kikwao.

Majuzi Oprah alimpa kila msichana wa shule hiyo, simu ya mkononi enye 'feature' inayomwezesha kupiga simu moja kwa moja Oprah Marekani.

Mmoja wa matron wa shule hiyo, Tiny Virginia Makopo, amefunguliwa mashtaka ya kupiga wasichana 15. Pia wasichana wandai kuwa alitaka kufanya ngono ya kishoga nao.
Mwalimu Mkuu, wa shule hiyo, Dr Mbulelo Mzimane, naye amefukuzwa kazi na Oprah kwa madai kuwa hakusikiliza malalamiko ya wasichana wa shule hiyo.

Oprah ametuma 'Trauma Specialist' kutoka Marekani kwenda kutoa tiba kwa hao wasichana kusudi wasipate majeraha ya fikra ya kudumu.



10 comments:

Anonymous said...

Oprah anataka kutengeneza madoli siyo watu wenye akili zao. Hao watakuwa mapuppet wake.

Anonymous said...

I am a South African woman. Yes Oprah did a good thing when she opened this school. But in a way it is not good. She is pampering and spoiling a few girls. They will most likely leave this country after they are educated. They already act like rich girls.

Oprah could have used the same money to build smaller less posh schools. She could have used the same money to help but uniforms and pay fees for the thousands of children struggling here.

Anonymous said...

Hiyo mitoto itajakuwa midebwedo, we subiri tu!

Anonymous said...

kama nilivyosema huko nyuma-Oprah ana "micro-manage" hii shule, pia swala la mila na utamaduni wa mwafrika naona anataka kuliua. Hili swala la kumpa kila mtoto cell-phone sasa ndio kuwadekeza hawa watoto!!

Anonymous said...

Anaharibu hao mabinti. Wakimaliza pale watafanya nini? Watakuwa na expectations za ajabu na maisha wakikosa wataanza kujiua.

Anonymous said...

Chemi, hapo shuleni wanasoma bure au ni private school? Au kama ni bure nani mfadhili wao?
Niliona ktk news mama mmoja (mzazi) mwenye mtoto hapo akimsifia sana Oprah!

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 9:35am, hao wasichana wanasoma bure kabisa. Wanalipiwa kila kitu na Oprah. Wakienda kwao likizo wanapelekwa na gari la shule na wanachukuliwa na gari la shule. Hiyo shule ni ya kifahari malazi ni mazuri kuliko hoteli za bei ya juu duniani kama Waldorf Astoia.

Anonymous said...

kiwi cha macho tuu.
Sijui kwanini Oprah aliichagua South Africa na wala siyo Benin, Mali, Sudan, au Angola.

Nisaidieni mawazo.

Anonymous said...

Au sijui kwanini shule hiyo hakuijenga kusaidia watoto wa New Orlean waliopigwa na hurricane Caterina

Anonymous said...

Oprah alichagua South Africa kwa sababu alidanganywa kuwa anafanana na wa huko na asili yake ni uzulu. Skip Gates wa Harvard alimfanyia DNA test. Kumbe kwao ni Liberia. Wanahitaji msaada mkubwa zaidi Liberia kuliko South Africa.