Sunday, March 21, 2010

Sinema - On the Mean Streets

Jumamosi niliigiza katika sinema fupi iitwayo 'On the Mean Streets'. Sinema hii imetungwa na mwanafunzi Brian Goodwin ambaye ni mwanafunzi Emerson College hapa Boston. Mimi niliigiza kama mwalimu wa Kiingereza wa Sekondari. Nakutana na kijana wa kizungu ambaye anadhani maisha ya Roxbury wa Boston ni ya ghetto na weusi wote huko ni maskini. Naishia kuchukia jinsi kijana wa kizungu alivyokuwa na mawazo finyu kuhusu Roxbury. Sinema inempigwa kama 16MM Format.

Kati ya Shots. Mimi kama Mwalimu Cheryl. Brian Goodwin aliigiza kama Pinkerton, mzungu mwenye mawazo finyu juu ya Roxbury.
Mshika Boom (Sauti), rafiki yangu na msanii mwanzangu katika kikundi cha Oscar Micheaux family Theater Charles 'Matumbi' Jackson, mimi na Brian. Charles aliigiza kama mlevi.

Tumemaliza shoot! Hapo ni mtaa wa Parker St. karibu na Roxbury Crossing. Huyo binti aliyeshika Camera alipata taabu sana maana ilikuwa nzito kweli. Walikuwa na tgripod, lakini kwenye script waliandika scene ipigwe kwa Handheld (Kamera Mkononi). Lakini binti alikuwa 'rpo' alisema ataipiga handheld!

1 comment:

Anonymous said...

Hongera Da Chemi!