Sunday, February 17, 2013

Padri Auwawa Zanzibar Akielekea Kanisani Leo!

TAARIFA  KUTOKA JAMII FORUM:

Default Update: Watatu wahojiwa Zanzibar kuhusiana na mauaji ya Padre na Taarifa ya Polisi


17/02/201




Padre Evaristus Mushi


UPDATE/TARIFA MPYA (saa nane u nusu mchana) Taarifa ya Polisi:

Watu watatu wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ya Padre Mushi. Tafadhali bofya vipande vya picha zilizopachikwa hapo ili kuvikuza na kusoma taarifa ya Polisi inayoonekana hapo (shukurani kwa Francis Dande).









UPDATE/TAARIFA MPYA (saa saba mchana) Taarifa ya habari Radio One Stereo:

Taarifa ya habari ya Radio One Stereo iliyosomwa saa 7 mchana imeripoti kuwa Padre Mushi aliuawa na watu walipolisimamisha gari la Padre huyo alipokuwa akielekea katika kanisa la Mtakatifu Theresia lililoko eneo la Mtoni, na alipopunguza mwendo ili awasikilize, ndipo alipopigwa risasi kichwani na kusababisha gari alilokuwamo kukosa uelekeo na kuigonga nyumba iliyokuwa jirani. Watu walioshuhudia tukio hilo walimchukua Padre Mushi ili kumwahisha hospitalini katika jitihada za kuokoa uhai wake, lakini alifariki dunia. Waliomwua Padre Mushi bado hawajakamatwa.
-----------------------


Akina mama wakilia kwa uchungu kuomboleza kifo cha ghafla cha kupigwa risasi Padre Evaristus Mushi kilichotokea leo asubuhi muda mfupi kabla ya kuanza Misa ya Jumapili kwenye kanisa la Kigango cha Mtoni, Zanzibar. (Picha na Martin Kabemba via Lukwangule blog)
Taarifa kutoka Zanzibar zikiripotiwa na mwanahabari Donisia Thomas wakati kipindi cha Patapata cha WAPO radio FM kinaendelea, zinasema kuwa Padre Evaristus Mushi wa Kanisa la Parokia ya Minara Miwili huko Zanzibar amepigwa risasi majira ya saa moja asubuhi -na watu wasiofahamika- na kufariki dunia.

Taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa na madaktari kutoka hospitalini alikopelekewa katika harakati za kuuokoa uhai wake.


Padre Mushi aliuawa akiwa anashuka kwenye gari lake tayari kuingia Kanisani kwa ajili ya kuendesha misa ya kawaida ya Jumapili katika kanida la Mtoni, mjini St. Joseph. Inaelezwa kuwa gari lisilofahamika lilifika na kufyatua risasi zilizomlenga Padre Mushi sehemu ya kichwani na hivyo kumsababisha majeraha yaliyokuwa yakivuja damu nyingi.


Mwanahabari anasema tukio hilo limezua taharuki kubwa miongoni mwa waumini ambao wamekataa kuahirisha ibada iliyokuwa iendeshwe na Padre huyo na kusema ikiwa kusudio ni kuwaangamiza Wakristo wote, basi na waangamizi wafike Kanisani wawaangamize wakiwa pamoja.


Jeshi la Polisi limeshafika katika eneo la tukio na kuanza uchunguzi.


Wakizungumza kuhusu hilo, raia wamesema hawana imani na Polisi wala Madaktari na hawatarajii jipya zaidi ya ripoti kuwa suala hili ni la uhalifu kwa kuwa tukio kama hili liliwahi kutokea mwishoni mwa mwaka jana kwa Padre Ambrose kupigwa risasi na taarifa zilisema lilikuwa ni tukio la kihalifu na kwamba risasi hazikutumika jambo ambalo halikuwa kweli kwani Padre Ambrose alikutikana na risasi alipohamishiwa katika hospitali ya Taifa, Muhimbili.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali fuatilia vyombo mbalimbali vya habari.


Father Mushi Alipokuta mauti yake


5 comments:

Anonymous said...

Marehemu padre Evarist Gabreli Mbilinga Mushi atazikwa huko zanzibar jumatano hii, hii ni kwa mujibu wa ndugu na uongozi wa kanisa katoliki zanzibar.


