Thursday, August 19, 2010

Tatizo Sugu la Msongamano wa Magari Dar


Nimepata hii kwa email.

Imeandikwa na Mdau

Malkiory William Matiya

Kuna haja ya kutafuta tiba ya gonjwa hili sugu la msongamana wa magari
ndani ya jiji la Dar es salaam.

Pengine hatua za tiba hii inaweza kuwa mwiba kwa wahusika au walengwa
wa chimbuko la tatizo hili, lakini tukumbuke kwamba maendeleo yeyote
au mabadiliko yeyote hayakosi kuwa na gharama zake, ninapoongelea
gharama hapa ninamaanisha hasara kwa wale ambao wanamiliki vyombo hivi
vya usafiri ambavyo ndivyo chanzo cha msongamano na pengine ajali za
mara kwa mara zinazosababishwa na baadhi ya vyombo hivyo vya usafiri
kutokuwa kwenye hali ya usalama au ubora unaotakiwa au hata pengine
kitendo cha vyombo hivi kujali maslahi binafsi kuliko usalama wa
abiria.

Hili ni dhahiri pale ambao unakuta dalala limesheheni abaria bila hofu
kuwa wamebeba binadamu na siyo nguruwe. Kwa upande wa serikali na
mamlaka husika gharama itakuwa ni lawama watakazozibeba pale ambao
wataamua kusitisha matumizi ya dalala hizi maarufu kama vipanya ambazo
kwa mtizamo wangu ndilo chanzo kubwa la msongoma katika jiji la Dar es
salaam.

Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo ilikuwa kazi kubwa kupitisha mguu
katika maeneo ya kariakoo na mtaa wa kongo kwasababu ya msongamano
uliokuwa ukichangiwa na wafanyibiashara wadogowadogo maarufu kama
wamachinga.

Kama nilivyosema awali kwamba mabaliko yeyote au maendeleo yanahitaji
wakati mwingine kujitoa mhanga au sadaka, kazi ya kuwaondoa wamachinga
haikuwa kazi rahisi kwani iliambatana mapambano kati ya wamachinga na
wanamgambo, jambo ambalo lilileta mijadala na kelele toka watu
binafsi, taasisi, waandishi na wanaharakati, lakini basi baada ya
zoezi hilo kufanikiwa ni nani leo hii asiyefurahia matunda ya kazi
hiyo.

Leo hii unapopita mitaa hiyo angalau kuna amani na usalama wa
watu,tofauti na hali ilivyokuwa awali mara mtu kachomolewa pesa
mfukoni mara wamepokonywa mikufu, saa, pochi na hereni zao za dhahabu.
Nikirudi kwenye hili tatizo la msongamano wa magari katika jiji la Dar
es salaam, kwa mtizamo wangu zaidi ya kwamba ni kero lakini pia kuna
madhara kadha wa kadha ambayo huambatana na msongamano wa magari
katika jiji la Dar es salaam, mfano, licha ya kuwa tatizo hili
hulipunguzia heshima nchi pamoja viongozi wake lakini pia husababisha
kero za kisaikolojia kwa wafanyakazi na wanafunzi pindi wanapochelewa
kufikia makazini na mashuleni kwa wakati unaotakiwa kwa kuwa mara
kwa mara wanakumbana na adha za kugombania daladala ili waweze kuwahi
maofisini na mashuleni.

Siyo hivyo tu lakini pia wakati wa kurejea manyumbani baada ya kazi na
masomo kero hizo zinabakia pale pale.

Sasa basi, nini kifanyike na ni jukumu la nani kutokomeza kabisa hili
tatizo au kero ya msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam?
Nadhani jibu liko wazi tu kwani dhama hii ipo mikononi mwa serikali na
mamlaka husika. Najua kabisa zoezi lolote litakalolenga katika
kusimamisha matumizi ya vipanya na kutafuta njia mbadala litakuwa ni
mwiba kwa wahusika au wamiliki lakini kwa upande wa serikali endapo
itakuwa tayari kufanya mapinduzi na mabadiliko ya kweli basi serikali
haina budi kuubeba huu msalaba na sharti izingatie ule usemi kuwa
ukitaka kumuua nyani usimtizame usoni .

Kama njia mbadala ya kukabiliana na tatizo hili, ningependekeza
serikali kuingia mkataba kwa kuwaruhusu wawekezaji binafsi ambao
wamebobea na kuonesha ufanisi wa hali ya juu katika sekta ya usafiri.

Ni ukweli usiopingika kuwa kuna makampuni ya mabasi yaliyofanikiwa
kujijengea heshima kibiashara kwa huduma zao nzuri na za uhakika. Kama
serikali itawapa dhamana ya kutoa huduma za usafiri katika jiji la Dar
es salaam, naamini kabisa makampuni kama vile DAR EXPRESS,
KILIMANJARO, ABOOD NA SCANDANAVIA wanaweza sana tena kwa kiwango cha
juu kutupatia huduma ya usafiri kwa kupitia mabasi makubwa na siyo
daladala maarufu kama vipanya kama ilivyo sasa.

