Monday, July 12, 2010

Mabomu Yaua Watu 74 Uganda

Watu walioenda klabuni kutazama Mashindano ya Kombe la Dunia huko Kampala, Uganda wameuaua katika shambulizi la mabomu.

Kwa sasa kundi fulani la magaidi kutoka Somalia wanasema kuwa wao ndo walitenda huo unyama. Wamediriki kufungua hata website ya kupokea pongezi!

Jamani, mnaua waafrika wenzenu, binadamu kwa ujumla halafu mnataka kupongezwa? Kweli mwisho wa dunia iko karibu!

Mungu alaze roho za waliokufa mahala pema mbinguni. AMEN. Mungu wape nguvu familia ya marahemu katika kipindi hiki kigumu.

Kwa habari zaidi someni:

http://news.bbc.co.uk/2/hi/world/africa/10605457.stm

http://edition.cnn.com/2010/WORLD/africa/07/12/uganda.bombings/index.html?hpt=P1&fbid=4CVcBwhbh2z

No comments: