Sunday, August 22, 2010

Rais Kikwete Alivyoanguka Jukwaani Jangwani

Masononeko na vilio mara baada ya Rais Kikwete kuanguka (photo: PwaniRaha.com)

Mnaweza kuona picha na video JAMII FORUMS:

http://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania-2010/70521-kikwete-aanguka-ghafla-jangwani-22.html

Wadau, nimesikitika sana kusikia habari kuwa Rais wetu mpendwa kaanguka Jukwaani. Kama ni shauri ya swaumu au tatizo lingine tumwombee.

Nimetazama video ya tukio na niliogopa. Unamsikia rais akihutubia kwa nguvu, ghafla anasema, "Aisei" halafu anaongea maneno ambayo hayaeleweki halafu mwisho anaanguka. Unaona maelfu wa watu wanakuwa na wasiwasi, unasikia akina mama wakipiga mayowe! Mtangazaji anasema "CCM JUU" Hakuna anayeitika watu waote hofu kwa rais. Nikajiuliza aliposema, "Aisei" alisikia maumivu fulani?

Kwa kweli viongozi wanaanguka mara kwa mara. Ratiba zao nzito wakati mwingine wanakosa muda wa kumpumzika. Rais Bush wa kwanza alianguka Japan tena alianguka kwenye bega la waziri mkuu wa Japan. Janet Reno naye alianguka hadi sakafuni, pwaaa kisa uchovu. Mgombea Rais, Bob Dole naye aliaanguka. Tanzania, wameanguka wengi shauri ya malaria, ulevi na matatizo mengine ya afya. Miaka ya 80 Kizito fulani alikuwa anahutubia huko kaanza kuharisha shauri ya kipundupindu. Acha tu. Uongozi si mchezo!

Hapa USA kiongozi akianguka wanaonyesha kideo mara mia na zaidi, na waletwa wataalamu wa afya kuchunguza kutoka kwenye kideo nini kilimsbabisha aanguke. Hivyo tusione jambo la ajabu. Rais ni binadamu kama sisi, siyo Superman.

Pole sana Rais wetu mpendwa, Mheshimiwa Jakaya Kikwete. Tunakuombea uzima.

5 comments:

emu-three said...

Raisi ni binadamu kama binadamu wengine, kasoro tu kule `kutukuzwa'. Kwahiyo kuanguka kwake kungeweza kutokea kwa mutu yoyote yule. Tusianze kutafutana `uchawi' Lakini sababu za kitaalamu walitaja, kwahiyo hakuna jipya.
Tunampa pole sana, mungu ampe afya njema aendelee na kunadi sera za chama chake

Anonymous said...

Nataka khanga na kitenge chenye picha ya Kikwete. Na kweli anaposema aisei ndo matatizo yanaanza. Nini kilimpata. Kalogwa.

Anonymous said...

Kikwete augua, wananchi walia
GHAFLA uwanja unazizima, kila aliye katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam anashindwa kuamini kinachotokea, hotuba ya mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia CCM, Rais Jakaya Kikwete inakatika.

Hali hiyo inajitokeza baada ya kuanza kuzungumzia suala la Utawala Bora katika hotuba yake ya uzinduzi wa kampeni za Chama hicho jana.

Kutokana na mshituko huo, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba anasimama na kuchukua kipaza sauti na kuwatuliza wanachama, wafuasi na wapenzi wa CCM waliofurika uwanjani hapo kushuhudia uzinduzi huo.

Baada ya muda inabainika kuwa Rais Kikwete amepata matatizo, ameishiwa nguvu na kusaidiwa na wasaidizi wake na kupelekwa kwenye zahanati ya muda nyuma ya jukwaa.

Walinzi walimbeba na kumpeleka kwenye zahanati ya muda iliyokuwa katika uwanja huo, lakini walipoikaribia, Rais alisimama na kuingia kwenye zahanati hiyo akitembea mwenyewe.

Baada ya dakika takriban 15 hivi alirejea kuendelea na hotuba huku akishangiliwa na umati huo. “Jamani nimefungulia,” alisema Rais huku akishangiliwa, akimaanisha kukatiza swaumu.

Hata hivyo, hakuweza kuimaliza hotuba hiyo iliyoonekana kuwa ndefu, pale aliposema tu kwamba Serikali yake iliweza kupandisha mshahara wa wafanyakazi ingawa kwa tofauti kidogo na kiwango kilichokuwa kikitakiwa na Tucta.

Lakini wakati anaanza kuzungumzia yaliyofanywa na Serikali yake katika sekta ya miundombinu, aliomba Watanzania waichague CCM na kumaliza hotuba hiyo.

Hali hiyo ilisababisha mshtuko na hofu ambapo baadhi ya wana-CCM walizirai na baadhi kuonekana wakilia kwa uchungu.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati, waliwahimiza waliohudhuria kutulia.

Wakati huo huo, katika hali isiyotarajiwa, mkewe Mama Salma naye alijisikia vibaya uwanjani hapo na kusaidiwa na kupelekwa kwenye zahanati hiyo, kupewa huduma ya kwanza.

Mama Salma wakati akielekea kwenye zahanati hiyo kumjulia mumewe hali, alipokaribia alidondoka na kudakwa na walinzi wake na wakati anaingizwa kwenye zahanati hiyo, alipishana na mumewe mlangoni akitoka.

Hili ni tukio la tatu kwa Rais Kikwete kudondoka mbele ya hadhara wakati akihutubia wananchi.

Oktoba 2005 alipatwa na matatizo kama hayo wakati akifunga kampeni ya kuwania urais kupitia CCM.

Katika tukio hilo, Rais Kikwete alilazimika kukatisha hotuba yake na kuondolewa uwanjani hapo.

Baadaye akazungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake akisema hali hiyo ilisababishwa na uchovu wa kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya nchi akifanya kampeni huku pia akiwa amefunga.

Oktoba mwaka jana, alijisikia pia vibaya na kuishiwa nguvu ghafla wakati akihutubia mamia ya watu katika maadhimisho ya miaka 100 ya Kanisa la African Inland (AIC) kwenye uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, hali iliyosababishwa na uchovu wa safari ndefu.

Madaktari wake walishasema hali yake kiafya ni nzuri na matatizo yaliyomkuta ni mabadiliko ya kawaida kiafya. Leo atakuwa Mwanza kuendelea na kampeni.

habari leo

Anonymous said...

I am concerned, was it real or was it a fake to lure in the multitude's sympathy just like how Hillary Clinton did on her campaigns by crying publicly?
But lets suppose he was not faking! Then What? Its horrifying to learn that CCM is entrusting the leadership of this country on a person who is not fit and healthy! Is it a ploy or a mistake? CCM needs to tell people what is this JK collapsing every now and then! We citizen of this country demand some answers, and damn good ones!
Mr JK, it is not a must that you go on aspiring the presidential position, if you are un-fit retire gracefully and this nation will remember you with pride, otherwise if you are unfit and should anything happen (God forbid) this nation will never forgive you by tricking it into standing behind you!

Anonymous said...

aaaa wameondoa clip lakini unaweza kuiona kweye you tube