Hakika matumizi ya daladala maarufu kama vipanya si tu kuwa ni chanzo
cha kero mbali mbali kama vile foleni, ajali, unyanyasaji wa
wanafunzi, kutotii sheria za alama za barabarani lakini pia daladala
hizi hushusha kwa kiwango cha juu hadhi ya jiji letu la Dar. Sitapenda
kufanya marudio yasiyo na maana kwani ufumbuzi wa namna ya kukubiliana
na hili upo kwenye makala yangu ya awali.

Tatizo lingine linalochangia foleni ya magari ni kutokuwa na barabara
za uhakika, barabara ambazo zimejengwa kitaalamu kukidhi mahitaji na
wingi wa magari. Nini kifanyike hapa basi, je ni tatizo la ukosefu wa
wahandisi wabunifu wa mambo ya barabara, au pengine ni ukosefu wa
mwamko na ubunifu miongoni mwa viongozi wahusika katika masuala ya
mipango miji/ city planning, hapa nitawalenga moja kwa moja watu kama
vile meya wa jiji, pamoja na wahandisi wakuu wa jiji n.k au ni tatizo
la ukosefu wa fedha za ujenzi wa barabara hizi muhimu za katikati ya
jiji ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa kero za foleni.

Sasa basi endapo tatizo ni ukosefu wa ubunifu miongoni mwa wahandisi
wetu wa mambo ya barabara ningependa kuishauri serikali kama
ifuatavyo, hapa Finland kuna wataalamu na wabunifu wa hali hali ya juu
katika masuala ya ujenzi wa barabara. Kwa jinsi ninavyowafahamu Wafini
ni watu wanaopenda kusaidia sana katika mambo ya maendeleo, hivyo basi
endapo serikali inaweza kuwasilisha ombi lake hata kwa kupitia ubalozi
wa Finland Tanzania, ili wahandisi wachache waje kufanya survey ya
namna ya kujenga barabara za katikati ya jiji ambazo ndizo chimbuko
hasa la msongamano wa magari nina amini kabisa serikali ya Finland
inaweza kabisa hata kwa bure kuja kuwatuma hao wahandisi bila ya
serikali kuingia gharama yeyote.

Kama tatizo ni ukosefu wa pesa na mwako miongoni mwa viongozi wahusika
na mambo mipango miji/city planning basi hapo mimi sina la kusema
kwani jukumu hilo litabakia kuwa mikononi mwa serikali, lakini kwa
upande mwingine siamini kama tatizo ni fedha. Maana hata donor
communities wanamwaga mapesa kibao katika miradi ya maendeleo hivyo
basi ni suala la serikali kuweka kipaumbele kwenye kutokomeza hili
tatizo sugu ambalo limebakia kuwa wimbo wa kila siku miongoni mwa
watanzania.

Tatizo lingine linalochangia katika foleni ya magari katika jiji la
Dar. ni ukosefu wa maeneo ya kuegeshea magari/car parking sites. Hivyo
basi ili kubaliana na tatizo hili, serikali lazima ianzishe utaratibu
wa kueleweka wa kukujenga maeneo ya kuegesha magari kutegemeana na
upatikanaji wa nafasi kati maeneo kama vile, benki, ofisi, hoteli,
supermarkets, vyuo, shule n.k. . Kama tatizo ni ufinyu wa maeneo ya
kujenga maegesho ya magari, wahandisi wanaweza kufanya ubunifu kama
vile kujenga underground car parks ua hata katika mfumo wa ghorofa.

Mwisho napenda kusema serikali isisite katika kuwekeza kwenye haya
maoneo ya kuegeshea magari. Kwani maegesho haya yanaweza kuwa njia
mojawapo ya serikali kujiongezea mapato yake. Ila itakuwa ni jambo la
kusikitisha kama mapato yatokanayo ushuru wa uegeshaji magari
yataingia mifukoni mwa watu binafsi wenye hulka ya ufisadi.


Malkiory William Matiya,

7 comments:

emu-three said...

Kwa tunaosafiri na daladala tunaumia sana, hili swala ni tatizo sugu na naona wahusika hawajali, watajali vipi wakati wao wakipita wanapishwa sie wana-nchi tunasubirishwa pembeni!

Kaka Trio said...

Ndugu mto mada umetoa mawazo mazuri sana kuhusu namna ya kuondoa kera za foleni na fujo za magari, ni mwanzo mzuri.

Hata hivyo mie nadhani ili kuondoa kabisa tatizo la foleni Dar inabidi sio tu vipanya ndio vinagaliwe.

1)Inabidi uzingatie kuwa idadi ya watu wanaishi jijini Dar imwekuwa kubwa mno. Kwa hivyo itabidi wahusika waangalie namna ya kupunguza watu wanaolazimika kwenda mjini ili kupunguza foleni

2) Miundo mbinu inabidi iangaliwe upya. Aidha miundo mbinu mingine itabidi iongezwe na iliyopo sasa hivi itabidi iboreshwe ili iwe ya kisasa zaidi. njia nyingine rahisi ni jinsi ya matumizi ya barabara, yaani kuwe na barabara zitazotengwa kwa ajili ya shughuli maalum kwa wakati maalum. kwa mfano barabara ambayo ni ya dala dala tu hususani mida ile ya rush hours ya asubuhi wakatiwatu wanenda makazini na jioni wanapokuwa wanarejea majumbani.

