Saturday, July 17, 2010

PASTOR ABIUD & CATHERINE Watakuwa Texas


Kwa heshima na unyenyekevu, ninapenda kuwatangazia watanzania na watu wote wanaoishi katika katika jiji hili la Dallas -Texas kwamba kutakuwa na SEMINA ya siku mbili ya neno la Mungu katika jiji letu la Dallas-Texas. Semina hii itaendeshwa na watumishi wa Mungu PASTOR ABIUD & CATHERINE PAMOJA NA EV.LENATA KUTOKA TANZANIA. Watumishi wa Mungu Mr&Mrs Abiud wanaheshimika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kutokana na wito wao wa kumtumikia Mungu kwa upendo na unyenyekevu mkubwa.

Kwa sasa hawa watumishi wameweka maskani yao katika jiji la Kansas -Missour (USA).Ninaomba kwa kila mtu atakaesoma tangazo hili amkaribishe mwenzake.Pamoja na semina ya Mungu, watumishi hawa watapata nafasi ya kutoa ushauri kwa watu wanye matatizo binafsi na kuwaombea.Kama unahitaji ushauri wa ndoa,uchumba, mahusiano na mambo kama hayo usisite kutujulisha ili utengewe muda wa kukutana nao ana kwa ana..

Kumbuka tarehe ni 17-18/7/2010-Jumamosi na Jumapili ya wiki hii.

Mahali ni-Umoja Church,127217 Hillcrest Rd,Dallas Texas 75230

Muda ni:Saa kumi na moja mpaka saa mbili usiku (11-2 usiku) 5pm 8Pm.

Maelezo zaidi;214 554 7381,682 552 6402,214 773 6697.

NB:Kutakuwa na chakula maalumu pamoja na vinywaji kila baada ya semina ili kufahamiana zaidi.

Karibuni wote
Uongozi wa kanisa la Umoja Dallas Texas.

1 comment:

Baraka Mfunguo said...

Aliimba wimbo wa kumsifu Mungu. Alimfagilia pia mkewe cheupe. Mama Abihudi ni mwasisi wa huduma ya Rising Daughters of Abraham. Safi sana.