Sunday, March 21, 2010

Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje Nchini Algeria

Kumradhi, taarifa hii nilikuwa nayo kwenye e-mail tangu 3/15/10. Taarifa inatoka kwa mwanafunzi wa kiTanzania anaye soma Algeria. Mheshiwa Membe alikuwa ziarani Algeria mwanzoni mwa mwezi huu. Mnaweza kupata picha na habari zaidi kwa Kaka Michuzi.


*************************************************************************

Na MDurban the King


ZIARA YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA TANZANIA NCHINI ALGERIA :
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA TANZANIA MHESHIMIWA BERNAD MEMBE AITEMBELEA ALGERIA NA KUFIKISHA UJUMBE MAALUM WA RAISI MHESHIMIWA JAKAYA KIKWETE KWA RAISI ABDUL AZIZ BUTAFRICA.MHESHIMIWA MEMBE ALIAMBATANA NA UJUMBE WAKE WA WATU WANNE AMBAO NI MBUNGE WA MBEYA, BALOZI ANAESHUHULIKIA MASUALA YA AFRICA, DR. LEONIDA MUSHUKOLWA NA MSAIDIZI WA WAZIRI.

PIA MHESHIMIWA MEMBE ALIWEZA KUKUTANA NA WANAFUNZI WA KITANZANIA WANAOSOMA NCHINI ALGERIA.

MHESHIMIWA MEMBE ALIONESHA MFANO WA KUIGWA SIO TU KWA TANZANIA BALI KWA NCHI EAST AFRICA KWA UJUMLA, KWA KUONESHA KUJALI RAIA WA NCHI YAKE KWA KUFANYA NAO KIKAO KILICHOCHUKUA ZAIDI YA MASAA MANNEE AKIWAELEZEA MASUALA YANAYOHUSU NCHI YAO KISIASA, KIUCHUMI NA KIJAMII, LICHA YA KUONESHA KUWA KIUTENDAJI TU BALI NI MTU ANAYEJUA MAJUKUMU YAKE PIA.

MFANO MMOJA YA MASUALA ALIYOYAZUNGUMZIA NI TANZANIA NA MGOMBEA BINAFSI, WATANZANIA KUWA DUO NATIONALITIES NA KUANZISHWA KWA DIASPORA YA WATANZANIA WANAOISHI NJE YA NCHI, MASUALA YA WABUNGE NA MENGINE MENGI MAZURI KAMA UTALII NA KADHARIKA.
PIA ALIWEZA KUPOKEA MAONI YA WANAFUNZI HAO JUU YA NAMNA GANI YA KULIENDELEZA TAIFA LAO,
MHESHIMIWA MEMBE WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA TANZANIA AMEONESHA KUWA MFANO WA KUIGWA KUTOKANA NA KUJALI RAIA WAKE BILA KUBAGUA RIKA WALA KABILA

TANZANIA INABAHATI YA KUPATA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WAZURI MFANO MWENGINE KAMA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE BALOZI SEIFU IDDY AMEKUWA AKISIFIWA PIA NA WANAFUNZI HAO, KWA UCHAPA KAZI WAKE NA UTU WAKE.
PIA MHESHIMIWA MEMBE ALIWEZA KUCHANGIA CHAMA CHA WANAFUNZI HAO ZAIDI YA DOLA 2000 ZA KIMAREKANI, WANAFUNZI HAO WALIOMBA MAWAZIRI WENGINE WAWE MFANO WA KUIGWA KTK UFANISI WAO WA KAZI NA KUYAJUA MAJUKUMU YAO KWA RAIA WAO.

AIDHA TANZANIA IEMKUWA NCHI RAFIKI WA ALGERIA KWA MUDA MREFU SANA!!WANAFUNZI HAO WALISISITIZA NCHI YA TANZANIA KUWA NA URAFIKI ZAIDI NA NCHI KAMA ALGERIA KWANI ZINAMANUFAA MAKUBWA ZAIDI ENDAPO NCHI HIZO ZIKIZIDISHA URAFIKI KULIKO TANZANIA KUWA NA URAFIKI NA NCHI KUBWA ZA KIBEPARI AMBAZO ZIMEKUWA NYONYAJI KWA NCHI MASIKINI.

CHI NYINGI MASKINI ZA AFRICA ZIMEKUWA ZIKIJISAHAU NA KUOMBA MISAADA AMA KUZIGEUKIA NCHI KUBWA ZIKIDHANI NDIYO SOLUTION YA KUMALIZA MATATIZO YAO WAKATI KUNA NCHI NDOGO AMBAZO ZINAWEZA ZIKAZISAIDIA NCHI MASKINI ZAIDI KULIKO NCHI BEPARI AMBAZO MARA NYINGI ZINAKUWA KIMASLAHI ZAIDI KULIKO FAIDA KWA NCHI MASKINI.

MFANO MZURI WA MAMBO WALIYOISHAURI SERIKALI NI ALGERIA INAWEZA KUTOA SCHOLARSHIP ZAIDI KWA TANZANIA. ALGERIA NI SOKO ZURI KWA KUUZA BIDHA ZETU ZA KILIMO KAMA MATUNDA,VIUNGO,CHAI KAHAWA N.K. PIA ALGERIA INAWEZA KUWEKEZA TANZANIA KTK NYANJA YA VIWANDA KTK BIDHAA ZA KILIMO N.K, INAWEZA KUISAIDIA TANZANIA KTK MASUALA YA GESI KWANI NI IMEKUWA NAUTAALAMU WA MASUALA YA NISHATI KWA MUDA MREFU SANA. ALGERIA IMEKUWA IKITOA GESI NA MAFUTA NA NDIYO INATEGEMEA PATO LAKE KUBWA KTK BIDHAA HIZI,ALGERIA NI MOJA YA NCHI ZINAZOTOA GESI KWA WINGI DUNIANI.

