Friday, April 19, 2013

Tuko Hoi Boston, Polisi Wametuambia Tukae Ndani!

Wadau, nimeamshwa na simu kutoka Emergency Alert ya mji wa Cambridge , MA wakisema kuwa ni maarufu kutoka nje ya majumba yetu leo! Hakuna usafiri, wameomba sehemu za kazi zisifungue!

Wadau, jana usiku ilikuwa balaa hapa Cambridge! Cambridge ni nje ya Boston.  Kwanza kwenye saa tatu na nusu (9:30PM) tulisikia kuwa majambazi walivamia duka la  7-11 Central Square!

 Kukaa kidogo tukasikia Polisi kapigwa risasi Chuo Kikuu cha MIT! Baada ya muda mfupi wakasema yule polisi kafa!

Kwenye saa Tano tukasikia Mtu kaibiwa gari yake aina ya Mercedes Benz, kwenye kituo cha mafuta!  Ni mwendo mfupi toka napokaa! Nikaanza kusikia milio ya gari ya polisi!

Kumbe polisi wa kila aina, walikuwa wanawafukuza  Karibu na Arsenal Mall milio ya risasi balaa, ambulance na magari ya polisi yalikuwa yanafukuzana, kwenye TV, tukaona kila mtu aliyefannana na Mspanish, mwarabu kasimamishwa na kusachiwa!

Sikulala hadi saa nane na nusu! Nimeamshwa na simu ya Emergeny Alert! Duh, hii ni kama SINEMA!

Wanasema huyo gaidi wanayetamfuta anaitwa Zohkar Sarnev  mwenye miaka 19, anatoka Chcchnya!

1 comment:

Anonymous said...

Pole sana, Da Chemi. Hiyo ndio the US of A.