Wednesday, December 21, 2011

Mafuriko Dar - Hali Ni Mbaya!

Wadau, kutokana na mvua mwingi kumetokea mafuriko ya ajabu mjini Dar es Salaam! Nasikia kuna daraja moja tu, kwenda maeneo ya Mbezi Beach!  Katika mji wa Dar es Salaam hasa Idara ya Mipango Miji naona wamesahau mambo ya STORM DRAINAGE!!!  Hata hivyo kutokana na Ujenzi holela mambo yangekuwa bure!

Nasikia kuna vifo!  Je, RED CROSS/RED CRESCENT wataingia kusaidia waathirika?

Msamaria akimvusha kikongwe mkazi wa Jangwani baada ya makazi yake kuharibiwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Desemba 20. (Picha na Fadhili Akida).

Jangwani nako  Balaa!

Old Bagamoyo Road baada ya Mafuriko. (Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)

BALAA TENKI BOVU


Baada ya daraja kati ya Lugalo na Tenki Bovu (Mbezi Beach) kumegeka...Inabidi watu watembee kwa miguu kwenda upande wa pili wa daraja iliwapate usafiri  kumaliza safari zao.


*****************************
MJI wa Dar es Salaam Umekuwa Ziwa Dar es Salaam

(Picha Zifuatazo Kwa Hisani ya Tutoke Media Blog)1 comment:

ELIA GODWIN MUNUO said...

it is very sorry for those who have lost their homes but may be next time u will realise that you have to leave those places