Monday, April 29, 2013

Padri MKatoliki Afumaniwa na Mke wa Mtu!

 Wadau, lazima niseme kuwa nafahamu mapdri wa Kanisa Katoliki waliozaa watoto, wana mke na familia kabisa! Pia, nilipokuwa Daily News, mwandishi wa habari mwenzangu (marehemu) alikuwa anatamba kuwa alikuwa antembea na Sista wa Kanisa Katoliki. Anasema alipokuwa anakutana na yule sista anavua shela yake, wakimaliza anaivaa! Duh! Hapa Boston walikuta skeletons za watoto wachanga kwenye basement ya convent fulani!  Kanisa Katoliki inazuia mapadri kutokuoa maana wanakuwa na ashki kama watu wa kawaida.  Pia umesikia skandali ya mapari wa Kanisa Katoliki kuwafanywa watoto vibaya.  Jamani, hebu waruhusu kuoaAu wakatwe dhakari kabla ya kuwa padri!

***********************************Kutoka Global Publishers:


KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia ,katika kashfa nzito baada ya padri wake, Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtuFather Ngowi akiwa ameduwaa baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa mtu aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.

Sakata la fumanizi hilo linadaiwa kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita chumbani kwa padri huyo, Marangu Wilaya ya Moshi Vijijini ambako Father Ngowi inasemekana alikutwa ‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.

Pamoja na kunaswa huko, vyanzo havijaeleza humo chumbani wawili hao walikuwa wakifanya nini!

Habari zinadai siku ya tukio, mwanamke huyo aliingia nyumbani kwa padri huyo ambapo baadhi ya ndugu wa mumewe walikuwa wakimfuatilia baada ya madai yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu wenye maswali mengi na mtumishi huyo wa Mungu.

“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba Mama P na Father Ngowi wana ukaribu wenye maswali mengi, mume wake alifuatilia na kubaini ni kweli lakini akashindwa kuutenganisha ukaribu wao,” kilidai chanzo.


Father Ngowi akijaribu kuomba samahani baada ya kufumaniwa.

Chanzo kikaendelea kudai kwamba baada ya kuona mkewe amejikita kwa mtumishi wa Mungu, mumewe alinyoosha mikono juu na kumwachia Mungu.

Chanzo: Sasa siku hiyo baada ya ndugu wa mume kumfuatilia mpaka anaingia kwa Father Ngowi, wakaona ni bora watafute mpigapicha ili kupata picha za tukio ambazo zitakuwa ushahidi siku za mbele.

“Walipompata wakazama ndani, sekeseke likaanzia hapo. Walimkuta mwanamke huyo na mtumishi wa Mungu wapo kitandani.”


Father Ngowi na Mama P wakivaa nguo zao kwa aibu baada ya kufumaniwa.
Habari zinadai kwamba kufuatia tukio hilo, tayari Kanisa Katoliki limemweka kitimoto padri huyo ambaye alikuwa akihudumu katika Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishwa na kupelekwa Parokia ya Makomu, Marangu ambako inadaiwa ameshushwa cheo.

Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo, Father Ngowi alikana kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake lakini alipobanwa sana na mabosi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Moshi, alikiri na kudai ibilisi alimpitia na kuomba kanisa limsamehe na kutompa adhabu kali ambayo itamuathiri kisaikolojia.

Hili ni tukio kubwa na la aina yake kuwahi kulikumba Kanisa Katoliki nchini kwa padri wake kudaiwa kukutwa na mke wa mtu chumbani
Father Ngowi na Mama P wakiwa na nyuso za aibu baada ya tukio hilo.
Kuna madai kwamba mwaka jana (2012), Father Ngowi, mbele ya waumini wake alisoma barua yenye kukana shutuma zote zilizoelekezwa kwake kwamba amekuwa na ukaribu wenye maswali mengi na wake za watu.

Taarifa zilidai kuwa padri huyo aliweka wazi akisema si kweli kwamba amekuwa na ukaribu unaotajwa, akawataka waumini wake wapuuze tuhuma hizo alizosema zina mwelekeo wa kuchafua sifa yake na taswira ya Kanisa Katoliki kwa jumla.

Hayo ni madai ya vyanzo vyetu ambavyo viliambatanisha na picha mbalimbali za tukio hilo lenye kushtua waumini sambamba na namba za simu za padri huyo kwa ajili ya mawasiliano ili kujiridhisha.
Father Ngowi akipatiwa suruali yake.
poleni sana mtakao ghafilika ni taarifa tu wandugu.myie wanaume mnamuona mwenzenu? itikadi za kidini weka pembeni tuzungumze fumanizi!