PIA ALGERIA INAWEZA KUSAIDIA TANZANIA KTK SUALA LA MIUNDO MBINU MFANO KUPUNGUZA TATIZO LA FOLENI TANZANIA KWA KULETA WATAALAMU WAKE WA KUJENGA BARABARA ZA JUU NA CHINI YA ARDHI KWA GHARAMA NAFUU,KUWEKEZA KTK USAFILI WA RELI TOFAUTI NA ILIVYOSASA KWA KUTEGEMEA NCHI KAMA INDIA AMBAYO KIMIUNDO MBINU KTK RELI NA BARABARA IPO NYUMA KULIKO ALGERIA.

PIA WAMETOA PROPOSAL YA KUIOMBA SERIKALI IJENGE BARABARA ZA MITAANI(ZA NDANI)NDIYO SOLUTION PEKEE YA KUPUNGUZA WIMBI SUGU LA FOLENI,MFANO WALIOUTOA BARABARA YA NEW BAGAMOYO KUIPANUA PEKE YAKE BILA KUTENGENEZA BARABARA ZA NDANI HAITOSHI KWANI RAIA WOTE WATAKAOTOKA BAGAMOYO,TEGETA KUELEKEA MJINI WATAITAJI KUPITA NJIA MOJA KWENDA MJINI KWAHIYO SOLUTION NI KUJENGA NJIA HIZI ZA MITAANI ZITAPUNGUZA FOLENI KWA WATUMIAJI HAO KWA KUZITUMIA,MFANO ZIJENGWE NJIA ZA NDANI KUANZIA MWENGE KIJITONYAMA,MAKUMBUSHO,MWANANYAMALA ZIJEZITOKEE KINONDONI. HII NDIYO SIRI PEKEE YA KUPUNGUZA FOLENI NA BARABARA NYENGINE ZOTE JIJINI ZINAHITAJI HII PROJECT,MIPIA ALGERIA INAUWEZO WA KUISAIDIA TANZANIA MADAKTARI KWA GHARAMA NAFUU.

SUALA AMBALO WANAFUNZI WAMEONESHA MSISITIZO ZAIDI NI TANZANIA KUTIZAMA SOKO LA WATALII KUTOKA ALGERIA, KWANI IMEKUWA IKITOA WATALII ZAIDI KULIKO KUINGIZA, KWA HIYO WALIHAMASISHA TANZANIA KUTIZAMA NAMNA YA KUPUNGUZA URASIMU WA KIMAWASILIANO KTK YA NCHI HIZI MBILI MFANO UPATIKANAJI WA VISA, USAFIRI WA DIRECT WA ANGA.

PIA WALIISHAURI WIZARA YA UTALII IBADILISHE MFUMO WA UENDESHAJI UTALII NA KUWA ENDELEVU(SUSTAINABLE TOURISM/TOURISME DURABLE) KWA KUENDELEZA UTALII TANZANIA NZIMA UKANUFAISHA WATANZANIA WOTE,SERIKALI KUJARIBU KUWEKA SERA NZURI ZA UTALII NA KULINDA MALI ASILI ZETU,PIA WALIONGELEA SUALA AIR PORT YETU KUWA PICHA NZURI KWA KUPUNGUZA UPOTEVU WA MIZIGO YA WASAFIRI NA KUOMBA RUSHWA,KWANI IMAGE HALISI YA TANZANIA INAANZA KUONEKANA MLANGONI HAPO,PIA WALITOAMAPENDEKEZO YA SERIKALI KUFUNGUA UBALOZI AMBAO UTARAHISISHA MAMBO MENGI BAINA YA NCHI HIZO MBILI.

PIA WALIMPONGEZA RAISI KWA KUIPA SECTOR YA UTALII KIPAUMBELE NA WAZIRI WA UTALII NA MALI ASILI KWA KUJITAIDI KUBUNI NA KUENDESHA UTALII VIZURI KULIKO HAPO AWALI, PIA WANAFUNZI HAO WALIISAURI SERIKALI KWA KULITIZAMA VIZURI SUALA LA MGOMBEA BINAFSI KWANI WATANZANIA WANAITAJI KUELEMISHWA JUU YA SUALA HILO KABLA YA SUALA LA MGOMBEA BINAFSI KUPITISHWA.

PIA MH : MEMBE ALIAHIDI KUSHUHULIKIA MATATIZO YA WANAFUNZI HAO KAMA VILE MATATIZO YA KUCHELEWESHEWA POSHO ZAO NA BODI YA MIKOPO KWANI LIMEKUWA TATIZO SUGU, TATIZO LA EQUVALENCE YA VYETI VYAO PINDI WAMALIZAPO MASOMO YAO.

2 comments:

Anonymous said...

Nchi yetu imelala mnafikiri kuishauri mazuri ndiyo utekelezaji?anyway good done

Anonymous said...

Tanzania ni nchi iliyojaa mafisadi kuna kila kitu lakini sisi ni maskini!!tuliwakaribisha india kuwekeza kwenye usafiri wkt wao pia wanashida ya usafiri