Tuesday, August 24, 2010

Barabara kati ya Tunduru na Masasi

Nimeona hii picha ya barabara kati ya Tunduru na Masasi. Nimeipenda sana. Imenikumbusha mbali. Picha ilipigwa na mtalii kutoka Uholanzi.

8 comments:

malkiory said...

Chemi: Barabara hii imefanana kabisa na ile ya kwenda kwetu Mbulu toka Arusha. Wanasiasa wakongwe akina Philip Marmo wamejisahau kabisa kuleta maendeleo pamoja na kuwepo kwake kwenye ngazi za juu serikali toka enzi za Nyerere.

Inasemekana mji wa Mbulu ulizinduliwa siku moja na jiji la Nairobi, lakini leo hii kama utafanikiwa kuzilinganisha utabaki kucheka.

Mbulu ni makao makuu ya wilaya, lakini usishangaa hata western union pale ipo kwa jina tu, kwani hata shilingi 100,000 hawana kwenye benki yao.

Anonymous said...

Ningejua njia ni nzuri hivi ningeenda Napacho. Ni juzi tu nimerudia Masasi mjini niihofu njia ni mbaya. Home sweet home.!

Yasinta Ngonyani said...

ndogo wangu hapo njila yinofu sana kuhamba kumbamba-bay ngati yitonyili mwee taabu sana.

Anonymous said...

Nimeipenda sana Taswira hii ya maskani.

Msaada kwatuta.

Soon nataka kwenda Home sweet Home Nachingwea. Ati vp bararabara ya Dsm-Kibiti-Lindi-Masasi hadi Nach,inaweza fikika kwa gari dogo kama Spacio?

Nawasilisha kwenu Wakunyuma.

Anonymous said...

Asante kwa kunikumbusha home. Kutembea na ndala mavumbi miguuni, huko Ugali wa moto na kitoweo kizuri cha maharage freshi inaningojea.

Anonymous said...

Njia ni nzuri sana huwezi kuamini, mimi nimetumia gari ndogo SUBARU FORESTER turbo. Ilituchukua saa 7 mpaka Lindi. Kipande kimoja tu ni kibaya kina kilometa kama 60 hivi kinaanzia nyuma kidogo ya nyamwage na kinaishia somanga. Hapo speed ni kama 40 tu hivi, barabara ndo inatengenezwa. Ukitoka hapo ni lami tu mpaka mtwara au lindi na masasi.Kumebadilika sana nyumbani, haswa Mtwara mjini.

Anonymous said...

Spacio inaweza kwenda kama hakuna mvua na hicho kipande kinachotengenezwa kitakuchelewesha kidogo maana itabidi utembee taratibu sana.

Anonymous said...

Ahsanteni sana wadau kwa kunipa mwongozo huo. Najipanga, then natoka bwii, linachomoza navuka Nkapa Bridge.

Haya ndo maendeleo tunataka. Che Nkapa, daima Kusini tunamkumbuka kwa mengi. Enzi za kulala Ikwiriri- mbu mara magari kutumbukia mtoni...du thax n God bless you guys!