************************************************************************
 
Father Urbanus Ngowi  photo from Catholicweb.comFather Urbanus Ngowi
 http://home.catholicweb.com/moshidiocese/index.cfm/NewsItem?ID=201906&From=Home
 

14 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Duh haya makubwa...tena mno ..ila nao ni binadamu labda waruhisiwe tu kuona kama waangalikana na dini nyingine...

Anonymous said...

Huyo Padri kazoea. Si mara yake ya kwanza kutembea na waumini wake!

Anonymous said...

Aibu kweli! Je, atsimamishwa Upadri?

mugaya said...

Hawezi kusimamishwa upadri watakachofanya ni kumpeleka jimbo jipya la mbali na hapo Kwani kanisa linawalinda sana mapadrii wake.Ila kwa kuwa wameshindwa kuzuia picha zake kutoka labda watamfukuza

emu-three said...

Asiye na dhambi, amuhukumu huyo padri.

`Tatizo ni ile hali ya kukubali majukumu kumbe huyawezi au sio?'

Anonymous said...

Alikuwa keshakula vitu au bado?

Anonymous said...

Aisei huyo Mama P mzuri kweli.

Anonymous said...

Ukute ana watoto kibao!

Anonymous said...


Ninapenda sana mapari hasa wa dini ya kikristu zisizowaruhusu waoe-waoe. Kwanza- mwanaume asiyerijali haruhusiwi kuingia upadri ili aweze kumudu kuhimili vishawishi. Lakini kwa sasa dunia imebadilika. Vishawishi ni vingi kwa Binadamu. wakiruhusiwa kuoa-itaondosha matatizo yaliyokuwa yanatokea na watoto wadogo na hii ya kufumaniwa na wake za watu, etc.

Biblia ni kitabu cha Mungu lakini Ulaya na marekani wameruhusu na kutambua ndoa za ushoga. Sisi tuachane na hayo pamoja kuwa ushoga na usagaji umeshamiri nchini-TUTAMBUE MAPADRI KUOA. Tukitambua hii Masista nao wataomba kuolewa. Unaweza kumcha Mungu hata ukiwa umeoa na ni mlokole, padri au sister. Kwani, mbona kuna watu wengi waliooa wange wengi ambapo ni wahuni pia hawatosheki kutokana na kujiendekeza na ngono? Pamoja na kuwepo HIV-mtu anajifanya hawezi kulala bila ya hiyo kitu ana vimada na huku ana wake zaidi ya 2. wapo wale ambao anatoka chumba cha mkewe anambaka mtoto wake mdogo chumba cha pili au housegirl.

Kuna haja pia ya kuwapa vijana mafunzo ya MAGOBE hapa chini kuhusu kujitambua, kujithamini, tujitunza, kuwa na malengo ya maisha na kujituma. Sex sio maisha. hii inawachanganya wanafunzi ambao huishia lodging, kuacha masomo akajikuta kadanganjwa na hata pale alipokuwa akipelekwa na bwana huyo kumbe sio nyumbani kwake kwa kumpata hana. Starehe ya sekunde chache sio maisha. Watu wawe na malengo na kuridhika na mmoja aliyemchagua. Hakuna mapendo sawa kwa mtu zaidi ya mmoja. Pia, ni kuharakisha maradhi ya kuambukiza hata kama si HIV yapo mengi hata kansa za aina mbalimbali.

Kuna haja ya wanaume kujua kuwa-kuna wanawake au wasichana wanatumika kumuaibisha mtu kutokana na chuki binafsi za audui. Kama anakuchukia kutokana na ushindani kibiashara, au vyovyote vile kwa vile una msimamo kikazi mlipo anakusukumizia msichana/mwanamke na fumanizi inapangwa. Mwanamke atakufuata mpaka unasema ngoja nifanyekitu sasa too much kujileta. Hapo mtandao unakula kazi unafumaniwa, unatoka gazetini wameandaa, unapigwa picha zinawekwa mtandaoni, anakuja na timu ya wajaza misuri wanakufanyia uchafu (sodomy) na kukupiga picha. Ukitaka picha zisitoke gazetini au mitandaoni wanasema uwape mamilioni ya pesa na kila wakati wanakutishia ili utoe hela. maisha yako yanakuwa duni na unaomba ufe. Kama si Padri unahama mji na biashara zako au unakimbia familia unatokomea. Tabia hii tulisimuliwa ktk tafiti mijini ushindani wa biashara au kugombania/kushindania wanawake. Kumuaibisha Padri inaweza kuwa pia ILIPANGWA. Upo mkoa mmoja kusini masuala haya ya kufumania na kutoa hela ni sehemu ya culture mama anatumwa kisha unalipa hela wanapata hela ya matumizi.

