Wednesday, June 08, 2011

Mama Bishanga Afiwa na Baba Yake Mzazi

MAMA BISHANGA AFIWA NA BABA YAKE

Leo tunasikitika kuwaarifu kuwa baba mzazi wa msanii maarufu katika fani ya filamu Mrs Christina Innocent Marolen, Mama Bishanga, Mzee Isaya Innocent Hatia (mtoto wa Mwenye Hatia Chifu wa Wamakua, Ashinnahatia) amefariki dunia huko Ndanda hospital masasi jana.

Mzee Hatia alikuwa na miaka themanini na mbili, ameacha mke Mwalimu Agnes Hatia, watoto saba ambao ni Mama Bishanga, na wadogo zake Geofrey anayeishi Namibia, Mwalimu Marck wa Azania Sekondari, Bernadeta, Isaya anayeishi Finland, Constancia na Oscar. Pia ameacha wajukuu na vitukuu.

Mzee Hatia atakumbukwa kwa kuwa mmoja wa wafanyakazi bora na wa muda mrefu wa kampuni ya Posta na simu tangu enzi za East Community huko Nairobi na Mombasa, na hapa nchini Dae-E.s-salaam, Dodoma, Tabora nk

Mazishi yatafanyika Ndanda Masasi ijumaa.

No comments: