Tuesday, July 06, 2010

MV Massachusetts Karibu Izame Boston Harbor!!!

Meli MV Massachsuetts inayozungusha watu kutalii kwenye visiwa vya bandari ya Boston, ilipata ajali siku ya jumamosi 7/3/10. Karibu izame baada ya kugonga kitu karibu na Deer Island.

Unauliza kwa nini nimeona ni muhimu kubandika habari hapa? Ni kwa sababu ni meli ambayo kanisa letu la International Gospel Church ilikodi and kufanya Dinner Cruise mwezi wa nne. WaBongo waliopanda wanaijua. Kweli maombi yanasaidia maana tulianza cruise na maombi na kumaliza kwa maombi! Tulirudi salama. Hiyo ajali ingetokea wakati imejaa waafrika ambao wengi hawajui kuogelea ingekuwa balaa!

Wakati wa ajali meli ilikuwa na abiria 174. Wote waliokolewa. Watu wanne waliumia. Ukipanda boti hakikisha unajua Lifejackets ziko wapi!

Wataalam wanasema meli imekuwa Write-Off!

Kwa habari zaidi someni:


2 comments:

Anonymous said...

Duh nimeona kideo wanaokoa watu. Kweli hali ingekuwa mbaya kama wasigingetokea kuwaokoa. Hizo lifejackets ni muhimu pia. Hivi Bongo kuna lifejackets za kutosha kwenye meli zetu?

Anonymous said...

Wabongo wanagejitosa kwenye maji wkidhani ni mwisho wa dunia kwikwikwikwi!