3) Vyanzo vingine vya usafiri kama vile Treni au Rapid bus system pia vinahitajika kwa jiji kama la Dar

4) pia tatizo hili linaeza kupunguzwa kwa kuwa na barababara za kulipia. yaani ukiwa na haraka zako unaeza pita barabara hiyo lakini kila baada ya kilomita 20 lazima uache mshiko tuseme wa shilingi mia 2

5)inabidi ifike wakati sheria za barabarani ziheshimiwe. Kama alama inasema SIMAMA/STOP ni lazima dereva wa gari afanye hivyo, na anayevunja sheria basi inabidi atwangwe faini inayolipika lakini itakayomuuma, nimesema atwangwe faini sio "Rushwa"

6) kuwe na point system kwa madereva ukivunja sheria ya kuovateki pasiporuusiwa unapewa point 5 tuseme, ukipaki vibaya point 10 nk zikifikia tuseme point 1000 dereva anayng'anywe leseni kwa muda fulani na endapo atakamatwa anaenmdesha wakati alinyanganywa leseni kwa muda basi na aongezewe faini na hata kifungo jela.

6) pia inabidi tuwe na Traffic management systems and Centers. Hapa nina maanisha kuw ana kamera barabarani ambapo kitu chochote kikitokea basi wanaitwa polisi au wahusika wowote ili kufanya wasafiri wasipate usumbufu sana, pia nina maanisha real time mabango (billibodi) kuwaeleza waenda kwa magari kuna mashaibu yametokea mahala kwa ivo kuwa mwangalifu.

Endapo gari inaharibikia njiani kuwa na kampuni zimejiandikisha kuaondoa magari hayo haraka iwezekanavyo kwa malipo kutoka kwa mwenye gari

7) kuwepo na ajenda za makusudi kabisa za kuboresha huduma yaani mipango yote ya maendeleo lazima izingatie ni jinsi gani ya kusafirisha watu na bidhaa kwa ivo kuwe na policy cordination and combination zinazopelekea kuboresha au kurahisisha usafari. utakuta viwanja vinapimwa huko mpiji lakini wa mipango miji hawawasiliani na watu wizara ya miundo mbinu ili waone ni jinsi gani usafa=iri utafanyishwa. ni lazima cordination iwepo baina ya wizara na wizara husika au na washika dau wengine.

Nafahamu kuna mambo mengi ya kufanya mabayo sikuweza kuyataja kwa sababu moja au nyingine, wadau wangine wanaweza kuchangia.

Anonymous said...

blah! blah! blah!

Maisara Wastara said...

Mbona tunapiga kelele sana, lakini tunaishia kumbiwa eti ndio matunda ya maisha bora kw akila Mtanzania...!!!

Wizi mtupu!

Anonymous said...

Tatizo siyo foleni, tatizo ni kwamba magari yameletwa kabla nchi haijakuwa tayari kujenge barbara. Na kama hawapo tayari wanauwezo wa kukataza gari zote za binafsi ndogo zisije mjini, kama vile wakati tulivyokuwa tunaambiwa hakuna kuendesha gari Jumapili kwa sababu ya mafuta. Watu wote wengi wenye magari walikuwa wanpanda mabasi, sasa kama kuna mabasi yaendayo kwa haraka ina maana kutakuwa hakuna msongamano wa magari kuna mjini. Mapka hapo barbara zitakapopanuliwa. Tatizo la msongamano Dar ni kwamba magari mengi ni mabovu, unavuta hewa mbaya kwani magari yantowa moshi mkali mapka machozi yankutoka, na utakuwa unavuta hiyo hewa mapka ufike kazini. Ni hatari sana . NI sawa na miaka ya 80 ambapo shirika la reli lilikuwa linapeleka mabehewa mapya Kigoma na mpanda yakirudi ni yamekatwa sponge yote. Ina maan kwamba watu walikuwa hawapo tayari kukalia viti vyenye sponge walikuwa wamezoe mbao, kwani dahani ya kiti kwao sio kitu.

Anonymous said...

Wewe unchokoza moto waondowe vipanya, yani sahau, kwani hiyo ni mitaji ya wenyewe, kila polisi na kila trafiki polisi na wengineo wengi, yani hiyo ni pesa ya kunywa chai asubuhi, ya mchana inapatikana pengine, ya chakula jioni pengine na mengineyo. Hiyo kwani ndiyo kujenge taifa. Tumbo na mtoto wangu aende shule wengine ambao hanma nafasi subirini wakati wenu.

Anonymous said...

Kweli siku hizi mtu hutaki kwenda mjini shauri ya foleni! Tumekuwa kama Lagos Nigeria.