Padre mushi ni mzaliwa wa uru mawela,kijiji cha kimnaganuni, moshi vijijini,alipata masomo yake katika shule ya msingi kimanganuni, na baadaye akajiunga na seminari ya uru , alipata upadirisho wake huko zanzibar.

Padre mushi atakumbukwa kote alikofanya kazi kwa utumishi kwa mungu uliotukuka. Leo asubuhi kabla ya kwenda kanisani aliongea na padre mwenzake aliyeko jamaica, akimhakikishia kuwa alikuwa amejiandaa vema kwa mahubiri yake kanisani, ilikuwa saa 12 na nusu. Mahubiri ambayo watesi wake hawakumpa muda ya kuyatoa, bali wakatoa uhai wake !

C Misango said...

Jana Jumamosi, niliandika makala ya NANI ANAJALI, nikaonesha jinsi watawala walivyoamua kupuuza kila dalili za machafuko ya udini zilivyoanza kujionesha mapema sana.
Kuna watu walipongeza na baadhi hususan waislamu walinishambuliana kwa matusi na kila aina ya kashifa. Lakini hata saa 24 hazijaisha, yametokea haya!
Chongolo, na wengine tujiulize, nani aliyekuwa akijinadi katika kampeni ama wagombea wa chama kipi walionekana bayana kufanya kampeni kwa mgongo wa dini? Je, watu wa aina hii, walitegemea nini?
Je, ripoti za uchunguzi wa kupigwa risasi kwa padri miezi iliyopita na kumwagiwa tindikari kwa Sheikh soraga ziko wapi? Je, kwa uzembe huu nani ataamini tena uchunguzi wa jeshi la polisi?
Kwa nini isiundwe timu ya uchunguzi kwa kushirikisha wataalamu huru na ripoti yao itangazwe waziwazi na wahusika bila kujali dhamana zao iwe za dini ama serikali au chama wachukuliwe hatua kali mara moja?
Kama watu wanauawa, mtu anasambaza kanda ya kuhamasisha watu kuua wenzao na bado yuko huru anakula, anatamba na polisi, usalama wa taifa, watawala wapo na hakuna lolote linalofanyika, wananchi watakosea wakisema kuna mkono wa serikali? Kwa sababu wakati mwingine, watu wanapewa cha kusema kwa sababu watawala wenye wajibu wa kulinda sheria, haki, uhuru na maisha yao wanaonekana kutojali!

Anonymous said...

Wakati maduka ya wamasai na wabara yakichomwa moto Znz ilikuwa ni kwasababu gani?
Mbona wepesi sana wa kusahau? Kulikuwa na udini hapo? Meseji inatumwa sasa ni baada ya ile iliyotumwa kutoiona kama ni meseji ya maana ya kuifanyia kazi.

Walianza na makanisa, then biashara za watu wara bara. Wakichoma makanisa ilikuwa ni indicator ya 'hatutaki WATANGANYIKA' wakijisikia kwamba wao ni safi na wanataka nchi yao..na kwamba bara ni wakristo, kwamba waislam wa bara si chochote.

Zilikuwa chokochoko za wazi....hatukuzisemea, sasa anapouwawa padri ndo maneno na ujuzi unaonekana.

1) Sheikh Ilunga akamatwe kwa uchochezi, ashitakiwe kwa mauaji yanayotokana na uchochezi wake
2) Waliochoma maduka na biashara za vijana wa tanganyika tuanmbiwe kama wamekamatwa na wamechukuliwa hatua gani.
3) waliochoma makanisa znz tuamiwe kama wamekamatwa na kesi zao zinaendeleaje
4) Waliokuwa wnaandamana hovyo na kudai Znz yao...walioambatana na sheikh Farid wako wpi ma kesi zao zinaendeleaje?

Anonymous said...


Mungu Baba,

Damu ya watumishi wako isipotee bure bali iwe sababu ya mapatano na mshikamano kati ya wana wa Tanzania. Nakupenda Tanzania. Padre Mushi, RIP... Amina.

Anonymous said...

Toka awamu ya Nne Imeingia madarakani ni wachungaji na mapadre kuuawa tu kila kukicha. Halafu mnaambiwa kuweni watulivu.

Waislamu wataendelea kuua wakristo mpaka lini?