Tuesday, April 16, 2013

Mabomu Yalipuka Mjini Boston!

Second Bomb explosion at Copley Square

Wadau, leo mabomu yamelipuka mjini Boston wakati wa Boston Marathon. Yamelipuka karibu na ninapofanya kazi Copley Square. Yaani, ni bahati niko safarini Maryland kwa ndugu zangu,la sivyo ningekuwa huko kwenye eneo bomu lilipolipuka. Watu watatu wamekufa na zaidiya watu mia moja kuumia. Wengi wampoteza viungo kama mikono na miguu.  Watu walizuiliwa kuingia wala kuondoka kwenye majengo hadi saa 11 jioni.  Ulzini ni mkali sana. Yaani wana Boston wanalia kwa uchungu kitendo cha kigaidi kufanyika hapa!

Tumeambiwa ofisi imefungwa kesho kwa vile polisi bado wanafanya uchunguzi.

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

No comments: