Friday, June 17, 2011

New England Umoja 10th Anniversary CelebrationN.E.U 10TH YEAR ANNIVERSARY

Ndugu wapendwa,

Natumaini wote mu wazima wa hali, na shughuli mnaziendesha ipasavyo.

Napenda kuwafahamisha rasmi kwa niaba ya wanakamati wenzangu kwamba Jumuia ya watanzania waishio New England (MA,NH,CT,RI,ME,VT na NJ), ikiwa chini ya mwamvuli wa NEW ENGLAND UMOJA FOUNDATION, INC, inawakaribisha rasmi kwenye ile shughuli ya kuvunja na shoka inayofanyika kila mwaka pale camp Keewanee, Greenfield, Ma.

Siku ya ijumaa na Jumamosi usiku kutakuwa na viburudisho rasmi kutoka kwa Ma-D.j's wetu ikiwa ni pamoja ni DJ Richimaka ambae atakuwa na vibao vipya kabisa kutoka BONGOLAND!!.

Siku ya Jumapili July 03/2011 ndio Shughuli yenyewe. N.E.Umoja inatimiza miaka 10 tangu zilipoanza sherehe hizi. Njoo wewe, na wale wote uwapendao ufurahi na watanzania wenzako kutoka sehemu mbalimbali, kuadhimisha siku hii muhimu tukikumbuka na kuuenzi utamaduni, desturi na mila za Ki-Tanzania!.

Shughuli hii itafanyika palepale Camp kee-wanee (www.campkeewanee.org), Greenfield MA. 01301.(9AM-9PM).

**ILANI: POMBE NI MARUFKU KATIKA CAMP SITE...PERIOD!!!!**(THE CAMP IS ALCOHOL FREE, AND WE MUST RESPECT THAT RULE PLEASE)

Shughuli hii ni ya aina yake mwaka huu, itatanguliwa na Muziki wa hali ya juu kutoka kwa D.J Eddie, DJ Luke bila kusahau dj waalikwa Dj Paul Masoud Dj Samora DJ Richmaka siku ya Ijumaa usiku 54 state st Lynn MA 8PM To 1 na pia pambano ya mpira wa miguu kati ya N.E Umoja Foundation-Combine itakapopambana na timu ngumu ya Jirani zetu kutoka Kenya, siku ya Jumamosi saa kumi jioni.

Siku ya siku, hiyo Jumapili, "Watu wazima", kutoka maeneo yote watajimwaga uwanjani kutoa jasho, na kujipima nguvu. Vile vile mwaka huu, kutakuwa na mbio za watoto wa kiume na wa kike, vijana, kina mama na pia kina baba. Akina Mama nao watakuwa na mbio za chupa, volleyball, na kutakuwa nn Basketball ya vijana.

Shamrashamra zitapambwa pia na mashindano ya kuogelea, na ndugu Baraka Mchome atatuimbia Mashairi na kutakuwa na ngonjera vilevile. Maonyesho ya mitindo ya nguo na kanga "Fashion show" ya aina yake yataletwa kwenu rasmi na Mama wa Ki-Tanzania, si mwingine bali ni dada yetu Mama maarufu wa mitindo Tanzania na East Africa, ASYA IDAROUS KHAMSIN. Kutakuwa pia na "Surprise Guest Singers/entertainers" ambao wamekubali kuja kujumuika nasi mwaka huu. Njoo ushuhudie waimbaji wenye vipaji wakiwemo vijana wetu wenyewe, pia "Old School" itawakilishwa vilivyo. Kutakuwa na ngoma za utamaduni, "Raffles" na zawadi kem kem!!
Bila Kusahau kutakuwa na Mahanjumati na Maakulati ya hali ya juu,Na wale wanaokula Halali wasiwe na wasiwasi kuna ngo'mbe wa miguu mine ataangushwa na kama mnavyoelewa kuwa” Mkono mmoja hauchinji Ngombe” kwa hiyo njooni tumshughulikie Ngombe aliyejaa viungo vyote kutoka nyumbani mafili mdawati, mafili mdawiya, mabili kompoza vyote vimo kwenye nyama choma ya kumwaga siku hiyo ya Jumapili!!!!!!!.

