Saturday, March 27, 2010

Kumbe Kweli Michael Jackson Alikuwa Anajichubua!

Michael Jackson kabla hajajichubua
Michael Jackson baada ya kujichubua


Ukweli umefichuka. Kumbe ni kweli Michael Jackson alikuwa anajichibua na makrimu, ndo maana rangi yake iligeuka kuwa kama mzungu. Jackson alikuwa anaumwa ugonjwa wa Vitiligo ambao muathirika anakuwa na mabaka mwilini. Ni mweusi lakini nakuwa na vipande vikubwa kama ngozi ya kizungu. Mimi niliona vigumu kuamini habari ya vitiligo. Kwanza nafahamu watu wengi hapa Marekani ambao ni waathrika na hata wakipaka make-up kuficha mabaka utawajua tu. Kumbe Jackson aliaamua awe mzungu kimoja na afute hayo mabaka meusi!

Leo kuna habari kuna tube kibao za krimu za kujichubua zilikutwa nyumbani kwa Jackson alivyofariki. Wanasema kuwa watu walijaribu kuzificha. Miaka ya 80 mwanzoni kulikuwa na madai kuwa Michael Jackson alikuwa anaoga katika madawa ya kujichubua na usikua alikuwa anajipaka makrimu kibao za kujichua na kusudi ziwe kali zaidi alikuwa anafunika mwili waka na plastiki (cling wrap) wakati analala. Kulikuwa na habari kuwa Jackson alisema kuwa anachukia weusi wake. Huenda ni kweli maana alichonga pua yake kuwa kama ya mzungu.
Kwa habari zaidi someni:7 comments:

Anonymous said...

Ukiwa mpumbavu utajichubua.

Anonymous said...

Dah! Mbona alijiharibu hivyo!

Kaka Trio said...

Nini kipya hapo ambacho tulikuwa hatukijui tayari? ni nani alikuwa hajui kama maiko Jakison kachonga pua? ni nani alikuwa hajui maiko anapenda uzungu?

watila said...

si mujinga tuu amekaa kama kima sasa si unona ankoo

Anonymous said...

Mbona hiyo habari ya kujichubua iko toka longi. Aliamua kujichubua ili kuondoa mabaka meusi ya vitiligo ili ibaki rangi nyeupe tu. Hata hivyo ukiangalia rangi yake utagundua sio weupe wa kawaida. Ni weupe wa vitiligo

Anonymous said...

kipya hapa ni kwamba kuna wapumbavu waliokuwa wanaamini kwamba maiko jakichoni alikuwa na matatizo ya ngozi na si wala kujichubua kulikomfanya ageuke mzungu koko. Lakini uzungu ulimpendeza sana

Anonymous said...

na huyu swuwain angekuwa mzungu weusi marekani wangemkoma. Huyu angekuwa mtu mbaya kuliko hata J. Edgar Hoover