Utashangaa pia mtu anafuma message ya mapenzi ktk SM kisha anamwambia-tupange mpango niwafumanie kama unataka mimi na wewe tudumu ktk ndoa ama sivyo ondoka. Kisha mpango unafanyika wanakwenda na media, police wanafumaniwa, bwana anapigwa na kutumbukizwa bisibisi matakoni, anang'olewa meno na kufikishwa police. Yote hayo ya kipigo etc police yupo kisha wanafungiwa chumba tofauti police kesho wanaambiwa-wakayamalize kifamilia nje ya mahakama (Soma Risasi Newspaper front page an page 2 la 1-3 May, 2013). Huyu baba tony aliyefumania na mke wa rafikie ana ofisi ya Uhandisi. Unajiuliza-mbona mke hakupigwa. Alijua kaolewa kwa nini alikubali kushawishiwa? Je, kosa ni la mmoja tu? unapomfumania unampiga mwanaume tu? ujinga gani huu? Pengine mkeo ndio alikuwa kishawishi mkubwa vipi adhabu ya Mwanaume Padri au Si Padri. Ipo namna pande zote 2 ziadhibiwe au ziache kuadhibiwa. Tuache ujinga na kuoneana

Anonymous said...

Halafu hawa watumishi wa mungu wanafaidi sana kwa sababu wanawajengea waumini hofu na kujifanya watakatifu halafu wanajimegea taaratibe hebu we imagine huyo father alikua anajimegea wake za watu kwa mda gani inawezekana ni miaka kibao na akisimama pale madhabauni wakati anaubiri labda zaidi ya nusu ya wanawake hapo kanisani anakua ameshajitafunia na yeye kazi yake ni kuchagua tu ajitafunie yupi.

Mimi huaga nina principal moja simwamini binadamu yeyote hata ajiite nabiii lakini naamini kuna mungu lakini hii ya kusema eti mke aende kanisani sijui misa za jioni sijui padre kamwita hiyo kwangu ni No.

Hivi yule padre Kimaro na ile kesi ya kitoto iliishia wapi?

Anonymous said...

Mmh Father Ngowi ana milonjo embu angalia miguu ilivo membamba..sijui aliwezaje kuisimamia ngoma kubwa kama iyo?,lol!

Anonymous said...

Nakubaliana na anony May 02, 2013 7:21 AM. Mama P ni janajike la nguvu. Hata mimi uzalendo ungenishinda.

Anonymous said...

nyie ndugu wa mume ningewaona wa maana kama mngeenda kufumania mwalimu wa shule anayosoma mwanao kama anafundisha au la? hilo ndio jukumu lako peleka kamera shule uhakikishe mwanao anafundishwa mtuondolee janga la taifa la division ziro badala yake mtu mzima bila aibu unaenda chumbani kwa watu wazima wanaofanya zinaa kurekodi hao ni watu wazima wameamua kufanya mapenzi nyinyi kinawakwanza nini? mume wa mtu ameshasema amenyanyua mikono kanisa linaendelea na kesi nyinyi msiokua na kazi kimbelembele kuchungulia ngono inafanyweje acheni ujinga watu wazima ovyoo ukiulizwa daftari la mwanao hujui linafananaje lakini unajua kila mwanamke alielala na padri mxiuuuu nyinyi ni wasafi kiasi gani mpaka mkafumanie mwenzenu, hao mnaowafumania wote ni watu wazima wanajua wanachokifanya nyie kinawauma nini? kuona wanafurahia uroda? acheni ujinga wa kuvuana nguo magazetini hivi mngesema tu kafumaniwa mngepungukiwa nini mpaka kufikia mnaweka picha za utupu wa watu wazima magazetini? acheni ujinga wenu hapo mnao watoto nyumbani wameshinda njaa nyinyi akili kufumania hebu fanyeni mambo ya maendeleo kafumanie kama mwalimu wa mtoto wako anafundisha darasani au vipi? halafu mnashangaa watoto wanapata division o kumbe wazazi ujinga kufata wapenzi chumbani ovyooo akili zenu sifuri

Anonymous said...

HATA KAMA AMEFANYA HILO KOSA, NYIE NI NANI MNAOMCHAFUA NA KUMWANIKA HADHARANI KWA LENGO LA KUFANYA BIASHARA ZENU NA WAKATI WENGINE WENU NI WACHAFU NA WAHUNI MARA MIA KULIKO HATA HUYU PADRI?????? AFADHALI HATA MNGEANDIKA TU HABARI NA SIYO KUMWEKA HADHARANI HIVI !! HATA YESU MWENYEWE ALIWAAMBIA WALE WATU "" AMBAYE HANA DHAMBI NA AWE WA KWANZA KUMTUPIA JIWE""" KUMBE WOTE WALIKUWA WAOVU!!! SHAME ON YOU!!!! I HATE THIS FOR REAL !!