Na wale walaji wa samaki wasiwe na wasiwasi wapo wa kumwaga Red sniper, king fish, Tuna, Dorado swordfish, kalamari ,ngandu wote wamo kwa wale wanaopenda kulakula.

Kumbuka, ni jukumu lako na langu kuifanikisha shughuli hii, kwani New England Umoja ni wewe na mimi. Ninaomba mfikishe salam hizi kwa ndugu, jamaa na marafiki zako wote, popote waliko hapa Marekani. Kama ilivyo miaka yote, itakuwa ni siku ya furaha kwa watanzania wote, siku ya kujivunia na kuuenzi utamadini wetu,Umoja wetu, desturi na mila za ki-Tanzania na upendo baina yetu na marafiki zetu. Njoo wewe, na na wale wote uwapendao upumzike mwa'kwetu!!.kama mnavyojuwa penye wengi pana mengi.

Bwana "Vijimambo" nae atakuwepo kukusanya habari za matukio mbalimbali kwenye shughuli hiyo, pia kwa mara ya kwanza kabisa, shughuli ya mwaka huu itapeperushwa hewani "LIVE" kupitia kwenye mtandao!.

YOU REALLY DON'T WANT TO MISS THIS YEAR'S EVENT !

Directions: from New York, Jersey City, Connecticut, and Springfield area:

I-91 North, to exit 26-bear and turn Right off the ramp) towards Rt.2A East-Greenfield Center. Proceed, passing Applebee's & Mobil gas station. Go thru 2 sets of Lights (you'll pass 2 gas stations , Dunki'n Donuts &Enterprise). Continue until you see Dillon Chevrolet Dealership. Turn Left on Conway St.. *DO NOT GO TO DOWNTOWN GREENFIELD!*. Drive for exactly 4.3 miles from Conway St. to the sign/entrance at Camp Keewanee (It is a residential area, which will turn into a farm area). Conway st. will turn onto Leyden Rd. Then you'll make a very sharp LEFT turn (almost like a U-Turn) @ the CAMP KEE-WANEE SIGN. Proceed slowly thru the gate, since the road is unpaved one, all the way to the Camp!

From Boston, New Hampshire, Rhode Island, Worcester, Fitchburg, Leominster, and Gadner.....

Take Rt.2 west to I-91 SOUTH , (DO NOT GO TO 91NORTH, You'll find yourself in Vermont!!)

then take Exit 26 (to Rt. 2 West). It is the 1st exit on your Right). Go around the Rotary, and follow the above directions. Gas stations all around Greenfield on either side of the Rotary

* If lost/need assistace, please call:

Siraji 978-413-1164, Richard 413-262-0400, Stephen 413-658-5253, Salum 617-308-2971,

Sangiwa E. 978-846-9898, Baraka 901-297-6464, Jamal 978-846-6218, Eddy 781-608-0665,

Maria 413-364-8146,Kawala 413-330-1609, Isaac 413-219-1153 & Marwa 978-799-5790.

Hotels/Motes in Greenfield:

Hampton Inn & Suites Greenfield

184 Shelburne Rd, Greenfield, MA 01301 (413) 773-0057 Website Directions

Quality Inn 125 Mohawk Trl, Greenfield, MA·

Days Inn Greenfield 21 Colrain Rd, Greenfield, MA·

Hotels/Motels in Springfield MA (about 50 minutes away)

Springfield Marriott 2 Boland Way · Springfield, Massachusetts 01115 USA

Holiday Inn Serving the Springfield Area. (877) 654-0232
*Gas Stations Rt. 5 &10 Both directions, also on Main St. and at the Rotary near McDonald's in Greenfield.

http://www.newenglandumoja.net/ for more details on Friday and Saturday for "Pre-Sunday's Event festivities". Please forward these directions to as many people as you can, or visit our website.

Come and celebrate its FREE!!!!..................KARIBUNI SANA WOTE!!!!!!!!!!!

No comments: