Wednesday, August 25, 2010

Onyo Kutoka Ubalozi wa Marekani Dar - Wizi

Wednesday, August 18, 2010, 3:20 AM

U.S. Embassy Dar es Salaam, Tanzania
Warden Message - Snatch and Grab Robberies
August 17, 2010

This Warden Message is being issued as a reminder of the continuing
problem of snatch and grab robberies in Dar es Salaam. Most recently,
occupants of a vehicle have grabbed bags, purses, and backpacks from
pedestrians and bicyclists traveling on the side of the road. Many of
these robberies occurred on the Msasani peninsula, specifically on Yacht
Club Road, Chole Road, and Haile Selassie Road. The latest incident
occurred the night of August 15 on Mahando Road near the Sea Cliff
Hotel. Several of these robberies occurred after the victim visited the
Barclay's bank in Slipway.

The U.S. Embassy reminds U.S. citizens to be aware of your surroundings
at all times and to be especially alert to individuals paying an undue
amount of attention to your activities. We also strongly advise against
carrying bags or purses while on foot or bicycle. If that is
unavoidable, be sure to carry the bag in front of you or on your side
furthest away from traffic. Bags that are nondescript, or even worn or
dirty in appearance, may be less appealing to criminals.
Facing oncoming traffic as you walk may allow you to anticipate a
robbery attempt and take evasive action. It is wise to avoid walking
after dark.

If you experience a snatch and grab robbery, release your belongings to
avoid physical injury. By hanging on, you risk being dragged down the
street (as has happened already), or getting caught under the rear wheel
of the car. To avoid losing your cell phone along with your bag or
purse, carry it in a pocket or somewhere else on your person.
The local equivalent to the "911" emergency line in Tanzania is: 111
U.S. citizens living or traveling in Tanzania are encouraged to register
with the U.S. Embassy through the State Department's travel registration
website, https://travelregistration.state.gov/ibrs/ui/, so that they can
obtain updated information on travel and security within Tanzania. U.S.
citizens without Internet access may register directly with the nearest
U.S. Embassy. By registering, U.S. citizens make it easier for the
Embassy to contact them in case of emergency. The Consular Section of
the U.S. Embassy in Tanzania can be contacted by telephone at [255] (22)
266-8001 x 4122 and by fax at [255] (22) 266-8238. You may also contact
the U.S. Embassy in Tanzania via email at drsacs@state.gov. For after
hours emergencies, U.S. citizens should call [255] (22) 266-8001.
U.S. citizens may also call the Office of Overseas Citizens Services in
the United States for the latest travel information. The Office of
Overseas Citizens Services can be reached from 8:00 a.m. until 8:00 p.m.
Eastern Daylight Time, Monday through Friday, by calling 1-888-407-4747
from within the U.S. and Canada, or by calling (202) 501-4444 from other
countries.

6 comments:

John Mwaipopo said...

na balozi zetu zingalikuwa zinatoa maonyo kama haya mambo yangekuwa poa sana. sidhani hata zinakumbusha watanzania kujithamini huko waliko na kukaa mbali na vishawishi vya uhalifu na madawa ya kulevya. sidhani pia kuwa balozi zetu zinashawishi watanzania kujiandikisha/kujitambulisha ubalozini, achilia mbali kutangaza nafasi za kazi za kimataifa kama vile zile za UN.

malkiory said...

Ni onyo nzuri lakini kwa upande mwingine lakini huenda ikaongezea hofu kwa watalii wenye nia ya kuja kutembelea Tanzania.

Hivyo kuna haja ya polisi wetu kufanya kazi ya ziada ili kuondokana na taswira hii kwa siku za usoni ili kujenga mazingira mazuri kwa watalii na wawekezaji wa kigeni.

Anonymous said...

john mwaipopo,sijui kama balozi za kitanzania zina faida yoyote kwa watu wake.ninachojua mimi wanajiona wanabahati kupata zile kazi,na biashara imeisha.

kuna kipindi nilikuwa maputo,nikapatwa na matatizo na polisi wa mozambique.nilikuwa na wife wangu tumefikia hoteli iliyo karibu na ufukwe kabisa.siku hiyo baada ya dinner nikamchukua wife tukawa tunapunga upepo ufukweni.haikufika hata robo saa ilifika gari lenye kundi la mapolisi wenye silaha.walichofanya ni kiniamuru kusimama wima na wakaanza kunisachi kuanzia juu mpaka kwenye viatu.sikufanya ubishi kwasababu hatukuelewana lugha vizuri.bahati nzuri,kwa kipindi kile pesa na kadi zangu zote zilikuwa kwenye mkoba wa wife wangu.walipoona hawakuambulia kitu,mmoja wao akashika mkoba wa mke wangu,hapo sikukubali.nikasema huyu ni mwanamke,huruhusiwi kumpapasa .kulikuwa na wageni na walinzi wanaona action yote,lakini walikuwa kwa mbali kidogo,nikadai kabla ya kumpekua mke wangu,tusogee kwao kwasababu kulikuwa na mwanga zaidi.kwakuwa hawakuwa na nia njema,nia yao ni kutuibia kwasababu sisi ni wageni,wakagoma kusogea kwenye mwanga na mmoja wao alinipiga kirungu kwenye goti langu la mguu wa kulia.nilisikia maumivu sana,nilipiga makelele ya kuomba msaada.walivyoona watu wanazidi kuvutiwa na nini kinachoendelea pale.wakapanda gari yao wakakimbia.
bahati nzuri,mtu mmoja alichukua namba ya gari yao.usiku nikapata huduma pale hotelini nikalala.hasubuhi nikaenda kituo kikuu cha polisi,cha ajabu wakaniambia hawana gari yenye namba zile.ndo nilipoamua kwenda ofisi za ubalozi wa tanzania pale maputo,kuelezea yaliyonifika,labda wanaweza kunisaidia kwa namna yoyote.majibu nilyopata nilichoka,eti ubalozi auhusiki na maswala kama hayo.nikakata tamaa,nikaendelea na shughuli zilizonipeleka.watanzania wanaoishi pale wakaniambie,eti wamesahau kama kuna ubalozi wao pale.ndo balozi zetu hizo.

Anonymous said...

ngoja niwaeleweshe wadau.

kazi ya balozi sio kuhukumu au kutoa warant of arrest kwa watu. kazi yao ni kulalamika kwa wizara ya mambo ya nje ya nchi waliopo pale itakapoonekana kuna raia wake hakutendewa haki. lkn suala la jee haki atapewa au la ni suala la serikali ya nchi ile sio ubalozi.

wengi wanadhani wakifika ubalozini ndio mambo yao yatanyooka na kuwa shida zao zimeisha. hiyo sio sahihi. ubalozi hauna power ya kumuarrest au kumpa surmon mtu yeyote kwa kuwa mtz amamlalamikia. pia uballzi hauwezi kuwasiliana na taasisi yeyote ya nchi mwenyeji isipokuwa kupitia foreign affairs ya nchi hiyo.

hivyo watz waache kulalama. pia wajifunze ustaarabu wa kufuata sheria za nchi za watu. sio wanavunjasheria kisha wategemee ubalozi uwatetee. hiyo kitu hakuna.

mdau wa kidplomasia.

Anonymous said...

Nafikiri tatizo sio kuwa watu hatuelewi mipaka iliyonayo ofisi za balozi zetu. Tatizo kubwa ni ATTITUDE za watumishi waliopo kwenye ofisi nyingi za balozi zetu ndio zinazolalamikiwa hapa.

Mfano mdogo ametoa huyo mdau hapo juu, nafikiri angepewa jibu kuwa ofisi yetu ya Ubalozi itapeleka malalamiko haya kunakohusika, na tunakupa pole kwa yaliyokukuta, siku nyingine likishaingia giza usiende beach! (Nafikiri Ubalozi wa Marekani ungemfanyia hivi mtu wao) Huyo mdau hapo juu angejisikia faraja kuwa japo nipo ugenini lakini ninapo kwa kukimbilia. Lakini kwa maofisa wetu walioko ubalozini wanajiona semi gods, wao hapo walipo wamefika na hawana haja ya kuhudumia watu wengine.

Wakati mwingine hata maofisini hawakai sijui wnakwenda kuzururia wapi maana unaweza kupiga simu wee hata hazipokelewi, sijui wanakwenda shopping, sijui hata wanafanyaje kazi. Kama ikitokea ermegency na watu wanatakiwa wawe evacuated sijui kama hata na hiyo evacuation plan, kila Mtanzania atajijua na lwake. Ingawa sio balozi zote zenye ugonjwa huu lakini majority ni kama wako holiday vile, leave ya Pinochio kutoka Januari mpaka Disemba.

Mwisho majibu yao yasioridhisha kwa wateja, hawana kabisa kauli nzuri hata ukiongea nao kwenye simu utakuta Afisa Ubalozi anafoka, unamfokea nani wote watu wazima? Na unatakiwa utoe huduma badala ya kuwa kama mwalimu wa shule ya msingi anayefokea wanafunzi watukutu? Hivi hicho chuo cha diplomasia Kurasini kinafundisha nini? Hakuna somo la Customer care? Hasa ukizingatia stress za ughaibuni mtu ana stress kibao kisha Afisa wa ubalozi naye anaongeza za kwake, ndio maana watu hawaoni umuhimu wa hizi ofisi ya ubalozi zilizoko nje wanaona kama ni kupoteza pesa za serikali tu na kupeana ulaji!

Jirekebisheni ili mrudishe hadhi ya ofisi za ubalozi sio kufoka foka tu. Jifunzeni huko mliko muone wenzenu wanavyo watreat watu/wateja wao maana tofauti ni kubwa mno jamani.

Anonymous said...

afisa diplomasia yamemgusa ndio maana anatoa maelezo hewa ubalozi wa Marekani umewapa tahadhari raia wake kwamba wawe macho na maeneo fulani kama ambavyo balozi zetu zinatakiwa kutoa muongozo kwa wananchi wake. Utaratibu huo huo wanaotoa ubalozi wa Marekani ndio huo huo balozi nyingine wanapaswa kufanya. Wametoa muongozo mambo yakiwa makubwa wanawasiliana na wizara husika sio unatuambia heshimuni sheria za nchi wakati wewe sheria za nchi yako huzijui vizuri ni bora wabaki balozi na katibu muhtasi wake wengine wote mrudi bongo maana hakuna cha maana mnacho kifanya. Juzi Carter kaenda kumtoa mtu North Korea sijawahi kusikia kiongozi yeyote wa Afrika akaenda kumtetea mfungwa wake Shame on you badilikeni sio kujidai Mungu watu limewachoma ndio maana mna hasira