Friday, June 24, 2011

Posho Za WabungeNimeona hii FACEBOOK:

BASHE: Ombi Langu kwa Wabunge wa Chama Changukuhusu POSHO

Ombi Langu kwa wabunge wa chama changu, si kila jambo kulipinga swala la Posho (sitting allowance) hakuna sababu ya kulivalia njuga na kulazimisha kulipata,wabunge wanapata Mshahara,posho ya kuwa nje ya kituo ,posho ya ubunge FEDHA HIZI zinawatosha ukiangalia hotuba ya zito tunasema pato la mtanzania ni 770,000 lakini kuna asilimia 20% ambao wanashikilia 42% ya pato la taifa (32trillion) kati ya hizo wakati 20% ya masikini wa chini kabisa wanashikilia only 7% ya pato la Taifa.

Kwa mtazamo wangu ikiwa sitting allowance ambayo kwa ujumla wake ikipunguzwa tuta save 900bn fedha hizi zikiamuliwa kupelekwa katika sekta ya ELIMU kuondoa kero ya waalimu kuishi madarasani kwa kuwajengea nyumba, kwa majirani,ama kuondoa kero ya Mabweni ktk shule za kata,ama kuondoa kero ya MAABARA katika shule za kata,ama kupelekwa katika sekta ya Afya , tutakuwa kama Taifa tutamaliza tatizo kubwa sana tutaipunguzia serekali na walipa kodi mzigo wa fedha ambazo haziendi katika shughuli za maendeleo,Niwaombe wasiitazame hoja imetoka kwa nani wa chama gani waipokee na kuiunga mkono Mtakuwa mmeitendea HAKI nchi yetu,na watanzania ambao mustakabali wa maisha yao katika miaka mitano ijayo upo mikononi mwa serekali ya CCM (cham chetu) hata kama kama mnaipata kwa mujibu wa sheria na kanuni fanyeni cost benefit analysis kwa kuliangalia taifa na si nyinyi peke yenu.kama taifa tutfaidika zaidi fedh hizi msipopokea na kuamua kama bunge zipelekwe katika shughuli za maendeleo.

Wapo wabunge ambao wana jenga Hoja ya kwamba Posho hizo zinawasaidia ktk shughuli za Majimbo, inawezekana inaukweli,lakini kama MFUKO WA MAENDELEO WA JIMBO ,POSHO YA UBUNGE 5M,ALLOWANCE YA KUKAA NJE YA JIMBO 80,000,MSHAHARA 2M vyote hivi vimeshindwa kukusaidia kuhudumia Jimbo basi hata hiyo Posho haita weza,naamini mnatuongoza tutawaona si wabinafsi mkiunga mkono hili kwani mnachpata kwa maisha yenu kinawatosha.

Itendeeni haki Nchii hii katika kipindi hiki ambachi ambacho maisha yanazidi kuwa magumu shilingi inashuka, kuna vijana wenzetu million 11 wanahitaji msaada waliopo mashuleni na vyuoni wanahitaji msaada wenu mtakuwa mmetenda haki sana kwa kusamehe hicho kidogo,nimuombe Mbunge wangu aunge Mkono kusamehe hiyo Posho 70,000 ni Tofali 350 za kuchoma kwa bei ya kule kwetu ,mara siku za vikao ,ni fedha nyingi tutapata mabweni, maabara,ama fedha hiyo utakuwa umesaidia vijana wengi kulipiwa ada ktk shule za Kata. Kwahiyo ni vizuri likaungwa mkono jambo hili ili kuisaida Nchi

SOURCE: Bashe's facebook note

2 comments:

Anonymous said...

Kweli hizo pesa zingeweza kuboresha elimu, hospitali, bara bara. Lakini TZ wamezoea mno mapsoho.

emu-three said...

Ujumbe umefika, na hizi posho, nk ndizo zinzwafanya watu wakimbilie kwenye siasa...wakati mwingine unashangaa mtu aatoka kwenye `profesheni yake' anakimbilia huko...kwenye poshoo nono...!