Wednesday, July 28, 2010

Wake wa Chifu!

Jamani, Chifu anakuwa na wake wangapi? Hao wanawake walikuwa wake wa Chifu fulani huko Dodoma. Naona mke wa missionary alienda kuwafundisha kuwa 'civilized'.

9 comments:

Anonymous said...

Chemi, karibu wake sita hivi ni wajawazito!

Huko Ikizu, Musoma, Chifu Makongoro, alikuwa na wake 72 wakati wa uhuru!

Kulikuwa na uvumi kuwa watotowake wa kiume wakubwa walikuwa wakifanya ngono na "mama zao wadogo" (yaani, wake wachanga wa Chifu)!

Anonymous said...

Kabla ya Uhuru ilikuwa jambo la kawaida akina mama kutembea vifua wazi. Fikiria kama bado wangekuwa wanatembea vifua wazi. Tusingeona ajabu kuona matiti. Sasa huyo chifu aliwatosheleza kweli wote hao? MHHH?

Kaka Trio said...

Enzi hizo mambo yoote kwa uwazi tu kwa Mzee King Mswati, sio siku hizi mawaziri wana vimada idadi hiyo hiyo au pangine zaidi lakini hakuna ajuaye!

Mziwa kuwa wasi sio kitu cha ajabu huko vijiji hadi leo akina mama wanaacha maziwa wazi tu. Wazungu ndio wanapenda kuficha maziwa lakini nyeti zingine wanaziacha nusu uchi. Utakuta mdada kaficha kila kitu lakini vijivazi anavyokuvalia kwene maungu ya karibu na chini ya kituvu we acha tu!

Kwa ivo kalcha yetu wanaume vifua wazi na wadada vifua wazi vile vile, usawa mbele kwa mbele.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hakijabadilika kitu. Kama isingekuwa kujifichaficha tungeona mengi. Ndiyo maana niliungana na Jacob Zuma alipowajibu waliokuwa wakichonga sana kuhusu ndoa yake ya hivi karibuni kwa kuwaambia:

“There are plenty of politicians who have mistresses and children that they hide so as to pretend they are monogamous. I prefer to be open. I love my wives and I am proud of my children.”

Angalizo kamili liko hapa:

http://matondo.blogspot.com/2010/01/zuma-yuko-sahihi.html

Anonymous said...

kwani kila la wazungu ndio civilized? basi katika hilo umechemsha. kuwa na wake wengi ndio civilized? na wale wanaojidanganya kuwa na mmoja matokeo yake huwa na vimada na nyumba ndogo zaidi ya 10. sasa bora lipi kuwa na wake wanaotambulika au kuwa na malaya wa kufanya nao ufuska kila mtaa, kazini, kwenye biashara mbali na kwenye vyama vya siasa?

Anonymous said...

Civilized ndo kuvaa hayo manguo enye joto kwenye jua kali? Lakini unakuta Chifu alitaka mke wake avae kama huyo missionari!

Anonymous said...

Picha ilipigwa mwaka gani? Kuna moja anafanana na jirani yangu Maimuna! Wallahi!

Anonymous said...

Da Chemi
Mbona mandhari si ya Dodoma?Kule nyumba zao ni za tembe na siyo vibanda vya nyasi.Lakini yaweza kuwa labda enzi hizo.

Anonymous said...

halafu nyie watu sio maziwa ni matiti ambayo yanatoa MAZIWA msichanganye lugha au maana halisi